Jumanne, 28 Aprili 2026

SOMO;AINA ZA UBATIZO

SOMO: AINA ZA UBATIZO, FAIDA NA MAANDIKO

Karibu Mtu Wa Mungu Tujifunze Kwa Ufupi Aina Za Batizo Kwa Maandiko Na Faida Sake Somo hili linakupa manga kujiuliza Umebatizwa Kwa Maji mengi Ubatizo ni ishara ya utii  na Ukamilishaji Wa Ukristo Ni Vizuri Ukiokoka Tu Upate Mafundisho Ya Kukuze Kiroho Kisha Ubatizwe Kwa Maji mengi Nitaruhusu Maswali inbox ili kujifunza Said
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
WhatsApp+255710889892

1. UBATIZO WA MAJI (UBATIZO WA TOBA)


• Mstari:✍🏾 Matendo ya Mitume 2:38 - "Petro akawaambia, Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu..."

• Faida: ✍🏾Ni ushuhuda wa nje wa toba ya ndani, ondoleo la dhambi, na utambulisho wa kufa na kufufuka pamoja na Kristo.


2. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU


• Mstari: ✍🏾Matendo ya Mitume 1:8 - "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu..."

• Faida✍🏾: Kupokea nguvu ya kiungu kwa ajili ya huduma, ushuhuda wenye ujasiri, na kuongozwa katika kweli yote.

3. UBATIZO WA MOTO (UTAKASO NA MAJARIBU)


• Mstari:✍🏾 Mathayo 3:11 - "...yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto."

• Faida:✍🏾 Kutakaswa kwa tabia (kama dhahabu ipitishwavyo kwenye moto), kuimarishwa kwa imani, na kuondolewa kwa makapi ya kidunia ndani ya mwamini.

HITIMISHO

Ubatizo ni lango la kuingia katika maisha ya utii. Kama waliookoka, tunafuata Ubatizo wa Maji mengi (kwa kuzamishwa) kama hatua ya kwanza ya utii baada ya kuamini, na tunatafuta Ubatizo wa Roho Mtakatifu ili kupata nguvu ya kuishi maisha ya ushindi.

Jumatatu, 27 Aprili 2026

SOMO:IBADA YA NYUMBANI

SOMO: IBADA YA NYUMBANI (MADHABAHU YA FAMILIA)
AGIZO LA KI MUNGU TUTAANZISHA MADHABAHU YA NYUMBANI KUANZIA LEO FATA MAELEKEZO KATIKA SOMO HILI

​1. UTANGULIZI

​Ibada ya nyumbani si mkutano wa kidini tu, bali ni kitendo cha kuweka wakfu nyumba na maisha ya kila siku chini ya mamlaka ya Mungu. Ni mahali ambapo familia inakutana na Mungu wao nje ya mazingira ya kanisani.. Ni Muhimu Nyumbani Tuwe na Ibada Familia Tuwe Tunakusanyika kabla Ya Kulala Tusali Pamoja Tutege Muda maalumu kuimarisha Madhabahu ya Nyumbani Tutakuwa Tunatoa na Sadaka Na Kila Jumapili Jioni KIONGOZI Atanipigia Naiombea Madhabahu Hiyo ya Nyumbani. 

NENO LINADHIBITISHA

​Zaburi 127:1 — "Bwana asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure."
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
ZINGATIA HAYA;

1:Tutatenga Muda Wa Ibada Maalumu Tutumie Muda mfupi Sana Dakika 15 au 10

2;Kiongozi Wa Maombi Ni Wewe Mwanangu uliye Kwenye Group Unapoishi Anzisha IBADA ya Familia. 

3:Kila Jumapili Kiongozi Atanipigia Anaweka Raoud Spika Naiombea Madhabahu ya Familia na Wana familia Wote Kwa Muda Wenu Huko Wa Maombi. 
4:Ibada Tutakuwa Tunatoa Sadaka Tunazikusanya Ili Watoto wazoe kutoa na Jumapili Ninapomaliza Kuwaombea Tutatoa Nitaombea na Mahitaji Yenu ya Ki familia. 

5;Kukiwa na SHIDA Kiongozi utanipigia kwa ushauri na Maelekezo ya KIROHO Usiwe Mbali na Askofu Richard Kila hatua ili kuimarisha Familia Zetu Pigs+255759861768 au +255710889892 Kiongozi Tu utanipigia kuwasilisha shida za familia mtakaomba. 


​2. UMUHIMU WA IBADA YA NYUMBANI KATIKA FAMILIA ZETU

➖​Urithi wa Kiroho:✍🏾 Ni darasa la kwanza kwa watoto na vijana kujifunza kumcha Mungu (Kumbukumbu la Torati 6:6-7).

​➖Ulinzi wa Kiroho:✍🏾 Inatengeneza mazingira ya uwepo wa Mungu yanayozuia roho za uharibifu kuingia kwenye familia.

​➖Umoja wa Familia✍🏾: Inasaidia kuondoa migogoro na kuleta upendo kwani familia inayoomba pamoja, hukaa pamoja.

​➖Kukua kwa Kanisa: ✍🏾Kanisa imara linajengwa na familia imara. Nyumba ikiwa na moto wa maombi, kanisa litawaka moto.pia tutaweka ukuta Wa moto hatutasumbuliwa. 


​3. FAIDA ZA IBADA YA MAJUMBANI


​➖Amani na Furaha:✍🏾 Uwepo wa Mungu unapoingia ndani ya nyumba, huzuni na hofu vinaondoka (Zaburi 16:11).


​➖Maelekezo ya Kiungu: ✍🏾Mungu anapata nafasi ya kusema na familia kuhusu maamuzi yao ya kila siku (Biashara, Masomo, Afya).


​➖Kujenga Imani: ✍🏾Kupitia kusoma neno, waumini wanakuwa na ufahamu wa kina wa maandiko.

​➖Uponyaji na Baraka:✍🏾 Ni mahali ambapo wagonjwa ndani ya nyumba wanaweza kuombewa na baraka za kiuchumi kutamkwa.


​4. NAMNA YA KUIFANYA IBADA YA MAJUMBANI (MIONGOZO RAHISI KWENDA NAYO)

​Ili kuifanya ibada hii iwe endelevu na isichoshe, waumini wanashauriwa kufuata hatua hizi:

➖​Chagua Muda Maalum: ✍🏾Panga muda ambao kila mtu yupo nyumbani (asubuhi na mapema au kabla ya kulala).

➖​Usiwe na Muda Mrefu Sana: ✍🏾Dakika 15 hadi 30 zinatosha ili kuwafanya watoto na watu wenye ratiba ngumu wasichoke.

​➖Shirikisha Kila Mtu:✍🏾 Badilishana majukumu; leo baba aongoze, kesho mama, keshokutwa kijana au mtoto. Hii inajenga ujasiri Katika Familia Yako


​UTARATIBU WA IBADA YA MAJUMBANI TUTAKAVYOOMBA 

Tutaenda Na Utaratibu huu Wa kuendesha ibada zetu. baada ya Kukusanyana

​➖Sifa na Kuabudu:✍🏾 Wimbo mmoja au miwili ya kumtukuza Mungu.


➖​Neno la Mungu: ✍🏾Soma kifungu kimoja cha Biblia na kutoa maelezo mafupi (Sio mahubiri marefu).

➖​Shuhuda/Mahitaji:✍🏾 Ulizana kama kuna mwenye hitaji au jambo la kumshukuru Mungu muombeane Mahitaji kila Mtu aandike Kwenye karatasi. 
Jumapili ninapowaombea mnayashika nayaombea.

​➖Maombi: ✍🏾Ombea familia, Kanisa, Taifa, na kazi za mikono yenu na Mchungaji

​➖Baraka: ✍🏾Kiongozi anatamka baraka juu ya nyumba.


​5. MISTARI YA BIBLIA YA KUTUMIA KATIKA IBADA YA MAJUMBANI

➖​Joshua 24:15 — "Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana."

​➖Mathayo 18:20 — "Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao."
➖​Mithali 22:6 — "Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee."

➖​Matendo 2:46-47 — "Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba..."

➖​Wakolosai 3:16 — "Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni..."

              HITIMISHO

Ibada ya nyumbani ndiyo "Betheli" (Nyumba ya Mungu) ndogo. Ukianza leo, utaona mabadiliko makubwa katika tabia za watoto wako na ustawi wa nyumba yako. Mungu Akubariki Mtoto Wa Mungu Kwa Kulichukua Kwa Uzito Kuanza rasimi ibada ya familia leo.

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania
Madhabahu Ya Moto Wa Yesu
Nipo Morogoro Vera Dakawa
Ndiye Kiongozi na Muasisi Wa Magroup yote matatu Maombi na Mafundisho Madhabahu ya Kwenye Group imekuwa Baraka Kwa Wengi Sana. 

WhatsApp Yangu +255710889892

SOMO;USALAMA WA KIROHO

SOMO: USALAMA WA KIROHO(Spiritual Security)

​Utangulizi

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro. 
Karibuni Katika Somo nzuri
​Usalama wa kiroho ni hali ya kuwa ndani ya ulinzi wa Mungu bila kutoa mwanya wowote kwa adui (shetani) kupata mlango wa kuingia kwenye maisha yako. Kama vile tunavyolinda nyumba zetu kwa mageti na walinzi, roho zetu zinahitaji ulinzi dhidi ya mashambulizi ya kiroho.


​1. Misingi ya Usalama wa Kiroho

​Ili uwe salama, lazima uwe na misingi imara inayokulinda na mishale ya adui:

➖​Wokovu✍🏾: Huu ndio ukuta wa kwanza. Bila kuwa ndani ya Kristo, hauna mamlaka ya kisheria ya kupinga mashambulizi ya giza

​➖Neno la Mungu✍🏾: Neno ni taa na silaha. Linakupa maarifa ya kujua mbinu za adui.
​"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa." (Hosea 4:6)

➖​Utii✍🏾: Maisha ya dhambi yanatengeneza matundu kwenye ukuta wako wa ulinzi. Utii unaziba mianya hiyo.


​2. Silaha za Kulinda Usalama Wako (Waefeso 6:11-18)

​Biblia inatupa "Vazi la Kinga"  ambayo kila mwamini anapaswa kuivaa kila siku:
Vazi hili Paulo Amefafanua Hivi Mtu Anatakiwa awe Hivi;

➖M​Kweli: ✍🏾Kuishi maisha ya uaminifu na bila unafiki.


➖Mtu Wa ​Haki: ✍🏾Dirii ya kifuani inayolinda moyo wako dhidi ya shutuma za adui.

➖​Injili ya Amani:✍🏾 Utayari wa kutumika na kufuata njia za Mungu.

➖​Imani: ✍🏾Ngao inayozima mishale ya moto ya yule mwovu.

​➖Wokovu:✍🏾 Chapeo inayolinda fikra na akili zako.

➖​Neno la Mungu✍🏾: Upanga wa Roho kwa ajili ya kushambulia na kujihami.


​3. Mambo Yanayovunja Usalama wa Kiroho (Mianya)

​Adui mara nyingi hapiti ukutani, bali anapita mlangoni. Jilinde na mambo haya:

➖​Hasira na Kinyongo: ✍🏾Biblia inasema usimpe Ibilisi nafasi kupitia hasira (Waefeso 4:26-27).

➖​Kutoomba✍🏾: Maombi ni mfumo wa mawasiliano na ulinzi (Radar). Ukikaa bila kuomba, unakuwa "blind" kiroho.

➖​Kushirikiana na Maovu✍🏾: Mazingira au marafiki wanaokuvuta mbali na Mungu wanadhoofisha kinga yako.

​4. Jinsi ya Kudumisha Usalama wa Kiroho Kila Siku


➖​Saa za Maombi: ✍🏾Tenga muda maalum wa kuimarisha roho yako (mfano: Maombi ya Alfajiri au Saa za Mfungo).

​➖Kutamka Neno:✍🏾 Usalama wako unategemea pia unachokiri. Tamka ulinzi wa Mungu juu ya maisha yako, familia, na kazi zako.
​Zaburi ya 91: Ifanye kuwa wimbo wako wa ulinzi. Inatukumbusha kuwa anayekaa chini ya uvuli wa Mwenyezi atakaa salama.

FAIDA ZA USALAMA ROHONI

1. Amani ya Ndani Inayopita Fahamu


​Unapokuwa na usalama wa kiroho, huna hofu ya ghafla wala wasiwasi juu ya kesho. Moyo wako unakuwa na utulivu hata katikati ya dhoruba.


  • Mstari: "Amani nawaachieni; amani yangu nawapa... Misifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na hofu." (Yohana 14:27)

​2. Ushindi Dhidi ya Mishale ya Adui


​Usalama wa kiroho unakupa uwezo wa kuizima mipango yote ya adui kabla haijakudhuru. Unakuwa kama mji wenye kuta imara ambapo adui hawezi kupenya.


  • Mstari: "Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote ya moto ya yule mwovu." (Waefeso 6:16)

​3. Uhakika wa Kusikiwa Maombi Yako


​Mtu aliye salama kiroho ana uhusiano mzuri na Mungu (Open Heaven). Hii inafanya maombi yake yawe na nguvu na majibu ya haraka kwa sababu hakuna kizuizi kati yake na Mungu.


  • Mstari: "Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia." (1 Yohana 5:14)

​4. Ujasiri na Kujiamini (Boldness)


​Usalama wa kiroho unakuondolea roho ya uoga. Unasimama kwa ujasiri mbele ya changamoto, ukijua kuwa aliye ndani yako ni mkuu kuliko mazingira yanayokuzunguka.


  • Mstari: "Wabaya hukimbia wasipofuatwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba." (Mithali 28:1)

​5. Kutembea Chini ya Ulinzi wa Malaika


​Unapoweka usalama wako kwa Mungu, Yeye anaamuru jeshi la mbinguni kukulinda katika njia zako zote, ukitembea bila hofu ya kutegwa au kuanguka.

  • Mstari: "Kwa kuwa atakuagizia malaika zake, wakulinde katika njia zako zote." (Zaburi 91:11)

​6. Kupata Pumziko la Kweli

​Dunia imejaa mambo ya kuchosha, lakini usalama wa kiroho unakupa mahali pa kukimbilia na kupata nguvu mpya (spiritual recharging).

  • Mstari: "Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama." (Mithali 18:10)

​7. Kinga Dhidi ya Laana na Mashambulizi ya Maneno


​Mtu aliye salama kiroho hawezi kurogeka wala kuharibiwa na maneno ya watu, maana ulinzi wa Mungu unakuwa kama kitalu kinachomzunguka.


  • Mstari: "Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya Israeli." (Hesabu 23:23)


​Hitimisho

​Usalama wa kiroho si tukio la mara moja, ni lifestyle (mfumo wa maisha). Unapokuwa karibu na Chanzo (Mungu), unakuwa mbali na hatari Mbali Mbali za Kiroho

​Mstari Wa Kusimamia: "Mpingeni Ibilisi, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi." (Yakobo 4:7-8)

Shirikisha Baraka Hizi na Wengine

Jumapili, 26 Aprili 2026

MAJINA YA KIKE NA MAANA YAKE

​MAJINA YA LIKE NA MAANA YAKE. 

Chunguza Jina lako Yamkini lipo ambaye Yupo Muunge Kwenye Group letu la Maombi na Mafundisho lilopo chini Ya Pastor Richard Wa Morogoro

1. Majina ya Kiswahili (Yenye Maana Nzuri)

​Majina haya yanatokana Na Wahega waliita kutokana na Msingi Wa Tukio


  • Amani – Utulivu na usalama.

  • Baraka – Zawadi kutoka kwa Mungu.

  • Faraja – Tulizo la moyo.

  • Lulu – Kitu cha thamani kubwa (vito).

  • Neema – Upendeleo usio na malipo.

  • Sifa – Shukrani au utukufu.

  • Tumaini – Matarajio mema.

  • Zawadi – Kitu kilichotolewa kwa upendo.

​2. Majina ya Kibiblia (Kiroho)

​Majina Haya Yalitokana Msingi Wa Imani Ya Kikristo Katika Biblia

  • Abigaeli (Abigail) – Furaha ya baba.

  • Bethania (Bethany) – Nyumba ya tini (mahali ambapo Yesu alipenda kupumzika).

  • Daniela (Daniela) – Mungu ni mwamuzi wangu.

  • Edeni (Eden) – Bustani ya furaha na anasa.

  • Elisheba (Elizabeth) – Mungu ni kiapo changu.

  • Hadassa (Hadassah) – Jina la Kiyahudi la malkia Esta (mti wa mirtoli).

  • Sela (Selah) – Pumzika na utafakari.

  • Talitha – Msichana mdogo (kutoka maneno ya Yesu: "Talitha kumi").

​3. Majina ya Kisasa na ya Kipekee 


Haya ni Majina Msingi Wake Ulitokana na Upekee Wa Mzazi Kumpata mtoto huyo
  • Brianna – Mwenye nguvu na heshima.

  • Clara – Mwenye kung'ara au mwangaza.

  • Eliana – Mungu amejibu.

  • Gianna – Mungu ni mwenye neema.

  • Ivanna – Zawadi ya Mungu.

  • Melody – Wimbo mtamu.

  • Naila – Mwenye kufanikiwa au kufika mbali.

​4. Majina ya Maua 


Haya msingi wake ulitokana na Maua yanayovutia Wakatoa Majina
  • Dahlia – Aina ya ua zuri.

  • Jasmine – Ua lenye harufu nzuri sana.

  • Rose / Rozina – Ua la waridi.

  • Zuri – Mzuri (kwa sura na tabia).

Kama Umebarikiwa Na Somo hili Waunge na Wengine wazidi kupata Vitu Vizuri Ndani Ya Group

Bonyeza Link hii Ujiunge na Group la Mafundisho na Maombi
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
https://chat.whatsapp.com/L4PQijdjZqQ2P1sYKYYPqe?mode=gi_t

Jumamosi, 25 Aprili 2026

MASWALI na MAJIBU YA BIBLIA

SUNDAY SCHOOL KANISANI LEO

KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Nipo hapa Tujifunze Biblia Kupitia MASWALI NA MAJIBU YAKE

1;Swali: Je! Kabila la Yuda liliishi eneo gani la Palestina baada ya uhamisho?

Jibu: Yudea

2;Swali: Yesu alifufuka kutoka wafu siku gani?

Jibu: Siku ya tatu

3:Swali: Ni kundi gani ambalo lilikuwa baraza la watawala la Wayahudi lililopanga mauaji ya Yesu?

Jibu: Sanhedrini

4;Swali: Je! Biblia ina sehemu na migawanyiko mingapi?
Jibu: 8

5;Swali: Ni mito ipi miwili inayopakana na Edeni katika Iraq ya kisasa?
Jibu: Tigress na Frati

6;Swali: Utatu ulifunuliwa lini?

Jibu: Wakati wa ubatizo wa Yesu


UFAFANUZI WA MAANDIKO KATIKA MAJIBU HAYA NILIYOKUPA Unaletwa na Pastor Richard Wa Morogoro Katika Kuchambua Biblia

1. Eneo la Yuda (Yudea) Baada ya Uhamisho
​Baada ya kurejea kutoka utumwani Babeli, eneo waliloishi liliitwa Yudea.


​Ezra 5:8: "Mfalme na ajue ya kuwa tulikwenda katika wilaya ya Yudea, mpaka nyumba ya Mungu mkuu..."


​Mathayo 2:1: "Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Yudea, zamani za mfalme Herode..."


​2. Siku ya Kufufuka kwa Yesu
​Biblia inathibitisha mara nyingi kuwa Yesu alifufuka siku ya tatu.


​1 Wakorintho 15:4: "...na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko."


​Luka 24:46: "Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu katika wafu."


​3. Baraza la Sanhedrini

​Ingawa jina "Sanhedrini" ni neno la Kiyunani linalomaanisha "Baraza," Biblia inawataja kama wazee, wakuu wa makuhani, na waandishi walioketi pamoja kutoa hukumu.


​Luka 22:66: "Hata kulipokuwa mchana, baraza la wazee wa watu, wakuu wa makuhani na waandishi, walikutana; wakamleta katika baraza lao (Sanhedrini)..."

​Mathayo 26:59: "Basi wakuu wa makuhani na baraza lote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua."


​4. Migawanyiko 8 ya Biblia


​Kitaalamu, Biblia hugawanywa katika sehemu kuu mbili (Agano la Kale na Jipya), lakini
 migawanyiko ya vitabu ndani yake hufikia 8:



​Agano la Kale (5): Sheria (Torati), Historia, Mashairi, Manabii Wakuu, na Manabii Wadogo.


​Agano Jipya (3): Injili na Matendo, Nyaraka (za Paulo na za Jumla), na Unabii (Ufunuo).

​Luka 24:44: (Yesu akirejelea migawanyiko ya kale): "...katika Sheria ya Musa, na katika Manabii, na katika Zaburi."


​5. Mito ya Edeni (Tigris na Frati)

​Mito hii inatajwa tangu mwanzo wa uumbaji.


​Mwanzo 2:14: "Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli (Tigris); ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati."


​6. Ufunuo wa Utatu Mtakatifu

​Wakati wa ubatizo wa Yesu, nafsi zote tatu zilijidhihirisha kwa pamoja: Mwana (anabatizwa), Roho Mtakatifu (akishuka kama hua), na Baba (sauti kutoka mbinguni).


​Mathayo 3:16-17: "Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini... akaona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye."

Ubarikiwe Mwana Wa Mungu

SOMO;MUNGU ANACHUKULIA NADHIRI KWA UZITO

​SOMO;MUNGU ANAICHUKULIA NADHIRI KWA UZITO SANA;


Nadhiri ni Kiapo cha Nafsi Ya Mtu na Mungu. Pasipo Kulazimishwa au Kushurutishwa Anaweza Kuweka Akiwa Peke yake Anakuja Kumpa Taarifa. 
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

Madhara Makubwa Huwa Pale Usipotaka Kuitengua Nadhiri Yako. Jamani Nadhiri Usipoiondoa Huwa Mbaya Sana

Haya Maandiko Yanatuongoza Hebu Tuyasome Mwanangu. 

Mbaya ni Wale Watu Wanaosema Baba Niombee Nikipata Kazi Sitaacha Madhabahu Hii Kutoa Zaka Akishapata Kazi Hufanyii Kazi. 

Tuwe Makini Na Vinywa Vyetu Tusiwe Tunaweka Nadhiri Mgumu mfano unasema nikipata Kazi nitajitoa kwa wahitaji kila mwezi mshahara Wenyewe ukija kuugawa unashindwa kutembea na Nadhiri Hiyo

Acha Kukurupuka Kuweka Nadhiri


1. Umuhimu wa Kutimiza Nadhiri Kwa Wakati



  • Mhubiri 5:4-5: "Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hana furaha na wapumbavu; iondoe hiyo uliyoinadhiri. Ni afadhali usiweke nadhiri, kuliko kuiweka usiondoe."

  • Zaburi 50:14: "Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; mtimizie Aliye Juu nadhiri zako."

  • Zaburi 66:13-14: "Nitaiingia nyumba yako na sadaka za kuteketezwa, nitakutimizia nadhiri zangu, ambazo midomo yangu ilizisema, na kinywa changu kilizinena, nilipokuwa katika shida."

​2. Nadhiri ni Hiari lakini ni Lazima Itimizwe



  • Kumbukumbu la Torati 23:21-23:

  • "Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, atauliza kwako hakika; nayo itakuwa dhambi kwako. Lakini ukijizuia usiweke nadhiri, haitakuwa dhambi kwako. Yaliyotoka midomoni mwako yashike na kuyatenda..."

​3. Tahadhari ya Kukurupuka


  • Mithali 20:25: "Ni mtego kwa mtu kusema kwa haraka, Kitu hiki ni kitakatifu, na baada ya kuweka nadhiri kuanza kuuliza-uliza."

​4. Mifano ya Nadhiri Katika Biblia


  • 1 Samweli 1:11 (Hana): 

  • "Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako... na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mwanamume, ndipo mimi nitakapomtoa kwa Bwana siku zote za maisha yake..."

  • Mwanzo 28:20-22 (Yakobo): 

  • "Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami... basi hili jiwe nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi."

HITIMISHO

Usiichukulie Kimzaha Nadhiri Sababu Inatesa Sana Utawapa Kazi Kuanza Wachungaji Kuvunja roho Kuvunja laana Kumbe Siyo Laana Ni Nadhiri Kunawengine Anapitia Matatizo Yaliyosababishwa Na Nadhiri. 

Jiseach Ndani Yako Ujiangalie Nadhiri Ambayo uliweka Uliendoa

Ijumaa, 24 Aprili 2026

SOMO:MAOMBI YA KAMBI YA MATESO

SOMO;MAOMBI YA KAMBI YA MATESO KUJIONDOA HUKO UNAPOTESEKEA

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
WhatsApp+255710889892


​Kambi ya Mateso ni Nini?

​Kambi ya mateso kiroho ni hali ya "kufungwa" (spiritual captivity). Ni mahali ambapo adui anashikilia hatima ya mtu, uchumi wake, afya yake, au ndoa yake ili asione nuru ya mafanikio.

MAMBO YA KUZINGATIA HAYA MAOMBI

. A) Usiombe Ukiwa Hujui Eneo Ulipowekwa mateka au unachoteswa nacho Muda mrefu

. B) Usiombe Ukiwa Umecho hii ni Vita ya Kiroho. 

C) Utaanza na Toba na Utafata hatua nilizoelekeza BILA Kukosea utasimama na MISTARI niliyokuwekea 

D) Utaomba Siku 5 Na Utayatolea Sadaka Yako Nzuri Unajua Sadaka Ndio inaenda kuleta Nguvu ya Kuvunja mamlaka Ya Kafara zao na miungu yao inayokutesa. 
E) Utayawekea Muda Uliotulia Utaomba BILA Kupishanisha Muda. 


​2. Mistari ya Kusimamia (Silaha za Vita)


​Isaya 49:24-25 (Uhakika wa Ukombozi):
​"Je! Aliyepata mateka aweza kunyang’anywa mateka yake? Au yeye aliyetekwa na mwenye nguvu aweza kuponyoka? Lakini Bwana asema hivi, Hata mateka yake aliye na nguvu atanyang’anywa, na mateka yake aliye dhalimu ataponyoka..."


​Zaburi 107:14-16 (Kuvunja Milango yao):
​"Aliwatoa katika giza na kivuli cha mauti, akavunja vifungo vyao... Maana amevunja milango ya shaba, amekata mapigo ya chuma."


​Obadia 1:17 (Kumiliki Milki Yako):
​"Lakini katika mlima Sayuni watakuwako wale... 


NAMNA YA KUOMBA MAOMBI HAYA FATA  MTIRIRIKO NA MAELEKEZO HAYA
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

1. Kuharibu Ngome na Kambi za Adui

​Hii ni hatua ya Kwanza Tutaomba hivi Kuagusha Ngome Zinazokutesa. 
Mfano;Madeni Hii ni Ngome Mfano huolewi hii ni Ngome mfano hupati Kazi magonjwa Nk

Utatamka Maneno "Naagusha Ngome Naagusha Ngome ya madeni Ngome ya Kutokuolewa utatulia kwenye Kuagusha Ngome inayokutesa 
. Utaomba huku unatembea Utafanya ishara ya Kuagusha Unakaza Maneno. 

MWANANGU Simama hii misitari rudia Rudia kuisoma

​2 Wakorintho 10:4 – "Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome."


​Zaburi 68:1-2 – "Mungu na ainuke, adui zake wapanyanyike, nao wamchukiao wakimbie mbele zake. Kama moshi upeperushwavyo, ndivyo uwapeperushe..."


​Yeremia 51:20 – "Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme."


​2. Kukombolewa Kutoka Utumwani (Kambi ya Mateso)

​Hapa Utaomba hivi Ninatoka utumwani Mimi Richard utajitaja Jina Halafu unatamka Utumwa unaokutesa kama unamuombea Mtu naye utaelekeza kwa kumtaja Jina unasema hivi mfano: Mchumba wangu Richard namtoa kwenye Utumwa Wa Uchumi akapate mahari akanitolee Katika Jina la Yesu. Unatulia Kwenye Kuwa unamtoa Utumwani tu. 


MWANANGU HAPA SOMA MISTARI RUDIA RUDIA

​Isaya 49:24-25 –
24 "Je! aliyepata mateka aweza kunyang'anywa mateka yake? Au yeye aliyetekwa na mwenye nguvu aweza kuponyoka? 

25;Lakini Bwana asema hivi, Hata mateka yake aliye na nguvu atanyang'anywa, na mateka yake aliye dhalimu ataponyoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe..."


​Zaburi 107:10, -14  "Wale walioketi katika giza na kivuli cha mauti, waliofungwa katika mateso na vyuma... Aliwatoa katika giza na kivuli cha mauti, akavunja vifungo vyao."


​Kutoka 3:7 – "Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao."


​3. Kuzuia Mateso Yasirudie Tena


​Baada ya kambi kuvunjwa, ni muhimu kusimama na Mungu Kuwa Muombaji Hapa Utaomba hivi ili Adui Asirudi Tena. 

Ninakataa Kurudia PITO nililopitia Mwaka Jana Nakataa Kurudia PITO Nililopitia Mwezi uliopita Omba kukukataa Hali Kuwa Inajirudia Omba Na Usimame Upone Kinywa chako Kisiwe Kinarudisha Matatizo. 


SOMA MISTARI HII RUDIA MARA 5

​Nahumu 1:9 – "Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili."


​Yohana 8:36 – "Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli."


​4. Kambi ya Mungu Dhidi ya Kambi ya Adui

​Mungu pia ana kambi yake (Majeshi ya mbinguni) inayowalinda walio wake dhidi ya kambi za mateso:
Kwa hiyo Hapa Omba Uwe na Ulizi Wa Kiroho Uwe  Kwenye Kambi Ya Mungu TOKA Kuwa Kwenye Kambi Ya Adui Tumia KINYWA CHAKO Kujiondoa Huko. 

Vitabu Soma RUDIA ×4

​Zaburi 34:7 – "Malaika wa Bwana hufanya kituo (hupiga kambi) akiwazunguka wamchao, na kuwaokoa."


​Zekaria 9:8 – "Nami nitapiga kambi karibu na nyumba yangu kwa ajili ya jeshi hilo, ili mtu asipite wala asirudi; wala mtesi hatapita kati yao tena..."


KAMBI KATIKA MAENEO HUSIKA YA KUDHIBITI AU KUSHUGHULIKA


1:​Kambi ya Kiuchumi ;(Umasikini na madeni).
Hapa Adui humuendesha Mtu katika Utumwa Wa Uchumi. 

​2:Kambi ya Kifikra: (Hofu na kukata tamaa).
Hapa Fikira hukamatwa Kufikiri Kushindwa Shindwa tu. 

​3:Kambi ya Miili :(Magonjwa sugu).
Hapa Adui huweka magonjwa matatizo mwilini. 

​4:Kambi ya Kiroho (Vifungo vya kishirikina au vya ukoo).
Hapa Wachawi Humtesa Mtu na Mateso Mtu Yasiyoisha

5;Kambi Ya Mawazo(nikuwa na msongo Wa mawazo
Hapa Huwa Wanakutumikisha Kupitia Kuwaza kufakufa au Mungu Amekuacha Kukata Tamaa


SADAKA YAKO Iombee Hivi

Baba Hii Sadaka Yangu Yakunitoa Kwenye Umateka na Kambi Zao Walipokuwa Wameniweka Katika Jina la Yesu. Amen

Kisha unatoa Kwa;

M-PESA 0759861768
Mix by Yas 0710889892.
Airtel Money 0780508066
Halo Pesa 0628355985

Jina :Richard Julius Kushoka. 

Ukituma Tu Muda huo huo nipigie Simu niombe nawewe utaniambia ulikuwa Maombi Haya. 

HITIMISHO

Maombi Haya Ni Vita Utagusa Vitu Vingi Unatakiwa Uwe tayari kutoka Kwenye Kambi Zao Jijenge Kwenye Ulimwengu Wa Roho Uwe Na Kambi Ya Mungu. 


Alhamisi, 23 Aprili 2026

SOMO: BABA WA KIROHO

SOMO:BABA WA KIROHO sehemu ya 2

MAANDIKO YANAYOONGELEA BABA WA KIROHO. 

Biblia Inaeleza Baba Wa Kiroho ni Mwalimu Mchungaji anayekufundisha Njia ya Mungu Masomo yake unamuelewa na Yanakubadilisha Tabia Bsba Wa Kiroho Siyo aliyekuongoza Toba Au Kukuombea tu Baba Lazima Akuongoze namna ya kusimama na kukuonya mambo yasiyofaa anakufundisha Habari za Mungu nakukuelekeza. 

Huyu ni Wa umhimu unaweza Ukawa naye ulipo au nje ya hapo Lakini Unafatiliaga Masomo na Kutuma FUNGU la Kumi kwake Kupitia huyo Mungu atamtumia kukuvusha Vingi Wewe msikilize na umuelewe maelekezo yake. 

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania

1. Msingi wa Uhusiano wa Kiroho


​Mtume Paulo anajipambanua kama baba wa kiroho kwa wale aliowahubiria na kuwalea katika Kristo.. 


  • 1 Wakorintho 4:15: "Maana ijapokuwa mnao walimu elfu kumi katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili."

  • Wafilipi 2:22: Paulo anazungumzia Timotheo: "Lakini mnavyojua sifa yake, ya kuwa kama mtoto atumikavyo pamoja na baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami kwa ajili ya Injili."

​2. Mifano ya Baba na Mwana wa Kiroho


​Kuna mifano ya wazi ambapo watu walishirikiana kwa karibu kiasi cha kuitana baba na mwana:



  • Eliya na Elisha (2 Wafalme 2:12): Elisha alipomwona Eliya akichukuliwa juu, alipaza sauti akisema, "Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake!"

  • Paulo na Timotheo (1 Timotheo 1:2): Paulo anamwandikia Timotheo akisema, "Kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani..."

  • Paulo na Tito (Tito 1:4): "Kwa Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki..."

​3. Wajibu wa Baba wa Kiroho


​Maandiko yanahimiza viongozi wa kiroho kuwalea wengine kwa upendo na unyenyekevu, si kwa mabavu.



  • 1 Wathesalonike 2:11-12: "Kama vile mnavyojua jinsi tulivyokuwa tukiwafariji na kuwatia moyo kila mmoja wenu, kama baba afanyavyo kwa watoto wake mwenyewe..."

  • Wagalatia 4:19: "Watoto wangu, ambao kwa ajili yenu nahisi utungu wa uzazi tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu."

​4. Tahadhari Kuhusu Jina "Baba"



​Ni muhimu kuzingatia fundisho la Yesu kuhusu unyenyekevu na kutokumpa mwanadamu utukufu wa Mungu:



  • Mathayo 23:9: "Wala msimwite mtu yeyote wa duniani baba yenu; maana Baba yenu ni mmoja, aliye mbinguni."Maelezo: Wasomi wengi wa Biblia hufundisha kuwa hapa Yesu alikuwa akionya dhidi ya kutoa heshima ya kiungu kwa mwanadamu au kutumia vyeo kwa ajili ya kiburi, badala ya kukataa uhusiano wa malezi ya kiroho (kama ule wa Paulo na Timotheo).

    Ufafanuzi.

    Wasomi wengi wa Biblia hufundisha kuwa hapa Yesu alikuwa akionya dhidi ya kutoa heshima ya kiungu kwa mwanadamu au kutumia vyeo kwa ajili ya kiburi, badala ya kukataa uhusiano wa malezi ya kiroho (kama ule wa Paulo na Timotheo).


FAIDA YA BABA WA KIROHO


​1. Kupata Mwongozo na Maelekezo (Direction)

​Baba wa kiroho anasaidia kukuonyesha njia sahihi ya kupita ili usipotee katika safari ya imani.



  • Andiko: 1 Wakorintho 4:15 – "Maana ijapokuwa mnao walimu elfu kumi katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili."

​2. Malezi ya Kiungu na Ukomavu (Mentorship)



​Kama vile mtoto anavyokua chini ya mzazi, muumini hukua kiroho chini ya uangalizi wa baba wa kiroho mpaka anafikia ukomavu.



  • Andiko: Wagalatia 4:19 – "Watoto wangu, ambao kwa ajili yenu nahisi utungu wa uzazi tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu."

​3. Kupata Ulinzi wa Kiroho na Maombezi



​Baba wa kiroho anasimama kama mlinzi (watchman) wa roho yako, akikuombea na kukukinga dhidi ya mashambulizi ya adui.



  • Andiko: Waebrania 13:17 – "Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu..."

​4. Kurithi Upako na Neema (Inheritance)



​Kuna baraka na neema ambazo hupitishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mwana kupitia uaminifu na huduma.



  • Andiko: 2 Wafalme 2:9 – "...Elisha akasema, nakuomba, sehemu mbili ya roho yako na iwe juu yangu." (Hapa Elisha anarithi kutoka kwa baba yake wa kiroho, Eliya).

​5. Sahihisho na Nidhamu (Correction)


​Baba wa kiroho ana mamlaka ya kukusahihisha unapokosea ili usije ukaangamia au kupoteza mwelekeo.



  • Andiko: Mithali 3:12 – "Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, kama vile baba mwanawe ampendaye."

​6. Utambulisho na Uwajibikaji (Accountability)


​Inakusaidia kuwa na mahali unapofahamika na kuwajibika, jambo ambalo linakuepusha na kiburi au kuishi bila nidhamu ya kiroho.


  • Andiko: Wafilipi 2:22 – "Lakini mnavyojua sifa yake, ya kuwa kama mtoto atumikavyo pamoja na baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami kwa ajili ya Injili." (Paulo akimzungumzia mwanawe Timotheo).


UNAWEZA UKAWA HUJIBIWI HUNA Baba WA KIROHO na Hakikisha FUNGU LA KUMI TOA KWA BABA YAKO WA KIROHO. 

Kama Pastor Richard ndio Baba Wa Kiroho Hakikisha huachi Kutoa FUNGU LA KUMI NA UNANIPIGIA NAKUOMBEA

SOMO: NGUVU YA UMILIKI KATIKA UKOO

SOMO: NGUVU YA UMILIKI KATIKA UKOO

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Katika Familia au ukoo huwa Lazima Uwe na Nguvu ya kumiliki.
Mfano: Elimu madaraka Imani na Pesa Familia Yoyote Lazima Awepo Mtu mwenye cheo kama familia Ya Yese Au Ibrahimu nk

​Neno Kuu: “Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; na mali ya mwenye dhambi huwekewa mwenye haki.” (Mithali 13:22)


​1. Msingi wa Umiliki: Agizo la Kiungu


​Mungu ndiye aliyeanzisha mfumo wa koo na familia, na alikusudia kila ukoo uwe na sehemu yake ya kumiliki ili kujiendesha.


​Andiko:
 Mwanzo 1:28 
 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha..."


​Tafakari: Kuitiisha nchi maana yake ni kuitawala na kuimiliki. Ukoo usioiliki rasilimali hauwezi "kuitiisha" nchi, badala yake unatiishwa na kutaabika.


​2. Umiliki wa Ardhi na Urithi wa Kudumu


​Katika Biblia, ardhi haikuwa mali ya mtu mmoja tu, bali ilikuwa ni dhamana kwa ajili ya ukoo mzima ili kuhakikisha hakuna kizazi kinachokuja kuwa maskini.


​Andiko:

 Walawi 25:23 –

 "Nayo nchi haitauzwakatika hali ya kupotea kabisa; kwani nchi ni yangu mimi..."


​Tafakari: Nguvu ya ukoo ipo kwenye ardhi. Tunapaswa kulinda maeneo yetu ya asili na kuwekeza kwenye ardhi mpya kwa ajili ya watoto wetu. Nabothi alikataa kuuza shamba lake la mizabibu kwa mfalme Ahabu kwa sababu alijua thamani ya urithi wa mababu (1 Wafalme 21:3).



​3. Umiliki wa Maadili na Baraka (The Spiritual Assets)




​Mbali na mali, ukoo unapaswa kumiliki "Agano" na Mungu. Baraka za ukoo hutiririka kupitia utii na kumcha Mungu.
​Andiko: Kutoka 20:6 – "Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu."


​Tafakari: Ukimiliki maadili mema na hofu ya Mungu, unawajengea watoto wako "akiba ya kiroho" ambayo itawafungulia milango hata kama hupo.


​4. Hatari ya Kupoteza Umiliki (Kuuza Uzaliwa wa Kwanza)


​Watu wengi hupoteza nguvu ya umiliki kwa sababu ya tamaa za muda mfupi au njaa ya leo, kama alivyofanya Esau.
​Andiko: Mwanzo 25:34 – "Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na mchuzi wa dengu... hivyo Esau akaidharau haki yake ya uzaliwa wa kwanza."


​Tafakari: Usiize urithi wa ukoo wako (viwanja, biashara, au heshima) kwa ajili ya anasa za muda mfupi. Linda "Haki ya Uzaliwa wa Kwanza" ya ukoo wako.



​5. Umoja Kama Nguzo ya Umiliki


​Nguvu ya kumiliki inategemea umoja wa ukoo. Ukoo uliogawanyika hauwezi kulinda mali zake.
​Andiko: Zaburi 133:1, 3 – "Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja!... Maana huko ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele."
​Tafakari: Tunapounganisha nguvu (mali na akili), tunamiliki makubwa. Umoja ndio unaleta ulinzi wa kile tulichonacho.


​HITIMISHO 


​Ili kurejesha Nguvu ya Umiliki katika ukoo wako, anza na hatua hizi:

​Toba: Tubu kwa ajili ya makosa ya ubadhirifu na utengano yaliyotokea nyuma.


​Maono: Weka malengo ya pamoja (Mfano: Kila mwanachama achangie kiasi fulani kununua kiwanja cha ukoo au kusaidia elimu).


​Wosia: Himiza watu wazima kuandika wosia ili kuzuia migogoro inayofifisha nguvu ya ukoo.

Simama Wewe ndiye Uwe Nuru ya Ukoo wako

Jumanne, 21 Aprili 2026

SOMO:AINA ZA KUHAMISHA

SOMO:AINA ZA KUHAMISHA. 

Maombi haya Kabla hujaomba jua Unahamisha nini Kisha endelea kuomba


​1. Kuhamisha Mamlaka au Baraka


​Katika maandiko haya, tunaona nguvu, baraka, au uongozi ukitolewa kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.


  • Hesabu 27:18-20: Mungu anamwambia Musa amwekee mikono Yoshua ili

  •  kuhamisha mamlaka ya uongozi mbele ya kusanyiko.

  • Mwanzo 27: Habari ya Yakobo kupokea baraka iliyokuwa ya Esau (uhamishaji wa haki ya mzaliwa wa kwanza).

  • 2 Wafalme 2:9-15: Eliya anapohamisha "maradufu ya roho yake" kwa Elisha kabla ya kuchukuliwa mbinguni.

​2. Kuhamishwa kwa Watu (Uhamisho na Makazi)


​Hii inahusu watu kuhama kutoka nchi moja kwenda nyingine, mara nyingi kwa mpango wa Mungu au kama matokeo ya vita.


  • Mwanzo 12:1: "Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako... uende mpaka nchi nitakayokuonyesha."

  • Wafilipi 3:20: Inazungumzia uhamisho wa uraia, ikisema kuwa uraia wetu uko mbinguni.

  • Wakolosai 1:13: Andiko muhimu kuhusu uhamisho wa kiroho: "Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake."

​3. Kuhamisha Milki au Mali


​Sheria kuhusu jinsi ya kuhamisha mali au mashamba ili haki itendeke.


  • Hesabu 36:7: "Hivyo urithi wa wana wa Israeli hautahamishwa toka kabila hii kwenda kabila hiyo..." (Sheria ya kulinda urithi wa familia).

  • Mithali 22:28: "Usiondoe kigingi cha mpaka wa zamani, uliowekwa na baba zako." (Katazo la kuhamisha mipaka ya ardhi kwa udanganyifu).

​4. Kuhamisha Milima (Imani)


​Huu ni usemi wa mfano unaoonyesha uwezo wa imani katika kufanya jambo lisilowezekana kuwa linawezekana.


  • Mathayo 17:20: "...Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali, mtauambia mlima huu, 'Ondoka hapa uende kule', nao utahamia; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu."

  • 1 Wakorintho 13:2: "...tena nikiwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu."

​Jitazame Ujione Unahamisha Nini

SOMO: MTAZAMO WA UMRI KATIKA UCHUMBA

"DARASA LA WANANDOA"

SOMO:UJUE UMRI WAKO KATIKA MAHUSIANO YAKO.

Watu wengi huwa hawaelewi Kuwa Umri unavyoenda mbele huja na vichocheo mbalimbali vya kihisia vinavyomfanya mtu awake katika Tamaa za Ujana huhitaji Ufahamu WA Juu kuujua Umri WAKO na Kuutawala Mwili wako. Bila hivyo utajikuta unapitia maumivu na majereha ya mahusiano kwa kukosa Elimu. 

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

WhatsApp+255710889892

​1. Wakati wa Ujana (Kujilinda na Tamaa Miaka 13-19


​Katika umri huu, Biblia inasisitiza umuhimu wa kutawala hisia na kujiweka safi wakati unatafuta utambulisho wako Au Mahusiano


​2 Timotheo 2:22 

 "Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi."


​Mhubiri 11:9

​"Wewe kijana, uufurahie ujana wako... lakini ujue ya kuwa kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni."

👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
​2. Wakati wa Kujenga Misingi
 (Miaka 20–30)
🤛🏿🤛🏿🤛🏿🤛🏿🤛🏿🤛🏿🤛🏿🤛🏿🤛🏿

​Huu ni wakati wa kuchagua mwenza na kuanza kuwajibika. Biblia inatukumbusha kuwa kuchagua mwenza ni jambo la hekima na baraka.


​Mithali 18:22
​"Apataye mke apata kitu chema; naye ajipatia kibali kwa Bwana."


​Mithali 31:30
​"Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa."

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
​3. Wakati wa Utulivu na Familia (Miaka 30–50)
✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾

​Katika hatua hii, mkazo upo kwenye upendo wa dhati, uvumilivu, na kutunza agano la ndoa katikati ya majukumu ya maisha.


​Waefeso 5:25
​"Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolilinda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake."

​Wagalatia 6:2
​"Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo." (Hii ni muhimu sana katika kulea familia na kusaidiana majukumu).

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
​4. Umri wa Kukomaa na Uzee (Miaka 50+)
✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾✍🏾

​Hapa Biblia inaangazia hekima, urithi wa maadili kwa vizazi vijavyo, na upendo unaozidi kuwa na nguvu licha ya mwili kudhoofika.


​Tito 2:2-4
​"Wazee wawe na kiasi, wastahiwa, wenye kiasi, wazima katika imani na upendo na saburi... ili wawafundishe wanawake vijana kuwapenda waume zao na kuwapenda watoto wao."


​Mithali 16:31
​"Mvi ni taji ya utukufu, ikiwa inaonekana katika njia ya haki."


​Kanuni Kuu kwa Umri Wowote:

 1 Wakorintho 13:11


​Kifungu hiki kinahitimisha safari ya ukuaji wa mtazamo kutoka utoto hadi ukomavu:
​"Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto."


   HITIMISHO

​Hii inamaanisha kuwa kadiri umri unavyosogea, ndivyo na namna tunavyopenda na kuchukulia mahusiano inapaswa kuacha mambo ya "kitoto" (hisia tupu na drama) na kuingia katika mambo ya "utu uzima" (hekima, uvumilivu, na kusudi).Unaanza Kubadilika Mwenyewe

SOMO:AINA ZA UBATIZO KIROHO

Somo: Aina Za Ubatizo na Faida Zake


​Ubatizo ni tendo la kiroho la utii na utambulisho. Neno "kubatiza" linatokana na neno la Kigiriki Baptizo, linalomaanisha "kuzamisha" au "kuchovya kabisa."

Karibuni Ujifunze Kwenye SOMO hili ujue Ubatizo ukoje


​1. Aina za Ubatizo Kimaandiko


​Katika Biblia, tunajifunza kuhusu hatua mbalimbali za ubatizo ambazo mwamini anapaswa kuzipitia:


  • Ubatizo wa Yohana (Ubatizo wa Toba): Huu ulikuwa ubatizo wa maandalizi kwa ajili ya kumpokea Masihi. Ni ishara ya nje ya kuonyesha kuwa mtu ametubu dhambi zake.
    • Andiko: Mathayo 3:11"Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba..."

  • Ubatizo wa Maji (Kwa Jina la Yesu): 

  • Huu ni ubatizo wa kuzamishwa kwenye maji mengi baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi. Ni agizo la Kristo kwa kila mwamini.

    • Andiko: Mathayo 28:19"Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu."

    • Andiko: Matendo 2:38"Tubuni mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu..."

  • Ubatizo wa Roho Mtakatifu: Huu ni ubatizo ambao Yesu mwenyewe anaufanya, ambapo mwamini anajazwa na nguvu ya Mungu kwa ajili ya huduma na ushuhuda. Mara nyingi huambatana na ishara ya kusema kwa lugha mpya.

    • Andiko: Matendo 1:5"Kwa maana Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache."

  • Ubatizo wa Moto: Huu unahusu utakaso wa ndani kabisa na wakati mwingine unawakilisha majaribu yanayomfanya mwamini kuwa imara zaidi au hukumu ya Mungu inayoteketeza makapi.

    • Andiko: Luka 3:16"...Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto."

Faida za Kiroho za Ubatizo Huwa Ni Hizi Zifatazo


​1. Kufa na Kufufuka Pamoja na Kristo


​Ubatizo ni ishara ya kifo cha utu wa kale na kufufuka katika maisha mapya. Unapozamishwa majini, unazikwa pamoja na Kristo, na unapotoka, unaanza maisha mapya ya ushindi.



  • Andiko: “Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.” (Warumi 6:4)

​2. Ondoleo la Dhambi na Utakaso


​Ubatizo unawakilisha usafi wa dhamiri na kuoshwa kwa dhambi. Ni hatua ya kisheria ya kuachana na makosa ya zamani na kusimama mbele za Mungu ukiwa safi kupitia damu ya Yesu.



  • Andiko: “Na sasa, unakawia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako, ukiliitia jina lake.” (Matendo 22:16)

​3. Kuunganishwa na Mwili wa Kristo (Kanisa)



​Kupitia ubatizo, mwamini anakuwa sehemu rasmi ya familia ya Mungu ulimwenguni kote. Hakuna tena utengano wa asili au hali ya kijamii; wote wanakuwa wamoja ndani ya Kristo.


  • Andiko: “Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; kwamba tu watumwa, au kwamba tu huru...” (1 Wakorintho 12:13)

​4. Kupokea Karama ya Roho Mtakatifu


​Ubatizo mara nyingi huambatana na ahadi ya Mungu ya kummiminia mwamini Roho wake, ambaye anakuwa msaidizi, mwalimu, na chanzo cha nguvu katika maisha ya kila siku.



  • Andiko: “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” (Matendo 2:38)

​5. Kuvaa Utukufu wa Kristo


​Unapobatizwa, Biblia inasema unamvaa Kristo. Hii ina maana unazungukwa na tabia, mamlaka, na ulinzi wa Yesu.


  • Andiko: “Kwa maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.” (Wagalatia 3:27)

​6. Wokovu na Dhamiri Safi



​Ubatizo si tu tendo la kusafisha mwili kwa maji, bali ni ombi la mtu kwa Mungu ili apate dhamiri iliyo safi. Ni sehemu ya utii unaothibitisha wokovu wetu.


  • Andiko: “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuweka mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri njema mbele za Mungu)...” (1 Petro 3:21)

                   HITIMISHO

Kama Hujabatizwa Kamilisha Haki Ya Kiroho ubatizwe Kuna Matatizo Mengine Yanatokana na Ubatizo kukosa kubatizwa kiroho unaondoa Kitu kikubwa. 

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

WhatsApp+255710889892

Ijumaa, 17 Aprili 2026

SOMO: NGUVU YA NDANI

SOMO: NGUVU YA NDANI (THE INNER STRENGTH)

Utangulizi

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Karibuni Somo hili nzuri Sana. 

​Nguvu ya ndani si uwezo wa kimwili au akili tu, bali ni uwezo wa Roho Mtakatifu unaofanya kazi ndani ya utu wa ndani wa mwamini. Wakati ulimwengu unategemea hamasa (motivation), mwamini anategemea upako na nguvu inayotoka ndani kwenda nje.


1. Chimbuko la Nguvu ya Ndani


​Nguvu hii haitokani na mazoezi ya mwili, bali inatoka kwa Roho wa Mungu. Ni nguvu inayomfanya mtu asikate tamaa hata kama mazingira ya nje ni magumu.


  • Maandiko: “Ili kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalie kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.” (Waefeso 3:16)

  • Jambo la Kujifunza: Utu wa ndani unahitaji "chakula" na "mazoezi" ili uwe imara kama unavyoulisha mwili wa nje.

2. Tofauti ya Nguvu ya Ndani na Nguvu ya Nje


  • Nguvu ya Nje: Inategemea fedha, vyeo, na afya ya mwili. Hizi zinaweza kuchakaa.

  • Nguvu ya Ndani: Inafanywa upya kila siku, hata kama mwili unachoka.

  • Maandiko: “Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.” (2 Wakorintho 4:16)

3. Faida za Kuwa na Nguvu ya Ndani


  1. Ustahimilivu (Endurance): Inakusaidia kupita kwenye jaribu bila kuvunjika moyo.

  1. Ujasiri: Inakupa uwezo wa kusimama mbele ya maadui (Kama Daudi mbele ya Goliati).

  1. Utulivu: Unakuwa na amani katikati ya dhoruba (Kama Yesu alivyolala kwenye chombo).

4. Jinsi ya Kuitumia Nguvu ya Ndani (The Application)



​Hapa ndipo waumini wengi hukwama. Nguvu ipo, lakini namna ya "ku-release" (kuachilia) ndio changamoto. Tumia hatua hizi:


A. Kwa Njia ya Kukiri (Confession)


​Nguvu ya ndani inakaa kwenye roho, lakini inatoka kupitia kinywa. Unapokiri neno la Mungu, unaachilia nguvu hiyo kwenye mazingira yako.unayoyapitia na inaleta udhibitisho


  • “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:13)

B. Kwa Njia ya Maombi ya Roho (Praying in the Spirit)


​Unapoomba kwa lugha, unajijenga nafsi yako (Edification). Hii ni kama kuchaji betri ya simu ili ianze kufanya kazi. Lazima unene kwa Lugha uirusu nguvu itende Ndani Yako


  • “Yeye anenaye kwa lugha hujiujenga nafsi yake...” (1 Wakorintho 14:4)

C. Kwa Njia ya Tafakari (Meditation)


​Nguvu ya ndani inahitaji mwelekeo. Tafakari neno hadi liwe sehemu ya ufahamu wako. Ukiamini ndani, utatenda kwa ujasiri nje.


D. Kuchukua Hatua ya Imani (Action)


​Nguvu ya ndani haionekani mpaka uanze kufanya jambo ambalo linaonekana haliwezekani. Unapopiga hatua, Mungu anaachilia utendaji (Activation).


Hitimisho kwa Kanisa:


​Waambie waumini wako: "Mazingira yako yasiamue hatima yako; bali nguvu iliyo ndani yako iamue mazingira yako." Yeye aliye ndani yao ni mkuu kuliko yule aliye katika ulimwengu (1 Yohana 4:4).


WITO

NIFATE WhatsApp Pastor Richard Nikuunge +255710889892

Jumatano, 15 Aprili 2026

SOMO:WANAWAKE WANAOSALITIWA HUWA KUNDI HILI LIJUE

​SOMO:WANAWAKE WANAOSALITIWA HUWA KUNDI HILI  LIJUE. 

Rejea Vitabu:Mithali;8;10 Mithali;12;1-5

Karibu Sana Mwana NDOA  Katika DARASA Hili Uongeze Ufahamu Wa Kujifunza ili Uwe na Ufahamu usiendelee Kulizwa Kwenye Mahusiano Karibuni Tuwe Pamoja. 
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
WhatsApp+255710889892

1. Wanawake "Wanaojitolea Kupitiliza" (The Over-Givers)


​Hawa ni wanawake ambao huweka kila kitu chao kwa mwanaume—fedha, muda, na hisia—huku wakisahau mahitaji yao wenyewe.


  • Sababu ya kuumizwa: 

  • Mwanaume anaweza kuanza kumchukulia mwanamke huyu kama "shamba la bibi" au sehemu ya samani (taken for granted), na hivyo kukosa hofu ya kumpoteza kwa sababu anajua atakuwepo daima hata akifanya makosa.

​2. Wanawake Wanaovumilia "Vichocheo vya Hatari" (Red Flags)


​Kundi hili huona dalili za usaliti au tabia mbaya mapema lakini huchagua kuzipuuza kwa matumaini kuwa mwanaume atabadilika.



  • Sababu ya kuumizwa: 

  • Huamini kuwa upendo wao una nguvu ya "kumtibu" au kumtengeneza mwanaume, jambo ambalo mara nyingi hupelekea usaliti wa kudumu mwanaume anapogundua kuwa hakuna madhara makubwa yanayotokea anapokosea.

​3. Wanawake Wenye Utegemezi wa Kihisia (Codependent)


​Mwanamke ambaye hawezi kufanya maamuzi au kuwa na furaha bila idhini ya mwanaume.



  • Sababu ya kuumizwa

  • : Kwa sababu mwanaume anajua mwanamke huyu hawezi kuondoka (hana ujasiri au mbadala wa maisha), anatumia udhaifu huo kufanya mambo ya siri akijua hata akigundulika, atasamehewa kirahisi.

​4. Wanawake "Wanaookoa" Wanaume (The Fixers)



​Hawa huwatafuta wanaume wenye matatizo (majeraha ya zamani, ukosefu wa kazi, au tabia mbaya) wakiamini kuwa watakuwa "mashujaa" wa maisha yao.



  • Sababu ya kuumizwa: 

  • Mara nyingi mwanaume akishatulia au "kupona" kupitia mwanamke huyu, hutafuta mwanamke mwingine wa kuanza naye maisha mapya, akimwacha yule aliyemsaidia akiwa na maumivu.

​5. Wanawake Wanaoweka Picha ya "Ukamilifu"


​Wanawake ambao wanajali sana jinsi jamii inavyowaona. Hawataki kuonekana wameshindwa katika ndoa au mahusiano.


  • Sababu ya kuumizwa: 

  • Wanaume hugundua kuwa mwanamke huyu ataficha siri za usaliti ili kulinda heshima ya familia au jina lake, jambo linalompa mwanaume uhuru wa kuendelea na michezo ya nje.

​Mambo ya Kuzingatia ili Kuepuka MAUMIVU HAYA


  • Weka Mipaka (Boundaries): Mwanaume anapaswa kujua kuwa kuna vitendo ambavyo haviwezi kuvumiliwa hata kidogo.

  • Jipende Kwanza: Unapojithamini, unakuwa na ujasiri wa kuondoka au kukataa mazingira yanayokuvunjia heshima.

  • Sikiliza Silika (Intuition): Mara nyingi sauti ya ndani hutoa onyo kabla ya usaliti mkubwa kutokea.

. HITIMISHO:

INi muhimu kukumbuka kuwa usaliti ni chaguo la msaliti, na mwanamke hapaswi kujilaumu kwa tabia ya mtu mwingine, bali anapaswa kujifunza jinsi ya kulinda moyo wake na amani yake.


Wito. 

Nakukaribisha Pastor Richard Wa Morogoro Jiunge Kwenye group la Maombi WhatsApp+255710889892

SOMO; NGUVU YA KUTAFISIRI UNACHOKISIKIA

SOMO: NGUVU YA KUTAFSIRI UNACHOKISIKIA. 

​Utangulizi:


​Kusikia ni tendo la kibiolojia (masikio kupokea sauti), lakini Kutafsiri ni tendo la kiakili na kiroho (kutoa maana). Nguvu ya maisha yako haitegemei kile unachokisikia, bali inategemea tafsiri unayoipa sauti hiyo.

MASIKIO HUSIKIA:Kinachoongelewa

AKILI HUTOA TAFSIRI:Hutoa Maana Ya Kile ulichosikia. 
Watu Wengi Wanakosana Kwenye Eneo la Kusikia Lakini Akili inakuja kutafisiri makosa au Vibaya nakijenga chuki Kati ya Mtu na Mtu au kundi na Kundi. 

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
WhatsApp+255710889892

Maandiko na Misingi ya Somo


1. Nehemia 8:8 "Nao wakasoma katika kitabu, katika sheria ya Mungu, kwa sauti ya kueleweka; wakatoa maana yake, hata wakayaelewa yale yaliyosomwa."


• Fundisho: Nguvu haipo kwenye kusoma au kusikia tu, bali kwenye kutoa maana (tafsiri) inayopelekea uelewa.


2. 1 Wakorintho 14:13 "Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe ili apate kuitafsiri."


• Fundisho: Mawasiliano yasiyo na tafsiri hayana manufaa kwa msikilizaji. Tafsiri ndiyo inayoleta thamani.


3. Mithali 18:13 "Yeye ajibuye neno kabla hajalisikia, ni upumbavu na aibu kwake."


• Fundisho: Inasisitiza umuhimu wa kusikiliza kwa ukamilifu ili kupata tafsiri sahihi kabla ya kuchukua hatua.


4. Yakobo 1:19 "...kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali awe mzito wa kusema, na mzito wa hasira."


• Fundisho: Unapochelewa kusema, unaipa akili nafasi ya kutafsiri ujumbe kwa usahihi badala ya kuitikia kwa hisia.



AINA ZA SAUTI NAMNA YAKUTAFISIRI

​1. Tafsiri kama Kichujio cha Mtazamo 


​Unachokisikia kinaweza kuwa ni "tukio", lakini tafsiri yako ndiyo inayofanya iwe "fursa" au "tatizo".


a) ​Sauti ya Nje: "Umekosea hapa."

​b)Tafsiri Hasasi: "Mimi ni mshindwa, sifai." (Hii inanyonya nguvu).


​c)Tafsiri Chanya: "Huu ni mwaliko wa kujifunza ili niwe bora zaidi." (Hii inaleta nguvu).


​2. Kutofautisha "Sauti" na "Ujumbe" (Subtext)

​Nguvu ya kutafsiri inakuwezesha kuona kile ambacho hakijasemwa kwa maneno.
​Muktadha wa Hisia: Mtu anaweza kusema maneno makali, lakini tafsiri yako ikakuambia "Mtu huyu anaumia au ana hofu."


​Matokeo: Badala ya kurudisha hasira, unatoa suluhisho. Hii inakupa utawala juu ya mazingira yako . 


​3. Nguvu ya Kutafsiri Sauti ya Ndani . 


​Siyo kila unachokisikia kinatoka nje; kuna sauti za ndani ya akili yako.

​Sauti ya shaka: Ukisikia sauti ikisema "Hutaweza," una nguvu ya kuitafsiri kama "Hofu ya kawaida kabla ya hatua kubwa" badala ya kuichukulia kama "Ukweli."

​Nguvu: Ukibadilisha tafsiri ya sauti zako za ndani, unabadilisha hatima ya maisha yako.


​4. Epuka "Mtego wa Tafsiri Ya Haraka. 

​Watu wengi hupoteza nguvu kwa kutafsiri mambo kwa kukurupuka.


​Nguvu ya Kusubiri: Kabla ya kutoa tafsiri ya mwisho, uliza: "Je, kuna maana nyingine ya hili nililolisikia?"


​Hekima: Tafsiri sahihi inahitaji utulivu. Kelele haziwezi kutafsiri kelele; ni utulivu pekee unaoweza kutoa tafsiri sahihi.

​5. Kutafsiri Maelekezo kuwa Matendo. 

​Mafanikio yanakuja pale unapotafsiri "Nadharia" unayoisikia kuwa "Vitendo."
​Ukisikia somo la ujasiriamali, nguvu yako ipo kwenye kuitafsiri ile elimu kuwa mfumo wa kazi unaoonekana. Bila tafsiri ya kimatendo, unachokisikia kinabaki kuwa kelele tu.


​HITIMISHO:

​"Usiamini kila unachokisikia, amini tafsiri iliyopitishwa kwenye mchakato wa hekima."
​Ukiweza kutawala tafsiri yako:
​Utapunguza migogoro isiyo ya lazima.
​Utajenga mahusiano imara.
​Utakuwa na amani ya ndani hata katikati ya maneno ya dhihaka.



SILAHA 15 ZA KUTUMIA KWENYE MAOMBI

SILAHA 15 ZA KUTUMIA KATIKA MAOMBI YA VITA 

ZABURI 144:1 “Na ahimidiwe Bwana, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana”

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno yake ya uzima. Leo tutaona namna ya kuomba maombi ya vita. Tukisema maombi ya vita tunamaanisha maombi ya kushindana na nguvu zote za Yule mwovu katika ulimwengu wa Roho, maombi ya kulegeza vifungo na nira, na minyororo, na kuangusha ngome pamoja na kuta za Yule mwovu zinazokinzana na sisi katika ulimwengu wa Roho, kupitia majeshi yake ya mapepo wabaya.

Ndugu ni lazima ufahamu, Kuna aina nyingi za maombi, kuna maombi ya shukrani, maombi ya mahitaji, maombi ya upatanisho n.k.. Yote haya yana wakati wake wa kuyatumia. Lakini pia yapo maombi ya Vita, ambayo ni lazima sana na ni muhimu kwa Mkristo kuyatumia.

Hivyo siku ya leo tutaona ni jinsi gani tunaweza kutumia maombi haya ili tuziangushe ngome za adui yetu ibilisi kiwepesi.

Baadhi ya watakatifu hawajui namna ya kuomba, wanafikiri pale unaposema shindwa shetani! Shindwa shetani! Kwa Saa tatu, au usiku kucha ndivyo wanavyomwangusha ibilisi. Uhalisia ni kwamba, hatumshindi ibilisi kwa maneno yetu kuwa mengi, Bali tunamshinda ibilisi kwa Neno la Mungu kukaa ndani yetu kwa wingi. Ambalo hilo litakusaidia kujua SILAHA unazopaswa uzitumie kumpiga nazo shetani. Bila kufahamu Silaha zako za kiroho, ni ngumu sana kumshinda shetani kimaombi. Kwasababu maombi yako yatakuwa ni ya juu juu, yasiyokuwa na nguvu za kiroho.

Bwana asipokufundisha kupigana vita, haijalishi maombi yako yatakuwa na maneno mengi kiasi gani, huwezi angusha ngome za adui. Hivyo penda sana kulisoma Neno la Mungu kwa kulitafakari kwasababu huko ndiko utakapojifunza kupigana vita vyako.

Kibiblia zipo silaha nyingi ambazo Mungu alizitumia kuwapigania watu wake, na Leo tutaziorodhesha chache, na tutaona jinsi tunavyoweza pia kuzitumia rohoni. Kwasababu kumbuka Neno la Mungu halijaandikwa kutupa stori  Fulani tu, tuifurahie halafu basi hapana, bali kila tendo, kila Neno linatafsiri kubwa sana rohoni.

Hivyo hizi ni baadhi ya silaha ambazo Mungu alizitumia kuwasaidia watu wake kupigana vita;
Ninaitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Moto Wa Yesu

1:MVUA YA MAWE:

Mvua ya mawe
Mungu aliangusha mvua ya mawe kubwa sana, kwa wale watu wa Yerusalemu na wenzake walioungana kupigana na Yoshua kipindi kile wanaenda kuimiliki nchi yao, Utaona baadhi yao waliuliwa na Israeli, lakini wengi wa hao Mungu alimalizia kutoa hazina yake ya mvua kubwa ya mawe ikawaangamiza wengi sana kuliko hata wale waliouliwa na Yoshua.

Yoshua 10:11 “Kisha ikawa, hapo walipokuwa wakimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa katika kutelemkia Bethhoroni, ndipo Bwana alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao hata kufikilia Azeka, nao wakafa; hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko hao waliouawa na wana wa Israeli kwa upanga”

Jinsi ya kuomba: Bwana peleka, mawe yako ya barafu, katika madhabahu Zote za ibilisi, peleka mvua yako ya barafu katika vilinge vya kichawi, vinavyosimama kinyume na imani yangu. Haribu, bomoa, kila mbinu iliyoundwa dhidi yangu mimi (Taja maeneo yote ya maisha yako). Kama ulivyomshindia Yoshua nishindanie na mimi. [Hivyo Endelea kuita mvua hiyo na katika ulimwengu wa Roho, kwa jinsi unavyoiita kwa imani ndivyo inavyokuwa].

2:KIKOTO:

Yesu alipoingia hekaluni, alikutana na watu walioigeuza nyumba ya Mungu kuwa pango la wanyang’anyi. Ndipo akaunda kikoto kile, akapindua meza zote na kuwachapa wote waliofanya biashara pale, akawafukuza hekaluni kwa mamlaka yote, hekalu likawa safi kwa muda mfupi.

Yohana 2:15 “ Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16  akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”

Namna ya kuomba: Bwana naunda kikoto chako, napindua madhahabu zote za kipepo zilizoundwa moyoni mwangu na Yule adui, ninatawanyisha, ninasambaratisha, kila uovu, kila sanamu iliyopachikwa na Ibilisi (taja maeneo yote yanayohitaji maombi), kinyume na mapenzi ya Mungu. Ninavuruga kazi zote za ibilisi, kikoto cha Bwana kisafishe mwili wangu, kisafishe ibada yangu, kisafishe maisha yangu ya rohoni, kisafishe nyumba yangu, Naondosha uovu wa kila namna hata katika kazi yangu. [Sasa kwa jinsi unavyoomba kwa bidii na kurejea tukio hilo, ndivyo katika Roho Bwana anamnyuka shetani kwa namna ile ile. Ng’ang’ania hapo omba kwa imani kwa muda mrefu, kwasababu ndivyo ibilisi anavyodondoshwa].

3:KELELE ZA VITA:

kelele za vita
Bwana hutumia vitisho pia, kuwaondoa maadui, utakumbuka wakati Fulani wana wa Israeli, walizungukwa na maadui kwa muda mrefu. Hadi nchi ikaingiwa na njaa, watu wakaanza kulana ili waishi. Lakini jinsi Mungu alivyowaondoa maadui zao inashangaza. Kwasababu alifanya tu, kuwasikilizisha sauti za vita. Hivyo wale maadui waliposikia waliogopa sana wakawa wanakimbia kwa hofu kubwa sana huku wanaacha nyara zao nyuma. Baadaye Wayahudi kwenda wanashangaa hawawaoni maadui zao, wakijuliza ni nini kimetokea, mpaka waache na nyara, wakagundua kuwa ni Bwana ndiye aliyewatetea. Ndipo wakazichukua nyara kiwepesi na vita vikawa vimeisha kwa namna ile.

2Wafalme 7:6 “Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.  7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao”

Namna ya kuomba: Bwana peleka sauti zako za vita, katika ngome ya ibilisi, wafukuze waende mbali nami, hazina zote na vipawa vyote walivyoniibia katika roho na mwili ninavirejeza kwa Sauti yako ya vita. Watawanyike kwa njia saba. Vyote walivyoviiba navirejesha, fungua mipaka yangu, safisha hema yangu, adui atoweke kwa sauti za vita vya Bwana. [ Omba kwa kutaja maeneo yote ambayo unataka Bwana akutetee katika hayo].

4:UPOFU:

Wale malaika wa Bwana walioshuka Sodoma ili kuipeleleza, walikutana na wenyewe wa mji ule, ambao walitaka kulala nao. Hivyo malaika wale wakiwa nyumbani kwa Lutu. Maandiko yanaema waliwapiga upofu watu wale wasiweze kuiona nyumba mpaka asubuhi. Utakumbuka pia Paulo alipofika katika kile kisiwa kilichoitwa. Alishindana sana na Yule mchawi mpaka akamwomba Mungu ampige kwa upofu akawa kipofu kwa muda.

Mwanzo 19:10”Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.  11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango”.

Namna ya kuomba: Bwana piga upofu majeshi ya mapepo yote mabaya yaliyokuja kufanya vita kinyume changu mimi, wasione roho yangu, uufiche uhai wangu ndani yako, shusha kiwi na giza mbele yao. Wapapase, wasione huduma yangu, (taja mambo yako yote ambayo unatamani ibilisi asiyaone), waangamie na kuishia shimoni, watafute lakini wasione. [Hivyo Kwa jinsi unavyosimamia vifungu hivyo ndivyo unavyoshinda vita rohoni kiwepesi kwasababu mambo hayo yanatendeka kwelikweli].

5:JIWE LA MUNGU:

maombi ya vita jiwe la Yesu
Jiwe la Mungu ni Yesu. Yeye mwenyewe alijifananisha na jiwe hilo lililo zito sana na gumu. Akasema. Likimwangukia mtu linamsaga tikitiki, na yoyote atakayeliangukia atavunjika vunjika Kuonyesha ni jinsi gani lilivyo bora, ndio lile lililopiga sanamu ya Nebukadreza, na kuisaga kama unga, na kupotea kabisa(Danieli 2:34).

Mathayo 21:44  “Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki”.

Namna ya Kuomba: Yesu simama mwenyewe unitetee, kama jiwe lililo hai lenye nguvu na imara. Piga kila aina ya kuta nzito za ibilisi zinazozuia upenyo wangu. Nazibomoa kwa jiwe hili, ninalirusha katika kila Nyanja, impige ibilisi katika kipaji cha uso wake, aanguke kama Goliathi mbele ya Daudi. Wewe uliye jiwe piga kila ngome, ya mwovu lisage na kuharibu na kusagasaga, kazi zote za mwovu mbele yangu ziwe kama makapi mbele ya Upepo.[Lielekeze jiwe hili, liangushe kwelikweli kwa imani ndivyo itakavyokuwa katika ulimwengu wa roho]

Natumai mpaka hapo umeshapata mwangaza wa namna ya kulitumia Neno kuomba maombi haya ya vita, Kwasababu ya muda, hatuwezi toa maelezo ya silaha zote zilizo katika biblia, Hivyo hizi ni silaha nyingine ambazo zitumie, zikusaidie.

6) UPEPO WA KUSULISULI NA RADI:  Andiko la kusimamia (Zaburi 77:18). Omba Bwana avuruge, na kuichosha mikakati yote ya adui dhidi yako mfano wa kisulisuli kizungushacho makapi.

7) GHARIKA YA BWANA: Andiko la kusimamia (Mwanzo 6:17). Kama Bwana alivyoangamiza waovu wakati ule wa Nuhu kwa gharika Omba Bwana akafungue madirisha yake ya mbinguni, agharikishe majeshi ya kipepo yanayokufuatilia yakuangamize, yaangamie kama majeshi ya Farao katika bahari ya Shamu.

8) UPANGA WA BWANA: Andiko la kusimamia (Ufunuo 19:15). Omba ule upanga wa Bwana ukatao kuwili, ukate, na kuua mambo yote maovu ya adui yanayosimama mbele yako

9) KUTAWANYWA USEMI: Andiko la kusimamia (Mwanzo 11:7-9). Kama alivyouvuruga usemi wa wajenzi wa Babeli wasielewane, vivyo hivyo akaruge hila za ibilisi na mapepo yake zisipatane juu yako.

10) MOTO WA BWANA: 

Andiko la kusimamia (2Wafalme 1:10). Moto ukaunguze mapando yote, ya ibilisi, aliyoyapanda moyoni mwako,

11) NZIGE, PARARE, MADUMADU, TUNUTU:

 Andiko la kusimamia (Yoeli 2:25). Bwana akatume jeshi lake la waharibuo, wakatafune kazi zote za mwovu, wakalete hasara, warudishe nyuma, na kudhoofisha ufalme wote wa giza.

12) MAJIPU YA BWANA:

 Andiko la kusimamia (Kutoka 9:9). Bwana alete hali mbaya ya mateso, kwa wakuu wote wa giza wafanyao vita kinyume na wewe.

13) TETEMEKO: 

Andiko la kusimamia (1Samweli 14:15) . Bwana alete utisho na mashaka, na tetemeko kwa wakuu wa giza na mapepo yasimamo kinyume cha kazi ya Mungu.

14) UKAME (kiu na njaa): 


Andiko la kusimamia (Amosi 8:11). Bwana alete ukame wa kiroho, kwa majoka yote yanayosimama kutaka kumeza watu wa Mungu, yafe na kuteketea kwa kukosa mawindo ya watu.

15) RUNGU LA BWANA: 

Andiko la kusimamia (Yeremia 51:20).  Lipige na kuleta majeraha katika ufalme wa giza, liziraishe mapepo yote na vikaragosi vyake vyote vifanyavyo vita na wewe.

Zipo na silaha nyingine nyingi katika maandiko Hatuwezi kuziorodhesha zote, Hivyo kwa jinsi Neno la Mungu linavyokaa ndani yako, ndivyo utakavyoweza kuzivumbua na kuzitumia. Na zote hizo ni sharti tuziombe katika jina la Yesu na uweza wa damu ya Yesu Maombi ya namna hii yana nguvu sana, na yatakufanya udumu kwa muda mrefu katika kuomba. Na kufungua vifungo vingi sana katika ulimwengu wa Roho.

Kumbuka pia, vita hivi hatuvielekezi kwa wanadamu, bali kwa Shetani na majeshi yake ya mapepo na kazi zake zote. Kwasababu maandiko yanasema vita vyetu sio juu ya damu na nyama, maana yake ni kwamba sio juu ya wanadamu wenzetu. Bali ni juu ya falme za giza, zikawaachilie mateka, waje kwa Bwana, na sio tuwaue wao pamoja na mateka wao.

Waefeso 6:12  “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 6.13  Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama”

Bwana akubariki Sana 

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania
WhatsApp +255710889892

Jumanne, 14 Aprili 2026

SOMO: BINT ANAYELIZWA KWENYE MAHUSIANO

    "DARASA LA WANANDOA"


SOMO: BINT ANAYELIZWA KWENYE MAHUSIANO YAANI WATU WA HIVI HUMIZWA SOMA DALILI HIZI. 

Mwanamke hushawishika Kupitia Maneno Tu Kwenye Uhusiano Pasipo kushirikisha Akili yake Hujikuta Amempa MOYO Wote hapo BINT hujikuta Akili Maamuzi na Fikira Sake Zimekamatwa mpaka aje Anasuliwe Kwenye mtengo huo Mpaka spare MTU amfugue kiufahamu Amfundishe Kuwa na Akili Kwenye Mahusiano Kuliko hisia Kuliko MOYO kuamini Amini.

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania
WhatsApp +255710889892

​1. Kutoa Matumaini Kupita Kiasi (High Expectations)


​Binti anayejenga picha kuwa uchumba ni sawa na ndoa tayari anaweza kuumia. Ikiwa anaamini kuwa mwanaume huyo hawezi kubadilika au kuwa na mapungufu, mdondoko wa kihisia (disappointment) huwa mkubwa sana pindi changamoto ndogo zinapojitokeza.


​2. Upendo wa "Kupitiliza" Mapema. 



​Sifa hii inahusisha binti ambaye anatoa moyo wake wote 100% kabla hata hajajua tabia halisi ya mchumba wake. Anapowekeza hisia zote, muda, na hata mali zake mapema sana, inakuwa vigumu kwake kujiondoa hata akiona dalili za hatari (red flags).



​3. Kujitenga na Jamii (Social Isolation)


​Binti ambaye anapofika kwenye uchumba anaacha marafiki zake, familia, na watu waliokuwa wakimshauri, anakuwa kwenye hatari kubwa. Akikosa "mfumo wa msaada" (support system), anabaki kuwa tegemezi kwa mwanaume mmoja pekee, na jambo hilo likiharibika, anajikuta hana pa kukimbilia.



​4. Kukubali Kila Kitu (Lack of Boundaries)


​Binti asiye na misingi au mipaka ya kile anachoweza kukubali na kile anachokataa anaweza kuumizwa. Hii ni pamoja na:



  • ​Kuvumilia manyanyaso kwa kisingizio cha "staha."

  • ​Kupuuza makosa makubwa ya tabia akidhani mwanaume atabadilika baada ya ndoa.

​5. Kutafuta Furaha Kupitia Mwanaume (Low Self-Esteem)


​Ikiwa binti hajisikii kuwa ana thamani mpaka awe na mwanaume, atafanya kila namna kumfurahisha mchumba wake hata kwa kujiumiza mwenyewe. Hofu ya kuachwa (fear of abandonment) humfanya aishi kwa wasiwasi, jambo ambalo ni maumivu tosha kabla hata uchumba haujavunjika.


​6. Kukosa Uhuru wa Kiuchumi na Kifikra


​Binti anayemtegemea mchumba wake kwa kila kitu (chakula, mavazi, au maamuzi madogo ya maisha) anapoteza sauti yake. Hii inamfanya awe mnyonge na akishindwa kupata anachohitaji au akitishiwa kuachwa, maumivu yake yanakuwa maradufu kwa sababu anahisi maisha yamesimama.


​Ushauri wa Kuzingatia Kwa Mabint


​Uchumba ni kipindi cha kufahamiana na kupima tabia, si kipindi cha kufumba macho. Ni muhimu kwa binti:

  • ​Kuweka akiba ya maneno na hisia.

  • ​Kuendelea kujiendeleza kimaisha (elimu, kazi, au vipaji).

  • ​Kusikiliza sauti ya ndani na ushauri wa watu wenye busara na maadili.

​Kuumizwa kwenye uchumba mara nyingi hutokana na kuingia kwenye mahusiano kwa hisia pekee bila kuhusisha mantiki (logic) na kanuni za maadili.



              HITIMISHO. 


Maumivu Yako Ni Kukosa Akili ya Mahusiano nakutanguliza Hisia Mbele Mtu Unamuweka Moyoni Kiasi Kwamba hats Ibada na Mungu unapunguza. 


Tabua Hili Kijana Wa Kiume huongozwa na Akili Sana Kwenye Mahusiano Na Bint Huongozwa na Moyo kupenda na kufanya uchanguzi kwa Hisia Pasipo Akili. 



WITO

Penda Kujifunza Sana ili Uelewe Kujiponya Nafsi Yako na Mahusiano. 

Somo: Utambuzi Wa Taarifa Kiroho

Somo: Utambuzi wa Kiroho na Kweli Katika Ulimwengu wa Taarifa


​Katika ulimwengu wa sasa, changamoto kubwa si ukosefu wa taarifa, bali ni kuchuja taarifa ipi ni ya kweli na ipi ni ya uongo. Kama ambavyo ngano na magugu hukua pamoja, ndivyo ukweli na uongo unavyochanganywa mtandaoni na mitaani.


​1. Msingi wa Biblia: Kupima Kila Kitu

​Neno la Mungu linatutaka tusiwe watu wa kuamini kila neno linalokuja mbele yetu. Biblia inatufundisha kuwa na akili ya kudadisi (critical thinking) iliyojaa Roho Mtakatifu.


  • 1 Yohana 4:1"Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani."
  • Mithali 14:15"Mjinga huamini kila neno; bali mwenye busara huangalia sana mendo yake."
  • 1 Wathesalonike 5:21"Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema."

​2. Madhara ya Taarifa Isiyo Sahihi

​Uongo hauji kama uongo wa wazi; mara nyingi huja kama "nusu-kweli." Madhara yake ni:

  • Kuvuruga Amani: Taarifa za uongo huzalisha hofu (2 Timotheo 1:7).
  • Kufanya Maamuzi Mabaya: Ukifuata taarifa isiyo sahihi, utafika mahali pasipo sahihi.
  • Kupoteza Muda: Kujadili mambo yasiyo na tija badala ya kujenga maisha.

​3. Jinsi ya Kupata Utambuzi (Discernment)

  • Neno la Mungu kama Kipimo: Ikiwa taarifa inapingana na kanuni za upendo, ukweli, na amani ya Kristo, iweke kando.
  • Tunda la Roho: Taarifa inayoleta chuki na mafarakano mara nyingi haitoki kwa Mungu.
  • Busara ya Kawaida: Chunguza vyanzo. Je, ni vya kuaminika? Je, kuna ushahidi?

​Sehemu ya Maombi

​Unaweza kutumia miongozo hii ya maombi kwa ajili yako binafsi au kwa kundi:

​1. Ombi la Kuomba Hekima na Utambuzi

​"Ee Bwana, asante kwa zawadi ya akili na maarifa. Nakuomba unipe roho ya utambuzi. Katika wingi wa maneno na taarifa ninazokutana nazo kila siku, nisaidie kuutambua ukweli na kuukataa uongo. Nipe hekima ya Sulemani ili nijue kutofautisha kati ya mema na mabaya. Amina."

​2. Ombi la Kulinda Moyo na Fikra

​"Mungu Mwenyezi, ninalinda moyo wangu na fikra zangu dhidi ya habari za uongo zinazoleta hofu na mashaka. Neno lako linasema nitalinda moyo wangu kuliko yote niyalindayo. Niongoze nisishiriki kueneza uongo, bali niwe mbeba habari za amani na kweli pekee. Amina."

​3. Ombi la Kukataa Roho ya Upotevu

​"Katika jina la Yesu, ninakataa kila roho ya upotoshaji inayolenga kunivuruga mimi, familia yangu, au jamii yangu kupitia taarifa zisizo sahihi. Ninavunja nguvu ya hofu inayotokana na 'fake news' na ninachagua kutembea katika nuru ya ukweli wako. Amina."

Neno la kufungia: "Nanyi mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." (Yohana 8:32)

Jumapili, 12 Aprili 2026

SOMO:JIPANGE HAYA UKITAKA KUOWA

DARASA LA WANANDOA

SOMO: JIPANGE HAYA UKITAKA KUOWA

Karibuni Wanandoa na Mnaotarajia Kuingia Kwenye ndoa SOMO hili Muhimu Sana
Naitwa Pastor Richard Ninakukaribisha fatatana na Mimi Ujue vitu vya kujipanga Kabla ya KUOWA. 


​1. Maandalizi ya Kisaikolojia na Kiakili


​Kabla ya kila kitu, lazima uwe tayari kubadilisha mfumo wako wa maisha.



  • Utayari wa Kubadilika: Utatoka kwenye maisha ya "mimi" na kuingia kwenye maisha ya "sisi." Maamuzi yako mengi sasa yatahusisha mtu mwingine.


  • Uvumilivu na Ustahimilivu: Ndoa ina changamoto. Unahitaji kuwa na uwezo wa kudhibiti hasira na kutatua migogoro kwa busara badala ya hisia.

  • Kujitoa : Hakikisha unajua kwa nini unataka kuoa. Je, ni shinikizo la umri, au ni utayari wa dhati wa kuishi na huyo mtu?


​2. Maandalizi ya Kiuchumi (Uchumi wa Kaya)



​Haimaanishi uwe tajiri wa kutisha, lakini unahitaji msingi imara wa kuendesha maisha ya watu wawili (na watoto baadaye).



  • Makazi: Lazima uwe na sehemu ya kuishi inayoeleweka, iwe ni ya kupanga au yako mwenyewe, ambayo mkeo atajisikia salama na huru.

  • Kipato cha Uhakika: Hakikisha una chanzo cha fedha kitakachoweza kuhudumia mahitaji ya lazima kama chakula, mavazi, matibabu, na akiba.


  • Bajeti ya Sherehe vs. Maisha Baada ya Harusi: Watu wengi hujipanga kwa ajili ya siku moja ya harusi na kusahau maisha ya miaka 50 ijayo. Jipange zaidi kwa ajili ya "ndoa" kuliko "harusi."


​3. Kumjua Mwenza Wako



​Hili ni eneo ambalo wengi hulipuuza, lakini ni la msingi sana.



  • Tabia na Maadili: Je, mnaendana kwenye mambo ya msingi kama imani, malezi, na mtazamo wa maisha?

  • Afya: Ni vizuri kupima afya pamoja (HIV, Sickle Cell, na magonjwa mengine ya kurithi) ili mjue namna ya kuhudumiana na kulinda kizazi chenu.

  • Malengo ya Baadaye: Ongeeni kuhusu idadi ya watoto mnaotaka, malezi yao, na namna ya kusaidia familia za pande zote mbili (ndugu na wazazi).


​4. Maandalizi ya Kijamii na Kifamilia



​Ndoa katika jamii zetu ni muungano wa familia mbili, si watu wawili tu.




  • Mahari: Kulingana na mila na desturi za upande wa mke, unapaswa kujipanga kwa ajili ya mahari na taratibu nyingine za kifamilia.

  • Baraka za Wazazi: Ni muhimu kupata ridhaa na baraka kutoka kwa wazazi au walezi wa pande zote mbili ili kuanza safari yenu kwa amani.


​5. Stadi za Maisha (Soft Skills)



  • Mawasiliano: Jifunze namna ya kuongea na kusikiliza. Mawasiliano mabaya ndiyo chanzo kikuu cha migogoro mingi ya ndoa.

  • Usimamizi wa Fedha: Jifunze namna ya kupanga bajeti ya familia na kuwa muwazi kwenye masuala ya pesa na mkeo.

HITIMISHO



Usisubiri mpaka kila kitu kiwe "perfect" ndipo uoe, maana ukamilifu hauji haraka. Muhimu ni kuwa na msingi (maono na kipato cha kuanzia) na utayari wa kukua pamoja na mkeo.

SOMO:UMHIMU WA SADAKA YA JUMAPILI

SOMO: UMHIMU WA SADAKA YA JUMAPILI

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro veta Dakawa
Leo Tunaenda Kujifunza Umuhimu Wa Sadaka Ya Jumapili Kwa Mkristo Anapotoa Sadaka Yake Jumapili. Tunapotoa Zaka Tunakiri Kuwa Ametulinda Wiki Nzima. 


1. Ni Sehemu ya Ibada na Kumshukuru Mungu



​Sadaka si malipo kwa Mungu, bali ni ishara ya kutambua kuwa kila tulicho nacho kinatoka kwake. Tunapomtolea Mungu siku ya Jumapili, tunakiri kuwa yeye ndiye chanzo cha baraka zetu.



  • Zaburi 96:8: "Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mwingie katika nyua zake."

​2. Kuendeleza Kazi ya Injili isonge mbele



​Sadaka zinazotolewa kanisani hutumika kugharamia utendaji wa kanisa, kusaidia wahitaji, na kueneza neno la Mungu maeneo mbalimbali.



  • Wafilipi 4:18: "Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi... nimeyapokea kwa Epafrodito vile vitu vilivyotoka kwenu; harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, inayompendeza Mungu."

​3. Kipimo cha Uaminifu na Upendo Kwa Mungu


​Kutoa ni kielelezo cha moyo uliofunguliwa kwa Mungu. Biblia inasisitiza kuwa kutoa kwa hiari na furaha hupendeza moyo wa Mungu.



  • 2 Wakorintho 9:7: "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."

​4. Maagizo ya Mitume Kuhusu Siku ya Kwanza ya Juma



​Katika Agano Jipya, tunaona utaratibu wa waumini kuweka akiba na kutoa kulingana na walivyobarikiwa, hususan siku ya kwanza ya juma (Jumapili).. 


  • 1 Wakorintho 16:1-2: "Kuhusu ile changizo kwa ajili ya watakatifu... siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake..."


​5. UFunguo Wa Baraka Zaidi


​Ingawa hatutoi ili "tumnunue" Mungu, maandiko yanafundisha kuwa kutoa hufungua milango ya baraka kwa mtoaji. Ni kanuni ya kiroho ya kupanda na kuvuna.


  • Luka 6:38: "Wapeni watu vitu nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu."

  • Mithali 3:9-10: "Mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote; ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi..."

Hitimisho:


Sadaka ya Jumapili ni tendo la kiroho linalounganisha moyo wa mwanadamu na ukarimu wa Mungu. Inatakiwa kutolewa kwa imani, unyenyekevu, na shukrani, tukitambua kuwa tunamrudishia Mungu sehemu ndogo tu ya kile alichotujalia



WITO

WhatsApp Ya Pastor Richard Jiunge Kwenye group la Maombi

Jumamosi, 11 Aprili 2026

MASWALI NA MAJIBU

KARIBUNI KIPINDI CHA

MASWALI NA MAJIBU


 SWALI 1: Katika Mathayo 15:21-28, Yesu alikuwa na maana gani alipomwambia huyu mama kwamba chakula cha watoto hawapewi mbwa?. Pia kwanini alisema hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Israeli.?

JIBU: Tusome, Mathayo 15: 21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.
22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile. “

Kumbuka Bwana Yesu alipokuja duniani, hakutumwa kwanza kwa watu wa mataifa, hapana kwasababu wao hawakuwa wanamtazamia mwokozi yeyote, kadhalika watu wa mataifa walikuwa ni watu wasiokuwa ni dini, wapagani, wasiomjua Mungu, walikuwa wanaabudu miungu,na ndio maana Bwana akawafananisha na mbwa katika mfano huo…

Lakini wayahudi ni watu wa Mungu tangu zamani uzao wa Ibrahimu, pamoja na hayo kwa miaka mingi walikuwa wanalitazamia taraja la wokovu wao ambalo lingeletwa tu na MASIHI mwenyewe atakayeshuka kutoka mbinguni, Hivyo kwa kuwa wale ni uzao wa Mungu, uzao wa Ibrahimu, sasa ulipofika wakati wa Mungu kuwatimizia haja yao waliyokuwa wanaisubiria kwa muda mrefu, ndio akamleta Bwana Yesu duniani aje kuwakomboa..

Na ndio maana sasa tunamwona Bwana Yesu alipokuwa duniani, hakuhubiri katika nchi yoyote ya mataifa, kadhalika hakuwatuma hata wanafunzi wake katika mji au kijiji chochote cha mataifa, kwasababu hakutumwa kwao, bali kwa wale waliomtazamia (yaani wayahudi).

Lakini hapa tunamwona huyu mwanamke ambaye ni mtu wa Tiro, (mwanamke aliyekuwa wa kimataifa), asiyekuwa na dini wala Imani katika Mungu wa kweli, alipomwona Bwana akipita kando kando ya miji yao, akamfuata ili ahudumiwe naye, lakini Bwana hakuonyesha kumjali kwa namna yoyote ile, lakini kwa vile alivyokuwa akimsumbua sumbua, ndipo Bwana akamwambia sikutumwa [kwa watu wa mataifa] ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (yaani wayahudi)..lakini alipozidi kumsumbua sumbua, aliongezea na kumwambia “si vema kutwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa”..yaani akiwa na maana kuwa si vizuri kuiondoa ile neema ya wokovu kwa wale waliostahili kuipokea(yaani wayahudi) na kuwapatia watu ambao hawakustahili kuipokea au kuitazamia(watu wa mataifa).

Lakini pamoja na hayo tunakuja kuona baadaye, ile neema ililetwa kwetu sisi mataifa, baada ya wale ambao waliostahili kuipokea kuikataa, hivyo sisi sasa sio mbwa tena bali tumefanywa kuwa wana wa Mungu kwa damu ya Yesu Kristo.
Hiyo ndio siri iliyokuwa imefichwa tangu zamani kwamba sisi watu wa mataifa tumehesabiwa kuwa warithi wa wokovu sawa na wayahudi kwa njia ya Yesu Kristo. Haleluya. Hivyo ndio maana Mtume Paulo akasema katika..

Waefeso 3: 4 “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.
5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6 ya kwamba MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; “

Hivyo somo la kujifunza, hapo ni lipi?. Tumwendeapo Mungu, kwa haja ihusuyo wokovu wetu, hata kama ni kweli tutakuwa hatustahili mbele za Mungu, pengine njia zetu zimekuwa mbaya sana, na tumeomba mara ya kwanza, na ya pili na ya tatu hatujajibiwa…Hatupaswi kukataa tamaa, tuzidi kuomba tuzidi kuomba kama yule mwanamke..Kwasababu Bwana Yesu alishatupa mfano unaofanana na huo, juu ya yule kadhi dhalimu, aliyekuwa hamchi Mungu, lakini yule mwanamke mjane alivyomwendea mara ya kwanza hakupewa haki yake, lakini kwa jinsi alivyokuwa akimwendea endea mara kwa mara, alimpatia haki yake, japo hamchi Mungu, ili asije akamsumbua daima…(Luka 18:1-8)

Vivyo hivyo na sisi tusiache kumwomba Mungu neema ya wokovu, neema ya uponyaji, mahitaji binafsi, hata kama hatutaona dalili zozote za kujibiwa maombi yetu. Kwasababu Mungu anapendezwa na mtu aombaye kwa bidii.

 SWALI 2: Ndugu zangu Mungu anasababisha AJALI yeyote?.Iwe ya meli,gari,pikipiki,baiskeli,angani ndege,moto n.k?.Mfano wa ajali ya meli ya 'titanic'","mfano wa ajali ya gari lililobeba wale watoto wa shule ya Lucky Vicent(na hizo ajali nyingine)","mfano wa ajali za hosteli/mabweni kuungua moto na watu kufia huko",n.K.K..Ndugu zangu hizi zote zinasababishwa na BWANA wetu YESU KRISTO au ni Shetani.?Karibuni sana ndugu zangu..

JIBU: Mungu hasababishi ajali yoyote ile, japo Mungu anaweza akamwadhibu mtu kwa makosa yake. Shetani ndiye mwenye lengo siku zote la kuangamiza hata wakati ambapo mtu hana makosa, kama alivyofanya kwa Ayubu, kwasababu biblia inasema yeye alikuwa ni muuaji tangu mwanzo.(Yohana 8:44).

Asilimia kubwa ya ajali na majanga yanaletwa na shetani. Na pia biblia inasema yapo majanga mengine yanaletwa na Mungu mwenyewe, na mpaka imefikia hivyo ujue ni adhabu kutokana na makosa ya watu wenyewe, na pia Bwana anasema huwa hafanyi jambo lolote bila kuwafunuliwa hao watumishi wake manabii, kuwaonya kama tunavyoona alivyofanya kwa watu wa Ninawi.

Leo hii mtu anamuudhi Mungu labda ni muuaji, lakini kabla Mungu hajamwadhibu atamwonya pengine kwa kumtumia Mtumishi wa Mungu au kwa kusikia mahubiri, na akajua kabisa Mungu anamwonya atubu utakuta pengine alisikia Neno likisema “Uaye kwa upanga, atauawa kwa upanga”..

Lakini yeye akapuuzia na kuendelea na tabia yake ya kuuiba na kuua watu pasipo hatia.. Sasa mtu kama huyo inatokea mazingira labda siku moja amekutana na kundi la wanyang’anyi usiku, na kwa bahati mbaya wakamvamia na kumchoma kisu, kisha na kufa..Sasa kwa nje unaweza ukasema ni shetani lakini sio shetani bali ni Mungu mwenyewe kamlipizia kisasi juu yake.

Hivyo zipo ajali zinazotoka kwa Mungu mwenyewe. Kadhalika zipo pia zinazotengenezwa na shetani, ambazo hizo ndio nyingi kuliko zile zinazotoka kwa Mungu.


 SWALI 3:Matendo15:37"Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.38"Bali Paulo HAKUONA VEMA kumchukua huyo aliyewaacha huko pamfilia,asiende nao kazini.39"Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana....,swali Kwanini huyu mtume Paulo hakumsamehe huyu Yohana aitwaye Marko hata waende naye wawe watatu yaani Barnaba,Yohana aitwaye Marko,pamoja na yeye Paulo wa tatu.Kwanini walishindana na wao ni Wakristo??


JIBU: Ukisoma kitabu cha matendo 13:13 utaona Yohana, aliwaacha wakina Paulo na Barnaba huko Pamfilia, inaonekana aliogopa dhiki itakayokwenda kuwakuta mbeleni, kwasababu Paulo bado mzigo wa kupeleka injili duniani kote alikuwa nao, hivyo walipomsihi waende pamoja alikataa, lakini sasa baadaye tunakuja kumwona tena akikutana na mtume Paulo na Barnaba na kutaka kujumuika nao katika kwenda kuipeleka injili, na ndio hapo tunaona mtume Paulo hakukubali jambo hilo kwasababu kama alishindwa kuandamana nao wakati wa tabu za awali,

kadhalika hataweza kushikamana nao katika dhiki zinazofuata, hivyo sio kwamba Paulo hakumsamehe, alimsamehe lakini hakutaka kuambatana naye tena ili asiwe kikwazo cha injili kwenda mbele.

Ni mfano tunaopaswa tujifunze na sisi [watumishi wa Mungu], kazi ya Mungu si ya kuifanya kirafiki tu, hapana bali wale watakaoitenda kazi kiuaminifu ndio tuambatane nao na kuwatambua hata kama watakuwa si watu wetu wa karibu sana. Lakini ikiwa ni ndugu halafu anaipuuzia kazi ya Mungu, hapo ni kumweka kando, Biblia ilishasema

Wafilipi 2: 12…utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu,


 SWALI 4: Ni sahihi kwa Mkristo mtakatifu kumwambia BWANA ailaze roho ya mtu aliyekufa mahali pema PEPONI?.Mfano mtu huyu ni Yeze amekufa aidha alikuwa Mwema ama muovu sasa ni sahihi kwa Mkristo mtakatifu kusema "Bwana Yesu Ailaze roho ya marehemu Yeze MAHALA PEMA PEPONI"?..


JIBU: Sio sahihi, kwasababu ameshakufa. Tumepewa amri ya kuombeana sisi kwa sisi, yaani tunapokuwa tunaishi hapa duniani, baada ya kufa hatujapewa amri ya kuombeana. Hakuna maombi yoyote yanayoweza kubadilisha hatima ya mtu aliyekufa, kilichobakia kwa mtu aliyekufa ni hukumu tu! (waebrania 9:27).

Mazishi ya watu wasioamini ni tofauti na mazishi ya watu waliomwamini BWANA wetu Yesu Kristo, wasiomwamini wao hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na mambo yatakayofuata baada ya kifo, ndio maana wanasema maneno hayo, lakini sisi tulioamini ndio tunaoelewa kwamba kama ndugu yetu amekufa katika Bwana, basi tunalo tumaini la kukufuka tena kwasababu ni kama amelala tu!.. Lakini kama mtu amekufa katika dhambi na hakumpokea Kristo basi huyo hana tumaini la uzima wa milele, hivyo hawezi kuokolewa kwa maombi yoyote yale. Kwasababu Bwana Yesu alitupa maagizo ya kuenenda ulimwenguni kote kuihubiri injili, AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA, hakutupa agizo la kuenenda ulimwenguni kote kuwaombea wafu waokoke au walazwe mahali pema peponi.

Kwahiyo saa ya wokovu ni sasa katika maisha haya, baada ya maisha haya ni hukumu



Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro veta Dakawa

WhatsApp+255710889892