SOMO;Jinsi Mazoea Yanavyozuia Baraka Zako
1. Mazoea Huzaa "Dharau ya Kiroho"
Unapomzoea Mungu, neno lake linaanza kuonekana kama hadithi za kawaida. Unaposikia mahubiri, badala ya kusema "Mungu nasikia usemi wako kwangu," unasema "Hili neno nimeshalisikia mara nyingi."
- Athari:
- .
- Baraka hupitia kwenye Neno. Ukidharau chanzo (Neno), unazuia mtiririko wa baraka hiyo maishani mwako.
- Maandiko:
- “Alipeleka neno lake, akawaponya...” (Zaburi 107:20). Ukizoea neno, unakataa uponyaji wako.
2. Kufanya Ibada Kuwa Mapokeo (Routine)
Mungu anatafuta uhusiano, si ratiba. Mazoea yanakufanya uombe kwa sababu ni saa ya maombi, si kwa sababu una kiu na Mungu. Unatoa sadaka kwa sababu ni utaratibu, si kwa sababu ya upendo na imani.
- Athari: Mungu anajidhihirisha kwa watu
- wenye kiu (Isaya 44:3).
- Mazoea yanakatisha kiu hiyo, na bila kiu, hakuna maji mapya (baraka mpya).
3. Kupoteza "Unyeti" wa Kiroho (Spiritual Sensitivity)
Mungu anapozingatia muda na majira, anatoa maelekezo ya namna ya kutenda. Lakini mazoea yanakufanya utende kwa kutumia akili na uzoefu wa jana.
- Mfano:
- Joshua aliambiwa azunguke kuta za Yeriko (silaha ya sifa). Kama angekuwa na mazoea ya vita vya kawaida (panga na mishale), asingeona muujiza ule.
- Athari:
- Unakosa fursa za msimu wako (Season) kwa sababu unatumia mbinu za msimu uliopita.
4. Kumfanya Mungu "Mdogo" mbele ya Shida
Mazoea yanakufanya uamini kuwa unamjua Mungu kiasi kwamba unajua "hadi hapa hawezi." Unaanza kupima uwezo wa Mungu kwa kulinganisha na uzoefu wako wa nyuma.
- Athari:
- Unazuia Miujiza ya Kiwango cha Juu (Creative Miracles) kwa sababu imani yako imefungwa na kile ulichozoea kuona.
5. Kupoteza Kibali (Favor) Mbele za Mungu
Mungu anatembea na unyenyekevu. Mazoea huleta kiburi cha siri—kujiona kuwa "mwenyeji" katika mambo ya Mungu (Spiritual Entitlement). Unajiona unastahili baraka kwa sababu umekuwa kanisani miaka mingi.
- Athari:
- Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa wanyenyekevu neema (1 Petro 5:5). Mazoea yanakunyang'anya neema na kukuacha na jitihada zako mwenyewe.
Hatua za Kuchukua ili Kuvunja Mazoea:
- Omba Upya wa Akili:
- Mwombe Mungu akusaidie kumwona kwa upya kila asubuhi.
- Tafuta Siri Mpya:
- Usisome Biblia ili umalize sura, isome ili upate maelekezo mapya kwa ajili ya leo.
- Heshimu Madhabahu na Watumishi:
- Usiwazoee wale ambao Mungu amewatumia kukubariki. Ukimzoea nabii, unapoteza thawabu ya nabii.
- Zingatia "Sauti ya Sasa":
- Usiishi kwa ushuhuda wa miaka kumi iliyopita; tafuta nini Mungu anasema na wewe SAIVI.
Kumbuka hili Mtu Wa Mungu
Mungu hadhibitiwi na muda wetu, bali Yeye anatumia muda kutupima kama bado tuna imani na kicho kwake. Usichoke kusubiri, na usizoelewe na hali ya sasa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni