Jumatano, 8 Aprili 2026

SOMO: ADUI KUTANGULIA MBELE YAKO

SOMO: ADUI KUTANGULIA MBELE


​Lengo: Kuelewa mbinu za adui za kuweka vizuizi kabla hujafika na jinsi ya kurejesha mamlaka yako.


​1. UTANGULIZI
Naitwa Pastor Richard
Ninakukaribisha SOMO hil
​Katika ulimwengu wa roho, kuna dhana ya "kutangulia." Kama vile Mungu anavyotangulia mbele yetu kunyoosha njia (Isaya 45:2), adui naye hujaribu kutangulia mbele ili kuchafua mazingira, kuweka mitego, au kufunga milango kabla hujafika kwenye hatima yako. Somo hili litakusaidia kuelewa kuwa vita vingi tunavyopigana leo, vilipandwa jana na adui aliyetangulia mbele.


​2. VITABU VYA KUSOMA

​Ili kupata picha kamili ya somo hili, pitia maandiko haya: Tafakari kwa Kina. 


​Kutoka 23:20-23 (Mungu anapotuma malaika atangulie).


​Mathayo 13:24-30 (Mfano wa ngano na magugu – adui alitangulia kupanda magugu usiku).


​Zaburi 139 (Mungu anavyojua mienendo yetu)..


​Waefeso 6:10-18 (Silaha za vita).


HASARA YA ADUI KUTANGULIA MBELE YAKO


1:Hasara: Mitego ya Siri Adui anapotangulia, huandaa mashimo na mitego ambayo huwezi kuiona kwa macho ya nyama.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ
 Zaburi 140:5 — "Wenye kiburi wamenificha mtego na kamba..."


2:Hasara: Kukatishwa Tamaa Unapofika kwenye fursa, unakuta "milango imefungwa" tayari kwa sababu adui alishachafua sifa yako mapema. 
πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ
Hesabu 13:31-33 — Wapelelezi walitangulia na kuleta ripoti mbaya.

FAIDA ADUI KUTANGULIA MBELE YAKO

1:Faida: Tahadhari  Kujua kuwa adui ametangulia hukupa 
"Inakupa tahadhari Huwezi kuingia kichwa kichwa; unakuwa na umakini wa kiroho. 


2 Wakorintho 2:11 — "...tusishindwe na Shetani; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake."


2:Faida: Ushindi wa Kishindo Adui anapotangulia na kushindwa, ushindi wako unakuwa mkubwa zaidi na unamtukuza Mungu mbele ya maadui. 


Zaburi 23:5 — "Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu."


NIFANYE NINI SASA?

 (Mwelekeo Wa Kibiblia) 


​Ili kukabiliana na adui aliyetangulia, fanya yafuatayo:


1;​Tuma Neno na Malaika Watangulie: 


Kabla hujaanza safari au mradi, amuru malaika wa Mungu watangulie mbele yako kufuta kila mtego wa adui.


​“Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani...” (Kutoka 23:20)


2:​Vunja Misingi ya Kale:

 Omba kuvunja kila agano au madhabahu ambayo adui aliijenga mahali unapoenda kabla hujafika.


3:​“Bomoeni madhabahu zao, vunjeni nguzo zao...

” (Kumbukumbu 7:5)
​Omba kwa ajili ya Upako wa Uvumbuzi 


4:Mwombe Roho Mtakatifu akuonyeshe yaliyofichwa mbele yako.


​“Yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri...” (Danieli 2:22)


HITIMISHO


​Adui anaweza kujaribu kutangulia mbele yako ili kukatisha tamaa safari yako, lakini kumbuka kuwa Mungu wetu ndiye Alfa na Omega – Yeye yuko mwisho wa safari yako akikusubiri, na yuko mwanzo akikuongoza. Hakuna mtego wa adui uliotangulia unaoweza kushinda mamlaka ya Jina la Yesu.



​WITO


​Je, unahisi kila unapopiga hatua unakutana na vizuizi visivyoeleweka? Usikubali kushindwa. Ni wakati wa kutumia mamlaka uliyopewa kupangusa njia yako kiroho.


​Wasiliana na Pastor Richard Kwa WhatsApp:
+255710889892

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni