Somo: Kushinda Vita Dhidi ya Maadui wa Kiroho Kupitia Maombi
I. Utangulizi: Hali Halisi ya Vita Ilivyo
Kabla ya kuanza kufundisha, ni muhimu washiriki waelewe kuwa wokovu haumaanishi mwisho wa vita, bali ni mwanzo wa vita vipya dhidi ya ufalme wa giza. Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro WhatsApp +255710889892
- Andiko Kuu:✍๐พ Waefeso 6:12 – "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
- Fundisho:✍๐พ Vita vyetu si dhidi ya binadamu wenzetu, bali ni dhidi ya nguvu zisizoonekana.
II. Adui wa Kwanza: Shetani na Majeshi ya Giza
Huyu ndiye adui wa nje anayetumia hila, mashaka, na vitisho kumrudisha mwamini nyuma.
- Andiko: ✍๐พ1 Petro 5:8 – "Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze."
- Mbinu ya Kumshinda✍๐พ: Yakobo 4:7 – "Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia."
- Msisitizo kwa Kanisa:✍๐พ Kumshinda Shetani kunahitaji utii kwa Mungu kwanza (nidhamu ya kiroho), kisha kusimama imara kumpinga kwa Neno.
III. Adui wa Pili: Mwili (Asili ya Dhambi)
Huyu ni adui wa ndani. Ni tamaa zinazoinuka ndani ya moyo wa binadamu zinazopingana na Roho wa Mungu. Huu ndio adui hatari zaidi kwa sababu hahitaji mwaliko wa nje.
- Andiko✍๐พ: Wagalatia 5:17 – "Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnavyotaka."
- Mbinu ya Kumshinda:✍๐พ Wagalatia 5:16 – "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."
- Msisitizo kwa Kanisa:✍๐พ Mwili haukemewi kama pepo; mwili unasulubiwa kwa kuishi maisha ya kujikana na kutawaliwa na Roho Mtakatifu.
IV. Adui wa Tatu: Ulimwengu (Mifumo ya Kidunia)
Huyu ni adui wa mazingira. Ulimwengu hapa ni mfumo wa kifikra, mavazi, mazungumzo, na tabia zinazomfanya mtu aone kuwa kumcha Mungu ni jambo la kizamani au lisilo na thamani.
- Andiko✍๐พ: 1 Yohana 2:15 – "Msiupende ulimwengu, wala mambo yaliyomo katika ulimwengu. Mtu akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake."
- Mbinu ya Kumshinda: ✍๐พWarumi 12:2 – "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu."
- Msisitizo kwa Kanisa: ✍๐พUshindi dhidi ya ulimwengu unaanza kwenye nia (mindset). Lazima ubadili namna unavyofikiri ili usimezwe na mifumo ya kidunia.
V. Hitimisho: Silaha na Ushindi Wetu
- Andiko:✍๐พ 2 Wakorintho 10:4 – "Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome."
- Maombi ya Kufunga:✍๐พ Omba hivi Baba nipe macho ya Rohoni nione Vita niwezekuwa mshindi KATIKA Jina la Yesu. Ameen
Share SOMO hili nzuri
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni