Alhamisi, 2 Aprili 2026

SOMO:UMHIMU WA MADHABAHU YA MUNGU

SOMO: UMHIMU WA MADHABAHU YA MUNGU NDANI YAKO. 
  
Hili SOMO lahitaji urudie rudie Mara nyingi Ili unielewe na ukinielewa Tu umepona kabisa. 
Madhabahu Ni Nguvu ya uhusiano na kitu. Mtu yeyote lazima awe na madhabahu ya ndani yake inayomfanya Awe hivyo alivyo. Mfano Wewe una Nguvu ya Kuomba Utaomba sawa Ili Maombi yako yakupe  Matokeo lazima Ujenge Madhabahu

Mahusiano hayo unayajengaje Kupitia Sadaka Kitu chochote Unachokiomba Kijengee Madhabahu Ili kukuletea Matokeo. 

Mfano;Unataka Kuolewa Unaomba Maombi ya NDOA lazima Ujenge Madhabahu ya NDOA Ili Mungu anapoleta Malibu yaje yafikie Kwenye Madhabahu ya NDOA ndipo utakapo Jenga kwa kutoa Sadaka ya Madhabahu ya ndoa. 

HAPA CHINI Ni MIFANO YA BIBLIA


. Nuhu: Sadaka ya Shukrani Baada ya Gharika


​Baada ya maji ya gharika kukauka na Nuhu kutoka kwenye safina, jambo la kwanza alilofanya lilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa wokovu.



  • Tukio: Nuhu alijenga madhabahu na kutoa sadaka za kuteketezwa za kila mnyama aliye safi na kila ndege aliye safi.

  • Matokeo: Biblia inasema Mungu alisinzia "harufu ya kuridhisha" na akaahidi kutoiangamiza nchi tena kwa gharika (Mwanzo 8:20-22).

​2. Ibrahimu: Sadaka ya Imani (Isaka)


​Ibrahimu anajulikana kama baba wa imani, na mara nyingi alijenga madhabahu popote alipoishi (kama vile Shekemu na Betheli). Hata hivyo, sadaka yake kuu ilikuwa kwenye mlima Moria.



  • Tukio: Mungu alimjaribu Ibrahimu kwa kumwambia amtoe mwanawe wa pekee, Isaka, kama sadaka.

  • Matokeo: Ibrahimu alijenga madhabahu na kumweka mwanawe juu yake. Mungu alipoona utii wake, alimpatia kondoo wa sadaka badala ya Isaka (Mwanzo 22:1-13).

​3. Eliya: Sadaka ya Kuthibitisha Nguvu za Mungu



​Katika Mlima Karmeli, Eliya alikabiliana na manabii wa Baali ili kuonyesha ni nani Mungu wa kweli nchini Israeli.


  • Tukio: Eliya alitengeneza madhabahu ya Bwana iliyokuwa imebomoka, akaweka nyama ya ng'ombe, na kumwaga maji mengi juu yake.


  • Matokeo: Eliya alipoomba, moto ulitembea kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka, kuni, mawe, na hata kuramba yale maji. Watu waliamini na kusema, "Bwana ndiye Mungu" (1 Wafalme 18:30-39).

​4. Sulemani: Sadaka ya Wingi na Utukufu



​Wakati wa kuweka wakfu Hekalu la Yerusalemu, Mfalme Sulemani alitoa sadaka ambazo hazijapata kutokea katika historia ya Israeli.


  • Tukio: Alitoa sadaka za amani za ng'ombe 22,000 na kondoo 120,000.

  • Matokeo: Moto ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka hizo, na utukufu wa Bwana ukalijaza hekalu kiasi kwamba makuhani walishindwa kuingia (2 Mambo ya Nyakati 7:1-5).

​5. Gidiyoni: Sadaka ya Kukubalika



​Gidiyoni alikuwa na hofu na mashaka juu ya wito wake wa kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Wamidiani.



  • Tukio: Alitayarisha nyama ya mwana-mbuzi na mikate isiyo na chachu na kuiweka juu ya mwamba (kama madhabahu).

  • Matokeo: Malaika wa Bwana aligusa nyama hiyo kwa ncha ya fimbo, na moto ukatoka kwenye ule mwamba na kuiteketeza ile sadaka, jambo lililomthibitishia Gidiyoni kuwa Mungu yu pamoja naye (Waamuzi 6:19-24).

​6. Abel: Sadaka ya Kwanza Iliyokubaliwa


​Huyu ni mwanadamu wa kwanza katika Biblia kurekodiwa akitoa sadaka iliyompendeza Mungu.


  • Tukio: Abel alitoa wazao wa kwanza wa wanyama wake na mafuta yake.

  • Matokeo: Bwana alimtazama Abel na sadaka yake kwa kibali kwa sababu ilitolewa kwa imani na kwa moyo mnyofu (Mwanzo 4:4, Waebrania 11:4).


SABABU ZA WATUMISHI HAWA KUJENGA MADHABAHU

| Nuhu | Shukrani kwa wokovu. |


| Ibrahimu | Utii na imani kwa Mungu. |


| Eliya | Kuthibitisha nguvu za Mungu wa kweli.

 |

| Sulemani | Kuweka wakfu nyumba ya Mungu. |

| Gidiyoni | Kutafuta ishara na uthibitisho wa wito.



JIFUNZE KWA WATUMISHI HAWA KATIKA BIBLIA
πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

              A:NUHU:

Nuhu Alipookolewa Ilibidi Ajenge Madhabahu Ya Wokovu Yeye na Familia Yake Akatoa Sadaka Kukamilisha Ujenzi huo. 

Hata Wewe Kama Kuna Mtu unamuombea aokoke Toa Sadaka Ya Kujenga Madhabahu Sadaka Itakayokuwa Alama nyumbani Pa Bwana. 

Ndio maana Unaweza ukakuta familia yote imeokoka kumbe Kuna Mtu anatoaga Sadaka kwa Ajili ya ndugu Zake wakolewe. 




             B:IBRAHIM:

Ibrahim  Yeye aliitaji Awe mtiifu kwa Mungu na Awe na Imani Ilibidi Ajenge Madhabahu na Aitolee Sadaka Kukamilisha Ujenzi huo Tunaona Anamtoa Isaka.
Kumbe Imani yako kwa Mungu inaendana na kuijenga Madhabahu ya Imani ndani yako na Kutoa Sadaka yako kubwa kuikamilisha Madhabahu yako. 
Huyu alijenga Madhabahu Ya Imani na Utiifu ndani yake


               C:ELIYA:

Eliya alijenga Madhabahu ya Maombi Yenye Kudhibitisha Matokeo Kiukweli Kuna Watu Wengi Tunaomba Maombi Yetu Hatuoni Matokeo Sababu Hatutaki kula gharama ya Kutoa Sadaka kuzifanya Madhabahu Zetu Zikamilike


           D:SULEMANI

Suleman Alijenga Madhabahu Ili Kuwa na Nguvu ya Kumjengea Mungu Nyumba za Ibada Na aliweza Kujenga Jengo la Ibada Kubwa Sana lilojaa Thamani za Dhahabu Tu. 

Ili Tuweze Kuwa na Nguvu ya kuweka Alama ya Ujenzi Wa Makinisa lazima Tutoe Sadaka Zinazoenda Kukamilisha Madhabahu ya Kujitoa Kujenga makanisa. 



             E:GIDION
Gidion Alijenga Madhabahu Ili atumike na Mungu kwa Nguvu ya Udhihirisho hakutaka Atembee na Mungu Wa Kubahatisha alitaka uhakika Wa Mungu alive Naye akimuomba atafanya Kama alivyoomba.



HITIMISHO

Swali La Sisi. 

Tumejenga Madhabahu ya nini ndani Yetu Je Hizi Madhabahu zilizopo ndani Yetu tumezitolea Sadaka Kama Wezetu Walivyozikamilisha Madhabahu Zao. 

Jiulize Hili Swali Kisha chukua mifano ya MTUMISHI Mmoja wapo niliowaeleza mfatilie vitabu nimeviweka hapo ukielewa ukitaka Kujenga Madhabahu utanifata inbox. 

Jenga Madhabahu yako ikutetee ikuletee Matokeo makubwa. 


Wito.

Kama unaswali Juu ya Somo hili umepata Swali maana Tumo humu ili kujifunza nifate inbox nitakujibu au kukuelewesha. 

Naitwa  Pastor Richard Wa Morogoro
WhatsApp+255710889892


#Hurusiwi kunakili au Kukopi bila idhini ya mwenye somo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni