SOMO: NGUVU YA NDANI (THE INNER STRENGTH)
Utangulizi
Nguvu ya ndani si uwezo wa kimwili au akili tu, bali ni uwezo wa Roho Mtakatifu unaofanya kazi ndani ya utu wa ndani wa mwamini. Wakati ulimwengu unategemea hamasa (motivation), mwamini anategemea upako na nguvu inayotoka ndani kwenda nje.
1. Chimbuko la Nguvu ya Ndani
Nguvu hii haitokani na mazoezi ya mwili, bali inatoka kwa Roho wa Mungu. Ni nguvu inayomfanya mtu asikate tamaa hata kama mazingira ya nje ni magumu.
- Maandiko: “Ili kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalie kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.” (Waefeso 3:16)
- Jambo la Kujifunza: Utu wa ndani unahitaji "chakula" na "mazoezi" ili uwe imara kama unavyoulisha mwili wa nje.
2. Tofauti ya Nguvu ya Ndani na Nguvu ya Nje
- Nguvu ya Nje: Inategemea fedha, vyeo, na afya ya mwili. Hizi zinaweza kuchakaa.
- Nguvu ya Ndani: Inafanywa upya kila siku, hata kama mwili unachoka.
- Maandiko: “Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.” (2 Wakorintho 4:16)
3. Faida za Kuwa na Nguvu ya Ndani
- Ustahimilivu (Endurance): Inakusaidia kupita kwenye jaribu bila kuvunjika moyo.
- Ujasiri: Inakupa uwezo wa kusimama mbele ya maadui (Kama Daudi mbele ya Goliati).
- Utulivu: Unakuwa na amani katikati ya dhoruba (Kama Yesu alivyolala kwenye chombo).
- .
4. Jinsi ya Kuitumia Nguvu ya Ndani (The Application)
Hapa ndipo waumini wengi hukwama. Nguvu ipo, lakini namna ya "ku-release" (kuachilia) ndio changamoto. Tumia hatua hizi:
A. Kwa Njia ya Kukiri (Confession)
Nguvu ya ndani inakaa kwenye roho, lakini inatoka kupitia kinywa. Unapokiri neno la Mungu, unaachilia nguvu hiyo kwenye mazingira yako.unayoyapitia na inaleta udhibitisho
- “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:13)
B. Kwa Njia ya Maombi ya Roho (Praying in the Spirit)
Unapoomba kwa lugha, unajijenga nafsi yako (Edification). Hii ni kama kuchaji betri ya simu ili ianze kufanya kazi. Lazima unene kwa Lugha uirusu nguvu itende Ndani Yako
- “Yeye anenaye kwa lugha hujiujenga nafsi yake...” (1 Wakorintho 14:4)
C. Kwa Njia ya Tafakari (Meditation)
Nguvu ya ndani inahitaji mwelekeo. Tafakari neno hadi liwe sehemu ya ufahamu wako. Ukiamini ndani, utatenda kwa ujasiri nje.
D. Kuchukua Hatua ya Imani (Action)
Nguvu ya ndani haionekani mpaka uanze kufanya jambo ambalo linaonekana haliwezekani. Unapopiga hatua, Mungu anaachilia utendaji (Activation).
Hitimisho kwa Kanisa:
Waambie waumini wako: "Mazingira yako yasiamue hatima yako; bali nguvu iliyo ndani yako iamue mazingira yako." Yeye aliye ndani yao ni mkuu kuliko yule aliye katika ulimwengu (1 Yohana 4:4).
WITO
NIFATE WhatsApp Pastor Richard Nikuunge +255710889892
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni