Ijumaa, 27 Septemba 2024

MSINGI IMARA WA NDOA

          SOMO; MSINGI IMARA WA NDOA 

Naitwa Mwalimu wa Wanandoa Pastor Richard Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 
Msingi Wa Ndoa Huanzwa Kujengwa Kwenye Uchumba Kabla hata hujampata mtu wako Sahihi Isaka Anasema Wakati Anamtafuta Rebeca Akaweka Vingezo Au Sifa Ya Kile Anachokitaka. Hicho ndicho kilichowaunganisha Rebecca na Isaka Vingezo alivyo navyo Rebeka Wengine hawakuwa navyo.

1;MSINGI WA KWANZA ANASIFA TOFAUTI NA WENGINE NDIYO MAANA UMEMPENDA.
Mwanzo;24 Habari ya ndoa ya Isaka.

Mwanamke au Mwanaume Mpaka Unakubali kuolewa au Kuowa ukafunga ndoa umemuona Anasifa tofauti na Wanawake Wengine heshimu hilo na ulinde na kutunza siyo siku mbili tu umeanza kuona Sifa zile hana umeanza kutamani wengine.


2:MSINGI WENU WA PILI; RUHUSU MUNGU MWENYEWE AWE MJENZI WA NDOA YENU.

Mnapoyapa nafasi maombi na Ibada Kwenda Kanisani kuomba kuombea malengo yenu na Kuwa Waaminifu Wa Fungu la Kumi  Mnamfanya Mungu Aijenge ndoa Yenu Vizuri Tena Kwa Upendo  

SOMA HII MISTARI;
             Zaburi:127;1
Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. 

       2 Wakorintho 3:17 
 Basi ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
===========================/

2:WAPENDENI NDUGU ZENU PANDE ZOTE MBILI;
Wakija ndugu kuwatembelea Unaweza ukaandaa kasupu kawasaki na Vinyard vya kukaaga mama wake zako unawakaribisha huku unajiongelesha yani huku mboga za shida Tumeamua tuwaandalie hii Mboga Mtusamehe tu. Wanawishe kwa heshima hapo.

     SOMA MISTARI HAYA:
             Warumi 12:10-15
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;

12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;

13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.

14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.

15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.

===========================

3:MSHIRIKIANE NA JAMII INAYOWAZUNGUKA MFANYIKE BARAKA KWA JAMII:

Shirikiana Na Jamii Katika Mambo Ya Msingi Ambayo hayakutengi na Mungu wako kama msimba maendeleo na Harusi mbalimbali nk unapokuwa umepewa taarifa.

      Mithali 1:14-16
14 Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika.

15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.

16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.

=================================

4:LINDENI HESHIMA YENU.

Jamii inayowashuhudia kwenye tukio la ndoa ambalo Tunalitaja Kuwa la heshima hiyo hiyo jamii itakuja kuwashagaa Mkija Kufanya mambo ya Ajabu.

Mfano; Mkaanza Kupigana Au Kunyanyasa watoto wenu mtakaobarikiwa nao.

Kosa lingine lipo kwa Mwanandoa Akaanza kumpa nafasi za mke wake mwanae mfano ukipata pesa mwanao ndiyo unamkabidhi mkeo anamuomba mwanao au kwenda kulala chumbani kwa mwanao Hii inaondoa heshima Sana.

MISTARI YA KUSOMA

         Zaburi 111:3-5
3 Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele.

4 Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; Bwana ni mwenye fadhili na rehema.

5 Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele.

=================================


5:MIOYO YENU IFUNGUKE NA KUWEKANA WAZI USIYOYAPENDA NA UNAYOYAPENDA.

Hakikisheni Tabia Ambazo Unaziona Zinataka Kuingia kwa Mwezako Unakaa naye chini Kwa Utaratibu Na Kwa Heshima muulize Tu Kwanini Anafanya Kitu Ambacho Ulishamwambia Hupendi Pia Mweleze Wewe Unapenda hiki na hiki.
===============================
MISTARI YA KUSOMA

          Mithali 17:26-28
26 Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri; Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.

27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.

28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
==============================

6:MALIZENI TOFAUTI ZENU NYINYI WENYEWE.

Kila Mnapokuwa mmetofautiana Au Kugombana Mnatakiwa Mmalize Tofauti Zenu Wenyewe bila kuzitoa nje. Msifanye Tofauti Zenu Zikafikia Hatua Zikawa Kubwa mpaka mkashindwa kuzitatua.
=======÷==========÷÷÷÷÷÷==========
MISTARI YA KUSOMA 
     Wakolosai 3:13-17
13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


7:CHANGUENI WALEZI WA NDOA  YENU WALIOKAA MUDA KWENYE NDOA 

Sifa za Mlezi wa ndoa 
a)Awe Amedumu kuanzia miaka 3 Nakuendelea

b)Awe na Hekima na Busara

C)Awe Mwenye Kuingwa na Mfano wa ndoa yake.

          Mithali 11:14 
 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.


8;Kila Mmoja Aufundishe Moyo wake Kupenda na Kuongea maneno ya Hekima .

Nyinyi ni Wanandoa Mnatakiwa Kupendana na Kuvumiliana Kila changamoto mtakayokuwa mnakutana nayo.

     ⁶Yohana 13:34
 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.


9:MANENO MATATU YENYE USHINDI 

1:Vumilia Katika Kila Kipindi

     1 Petro 2:19  
Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.

2:Usiongope changamoto za Kwenye ndoa

          Yeremia 1:8 
 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.

3;Amini Kila Jambo linasababu yake.

            Mhubiri 3:1 
 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.


10;MAFANIKIO NA UPENDO NDANI YA NDOA

MAFANIKIO HUJENGWA NA VITATU HIVI;

1;MUNGU AWE NAMBA MOJA.
Msifanye jambo lolote bila kumhusisha Mungu.

2;MKEO AWE NAMBA MOJA .
Usifanye kitu chochote bila kushauriana na mkeo

3:MUME AWE NAMBA MOJA.
Usifanye Kitu chochote bila kushauriana na mumeo.


UPENDO HUJENGWA NA VINNE.

1;Tumia Neno la "NAKUPENDA" lifelike kwa mwezi wako mara kwa mara 
Muite majina mazuri mazuri Hanny Sweet My love mke wangu mume wangu nk

2:Tumia Neno "SAMAHANI" kila mnapokoseana au kwenda tofauti  tumia neno Samahani mume wangu.


3:Tumia Neno "ANSATE" kila unapoletewa kitu au kupewa kitu na mwezi wako.

4:Tumia Neno "POLE" Kila Unapomuona mwezako ametoka kazini au chochote Kile Kinachoonesha neno hili litumie.



Nataka Kusema Ndoa inajengwa na nyinyi wawili na wawili nyinyi mnaweza Kuivunja ndoa  Lindeni Agano hili mnalolipokea leo liwe mfano wa Kuingwa kwenye mioyo Yenu..


@Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 




Kanuni 10 za Uchumba


Somo:Kanuni 10 za Uendeshaji wa Uchumba

Picture
Kwanza

Wewe na mwenzako mnaweza kuwa na sifa nyingi kama wachumba. Huenda mkijitazama na watu wakiwaona, hakuna anayetilia mashaka kwamba mna wasifa na mmekomaa tayari kwa ndoa. Lakini kama dereva yeyote aliye na sifa anavyopaswa kuzingatia sheria za udereva, mnapaswa kuzingatia kanuni za uendeshaji uchumba ili mfanikiwe kusomana kama mnafaana kwa ndoa. Zipo kanuni nyingi, nafasi ni finyu na muda hautoshi. Lakini niruhusu nishiriki nawe kanuni hizi chache zikizo na uzito usiopungua busara na maarifa ya kimbingu:
Naitwa pastor Richard Wa Morogoro
Katibu nikukaribishe. 


1. Mruhusuni Mungu awe Mjenzi mkuu wa uchumba wenu

Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. (Zab 127:1)

Wachumba wanaomkaribia Mungu huishia kukaribiana wao kwa wao. Mungu akiwa juu ya pembe tatu, umbali baina yao hupungua kila mmoja anapomkaribia Mungu. Tafuteni muda wa kusoma vitabu vya uvuvio na kuomba pamoja, nanyi mtauweka uhusiano wenu katika msingi imara.

2. Uwekeni uchumba wenu wazi mbele ya watu wanaowapenda

Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? (Mwa 4:9)

Tambueni kuwa wanandugu wanaowapenda ninyi ni walinzi wa kuaminika wa ndoto yenu kuunganika mwili mmoja. Waruhusuni wazazi wenu, ndugu zenu na rafiki zenu wanaowafahamu waufahamu na kuukaribia uchumba wenu. Uchumba si siri. Msiwaweke mbali nanyi wanaowatakia mema maishani—hao ni walinzi wenu wa kuwaangalia, msiwafiche. Wanaweza kuwasaidia kuyaona msiyoyaona. Kumbukeni, nyani haoni kundule.

Picture
3. Jichanganeni na jamii katika shunguli za kijamii

Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa. Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote. Basi yule mtu akamkazia macho…(Mwa 24:19-21)

Mnapojihusisha katika shughuli za kijamii mna unajianika ulivyo. Rebeka alipomsaidia mgeni asiyemfahamu hakujua anajitangaza kwa mshenga. Na mshenga alipopokea msaada wa Rebeka, hakuchelewa kumvika pete ya uchumba kwa niaba ya Isaka, mme mtarajiwa. 

Zaidi ya wengine kuwatambua, ninyi kwa ninyi mtazidi kufahamiana. Wewe na mchumba mwenzako mnapojumuika na familia zenu, majirani wenu, au waumini wenzenu katika arusi, misiba, au kazi yoye inayowajumuisha na watu wengine mtapata fursa ya kufahamiana zaidi ninyi kwa ninyi. Kila mtu hujitambulisha tofauti tofauti kulingana na mazingira aliyopo. Utang’amua sura mpya au tofauti ya mwenzako anapokuwa katika mazingira tofauti na mnayokuwepo mkiwa wawili tu. 

Picture
4. Lindeni majina yenu yasiingie madoa

Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. (Mith 22:1)

Ninyi ni watoto wa Mungu na mnaitwa hivyo. Msijiachie kwenye majaribu ya mapenzi na kuruhusu jina mlilopewa na Mungu lipakwe madoa ya kashfa. Bora uwe muoga kuvunja miiko ya maadili kuliko jasiri kujiachia na kuchafua jina lako la thamani. Uchumba wenu ukiheshimiwa na watu, ndoa yenu itapanda thamani machoni penu na mbele ya jamii—hata hakuna kati yenu atakayeona rahisi kutilia mashaka kwamba Mungu habariki mipango yenu.

5. Msiwashane moto wa mapenzi msioweza kuuzima

Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha (Wimb 8:7) Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe (Wimb 2:7)

Japo si ajabu kwa wapendanao kuoneshana hisia kuwa wanapendana; lakini, hisia hizo zinapaswa zioneshwe kulingana na kiwango na mipaka ya uhusiano uliopo.  Kubalianeni miiko ya kuizingatia. Msiwe mabubu. Badala ya kuonesha hisia kimyakimya,ongeeni wazi wazi. Kila mmoja ajue maeneo yasiyoingiliwa. Mnapochora pamoja mstari mwekundu usiopaswa kuvukwa kama wachumba, na kila mmoja akawajibika kuiheshimu basi uhusiano wenu utazidi kupanda thamani machoni penu wenyewe na mbele za jamii.

Picture
6. Fungukeni mioyo na ongeeni kwa uwazi bila kufichana

Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu. Mithali 17:28
Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake. Waef 4:25


Kuwa huru na wazi kwa mwenzako kadri uhusiano wenu unavyosonga ili mzidi kufahamiana. Ukifungua moyo wako wazi mno na mapema mwanzoni mwa uhusiano wenu utamshtua mwenzako (hatuvui nguo kwa mgeni). Lakini pia ukiufunga moyo wako na kumzuia mwenzako asichungulie kurasa za nyuma za maisha yako, mwenzako atashindwa kukukaribia ili kufahamu (mficha uchi hazai). Lakini huitaji kumvulia nguo ili akufahamu. Funguka moyoni apate kukujua. Kadri unavyofunguka ndivyo naye atafunguka na pamoja mtazidi kufahamiana.

7. Malizeni tofauti zenu kistaarabu mara zinapojitokeza

Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka. Waef 4:26

Usikae na kinyongo moyoni. Uchungu ni sumu inayoanza kummaliza  anayeitunza moyoni kabla haijamjeruhi yeyote aliye karibu. Mwageni yote machungu ya moyoni katika meza ya mazungumzo. Zungumzieni tofauti zenu kwa uwazi kama watu mnaopendana na kuheshimiana. 

Ongea uso kwa uso mkiangaliana na si nyuma ya mgongo wa mwenzako. Ongea wakati hisia kali zimepungua, na katika mazingira tulivu. Jifunzeni kugongea katika namna ambayo mwenzako atakuelewa.

Usipuuzie. Usidhani magugu ya uchungu moyoni yanajiozea unapojizuia  kuyazungumzia. Anika uchungu wote mbele ya jua la ukweli kabla hujawa na hakika ya kuwa mizizi yake imeunguzwa kabisa hata haiwezi kuchipuka tena na kuwasumbua.

8. Chagueni wanandoa waliowatangulia watakaolea uchumba

Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. (Mith 11:14)

Mnapoendelea na safari ya kusawazishana, hamna sababu ya kubahatisha pa kukanyaga na mwishowe muanguke kama wapo waliowatangulia wanaweza kuwaelekeza njia salama. Tafuteni wanandoa ambao wote mnavutiwa nao kama mfano wa kuigwa na muwafanye walezi wa uchumba wenu.  Wawe walezi ambao mpo huru kwao kuwaeleza mashaka na hofu mlizo nazo. Wazazi wanaoweza kuwashauri maswala ya utawala wa fedha, uhusiano na wanandugu, uzazi wa mpango, tendo la ndoa na kadharika. 

Haitoshi kusoma vitabu au kuhudhuria semina za uchumba. Jifunze pia moja kwa moja toka kwa maisha ya wanandoa mbalimbali mlio karibu nao.

Picture
9. Kila mmoja ajifunze kuongea lugha ya upendo ya mwenzake

Amri mpya nawapa, Mpendane (Yoh 13:34) Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo. (Gal 6:2)

Kila mmoja wenu ana lugha ya upendo aliyokuzwa nayo. Unaitumia kirahisi kuonesha unapenda na ikitumika unahisi kupendwa. Si rahisi wapenzi wawili wakutane wanaongea lugha moja ya mama. Gundua lugha yako kwa kujiuliza: Nimezoeaje kuonesha upendo kwa wengine? Mara nyingi ninanungunikia nini? Muda mwingi ninaomba nini? Ukimgeuzia mwenzako maswali hayo hayo utagundua lugha yake. Jambo la muhimu ni kupenda katika namna ambayo mwenzako atakuelewa unampenda.

Nategemea kila mmoja wenu atakuwa anatumia mojawapo ya lugha hizi kuu za upendo kama zilivyofafanuliwa na Dr Gary Chapman. Nitazijadili kwa undani wakati mwingine. Lakini kwa sasa nizitaje, nazo ni: (a) lugha ya maneno ya kujali, (b) lugha ya kupeana zawadi, (c) lugha ya kusaidiana, (d ) lugha ya kutumia muda mwafaka pamoja na (e) lugha ya mguso wa upendo (miguso salama na inayokubalika). Unapojifunza kumpenda mwenzako zaidi ya ujuavyo wewe na kama ajuavyo yeye utakuwa unatekeleza vilivyo sheria ya Kristo.

10. Ingia katika uhusiano wa uchumba kama upo tayari kwa ndoa

Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu (Mhu 3:1)

Kusudi la uchumba chini ya mbingu ni kukuandaa wewe na mwenzako kwa ndoa. Kama unachumbia hata kwa kuzingatia kanuni tajwa hapo juu lakini hauko tayari kwa ndoa basi uhusiano wenu hauna maana. Ingia katika uchumba kama muda umewadia. Ingia kwenye uchumba na mtu unayedhani anaweza kuwa mwenzi wa maisha. Kuingia katika mahusiano na mtu yeyote kwa sababu amekuvutia kimwili lakini huoni anafaa katika maagano ya milele si salama. Usicheze na mkondo wa mapenzi unaopita kwa kasi. Utajitambua baada ya kunywa maji.


Mwisho

Huenda kanuni nilizozijadiri hapo juu ni kama marudio kwako, hilo sishangai. Na sioni ajabu dereva aliyepitia mafunzo, mwenye sifa zote, na kupewa leseni ya uendeshaji vyombo vya moto akipata ajali. Usipoendesha uchumba wako kwa kanuni zinazomulikwa na nuru ya Maandiko, hakika utajikwaa kabla ya kufika uendako. Kwa kuwa natamani ufaulu, nimekukumbushia kanuni hizi za uchumba kwa mkazo na si zaidi.

Ninamaliza kuchapa mstari huu wa mwisho nikimpigia Mungu Baba, “Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu” (Yuda 24)

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

WhatsApp

Jumamosi, 14 Septemba 2024

SOMO;MADHARA YA KUCHEZEA AGANO LA NDOA

SOMO: MADHARA YA KUCHEZEA AGANO LA NDOA.

Kuna watu wamekuwa wakichukulia kuowa au kuolewa ni kama mchezo fulani Ambao utaenda madhabahuni  unaapa na kufungishwa ndoa baada ya muda Anavunja uaminifu au ndoa kimya kimya Tena Anaenda kuolewa au kuowa pasipo kupeana Talaka kisheria Hii huwa hatari kuliko hata ugonjwa mtu anaweza kutibiwa.


1:Madhara utakayoyapata usipompa talaka kwa kosa la uzinifu au hana nguvu za kiume au nguvu za kike. Hili kosa uwe na Ushahindi umeona mwenyewe mwezako anatatizo hili ukienda kinyume eidha kwa sababu zingine nje na hizi utakuwa umeivunja ndoa mwenyewe na utateseka mno tena sana kuliko ulivyodhania.


2:Ndoa Isiyo na maelewano Takiribani ni mwaka mmoja ndani ungomvi hii inavunjika kwa sababu mnaweza kuja kuuwana ni bora mkatengana lakini Hampigani mnanuniana tu ukataka ndoa uvunje itakutesa sana.

3:Hurusiwi Kuivunja ndoa ikiwa hata mwaka haijamalizika ukifanya hivyo utaadhibiwa kimaisha Utatembea na laana isiyofutika.


4:Hutakiwi Ndoa yako uivunje kienyeji ukarukia moja kwa moja mahakamani bila kuanza huku chini kwa msajili wa ndoa nikosa kubwa Sana Usipofata utaratibu hiyo laana itakutesa milele.


5;Msajili Akisema hapana hata mbele huku hutakumbalika maana hamkukaa ulijiamulia tu hakikisha unafata utaratibu wa kisheria unapotaka kuvunja ndoa.


6:Ndoa inaweza kuvunjwa na hawa wawili wakawa huru lakini siyo rahisi rahisi sababu ambazo hazina mashiko.

Kwa Mungu Inamuonya huyu mtu anayeingia Kwenye ndoa Baada Ya Muda Anadai ndoa ivunjike chezea vyote usije ukacheza na Agano la ndoa

Tunasoma
Marko 10:9 
 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.



HITIMISHO 

Ndoa inaitaji ilindwe na watu wote ikiwemo nyinyi Wanandoa Ndoa Siyo fashion

Jumatatu, 9 Septemba 2024

MAOMBI YA KUOMBA KUFUNGUA KIZUIZI



        DARASA LA MAOMBI 

SOMO: MAOMBI YA KUFUNGUA KIZUIZI.

Ukiona Unataka ufanye kitu kinaingilia kitu kilichokuwa haikipo kwenye hesabu zako ujue hizo ni Vizuizi.
Mfano; Unanyumba Unauza Wateja wanafika pale mnapanga bei gafla wakirundi wanasema hawanunui ujue kuna Kizuizi.

UNACHOTAKIWA UOMBE SASA.

Utafata hivi ninavyoelekeza 

KWANZA TAFUTA MSTARI 

Tunasimamia:
Marko 3:27 Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

"Baba Nasimama Sawasawa  Na Neno lako Katika Kitabu cha Marko:3:27 Namuondoa huyo Mtu Anayenizuia Mimi Au Kuweka uchawi wake wa Kunirundisha nyuma Kwa Jina la Yesu Navunja vipande Magongo na Kamba Zilizofunga hili swala langu la ndoa au Kiwaja au Kazi nisipate Kwa Jinaa la Yesu Fuguka Fuguka fuguka kwa sasa nakuendelea sitaki kuwa mnyonge Kuanzia muda huu nitakuwa na nguvu na nguvu kweli kweli Ninaomba Kwa Imani ya Jina la Yesu.Amen 

RUDIA ×8 KUOMBA

Kama Hujaungwa Kwenye Group la Maombi na Mafundisho mfate WhatsApp Pastor Richard Akuunge +255759861768 Utajibu maswali kabla hujakubaliwa kuwa mwanangroup


Jumamosi, 7 Septemba 2024

Maswali na majibu Jumapili.9/9/2024

   DARASA LA
BIBLIA MASWALI NA MAJIBU  

Karibu katika Kipindi Kipya kitakakuinjia kwenye Group letu la Maombi Kila Jumatatu Asubuhi Lengo Ni Wewe Kuendelea Kuzidi kujifunza Maswali na Majibu mbalimbali 
Hakikisha unaandika maana usije ukaniambia nirushe swali ambalo lilishapita kuanzia Leo Anza Kufatilia.
Naitwa Pastor Richard 

TUMEANZA NA HAYA MASWALI:    

 Swali:1
Nini Kitanizuia nisibatizwe kwa maji mengi..?
Ni kitabu ngani kinasema hivyo na Ni nani aliyesema maneno hayo..?

Jibu;Matendo;8:36

              Swali:2
Biblia haikuandikwa mambo yote ingeandikwa kitabu kisengetosha..?
Kitabu ngani kinasema  maneno haya.
A.Mwanzo
B.Hesabu
C.Luka
D.Yohana 21:25✅
E.Zaburi.

             Swali: 3
Utatu mtakatifu ulifunuliwa au ulitambulishwa lini kwetu mpaka Tukaujua..?

Jibu;Kipindi cha Ubatizo wa Yesu. 
Mathayo;3;16-17


       Swali:4
Swali la Kwanza Toka Dunia iumbwe  liliulizwa na nani..? Aliliuliza Akiwa  Wapi..?

Mwanzo:3:1



MASWALI NA MAJIBU JUMAPILI TAR.15/9/2024

🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🎈
SWALI;1

1:Yesu alipoletwa Hekaluni akiwa mtoto mchanga, ni nani aliyemtambua kuwa ndiye Masihi?

Jibu: Simeoni ( Luka 2:22-38 ).


SWALI:2

2. Ni mgombea gani ambaye hakuchaguliwa kwa wadhifa wa mtume baada ya Yuda Iskariote kujiua, kulingana na Matendo ya Mitume?

Jibu: Yusufu Barsaba (Matendo 1:24–25).


SWALI:3

3. Ni vikapu vingapi vilivyobaki baada ya Yesu kuwalisha wale 5,000?

Jibu: Vikapu 12 (Marko 8:19).


SWALI:4

4. Katika mfano unaopatikana katika Injili tatu kati ya nne, Yesu alilinganisha mbegu ya haradali na nini?

Jibu:  Ufalme wa Mungu ( Mt. 21:43 ).


SWALI:5

5: Musa alikuwa na umri gani alipokufa, kulingana na kitabu cha Kumbukumbu la Torati?

Jibu: Miaka 120 (Kumbukumbu la Torati 34:5-7).


SWALI:6

6: Ni kijiji gani kilikuwa mahali pa kupaa kwa Yesu, kulingana na Luka?

Jibu: Bethania ( Marko 16:19).


SWALI:7

7. Ni nani anayefasiri maono ya Danieli ya kondoo mume na beberu katika Kitabu cha Danieli?

Jibu: Malaika Mkuu Gabrieli ( Danieli 8:5-7 ).



TAR.22/9/2024 JUMAPILI 


SWALI:88:Ni yupi kati ya mke wa Mfalme Ahabu, aliyetupwa kutoka dirishani na kukanyagwa kwa miguu?

Jibu: Malkia Yezebeli (1 Wafalme: 31).



 

 Nifanye nini ili niokolewe?

  •  Unapaswa kuamini kwamba Yesu alidhabihu uhai wake kwa ajili ya dhambi zetu. (Matendo 16:30, 31; 1 Yohana 2:2) Hilo linamaanisha kuamini kwamba Yesu alikuwa mtu halisi na kwamba mambo yote ambayo simulizi la Biblia linasema kumhusu ni sahihi.

  •  Jifunze kile ambacho Biblia inafundisha hasa. (2 Timotheo 3:15) Biblia inasema kwamba mtume Paulo na Sila walimwambia hivi mlinzi wa jela: “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokolewa, wewe na watu wa nyumba yako.” Kisha, baada ya hapo, walianza kumfundisha mlinzi huyo wa jela “neno la Yehova.” a (Matendo 16:31, 32) Hilo linaonyesha kwamba mlinzi huyo wa jela hangeweza kumwamini Yesu bila kuwa na ujuzi wa msingi wa Neno la Mungu. Alihitaji kuwa na ujuzi sahihi wa Maandiko.—1 Timotheo 2:3, 4.

  •  Tubu. (Matendo 3:19) Pia, lazima utubu, au uhuzunishwe sana, kuhusu mwenendo na mtazamo mbaya uliokuwa nao. Wengine wataona toba yako kadiri unavyoacha mazoea yanayomchukiza Mungu na unapofanya “matendo yanayoonyesha toba.”—Matendo 26:20.

  •  Ubatizo. (Mathayo 28:19) Yesu alisema kwamba wale ambao watakuwa wanafunzi wake wanapaswa kubatizwa. Mlinzi wa jela aliyetajwa hapo awali alibatizwa. (Matendo 16:33) Vivyo hivyo, baada ya mtume Petro kufundisha umati mkubwa ukweli kumhusu Yesu, “wale waliokubali neno lake kwa furaha wakabatizwa.”—Matendo 2:40, 41.

  •  Tii maagizo ya Yesu. (Waebrania 5:9) Wale ambao ‘wanashika mambo yote’ ambayo Yesu aliamuru wanaonyesha kupitia maisha yao kwamba wao ni wafuasi wake. (Mathayo 28:20) Wanakuwa “watendaji wa neno, na si wasikiaji tu.”—Yakobo 1:22.

  •  Vumilia mpaka mwisho. (Marko 13:13) Wanafunzi wa Yesu ‘wanahitaji uvumilivu’ ili         


3:Mtu Akianguka kwenye dhambi na alikuwa Ameokoka shetani humpiga mara mbili yake
Kitabu ngani kinasema hivi.

Jibu; Waebrania;6;4-6




4:Biblia Ni nini?

Jibu la Biblia

 Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vitakatifu. Iliandikwa katika kipindi cha miaka 1,600 hivi. Biblia ina ujumbe kutoka kwa Mungu—“neno la Mungu.”—1 Wathesalonike 2:13.

Tar.7/10/2024

5:TUNAJIFUNZA NINI KWA ABIGAIL
Baadhi ya wanawake wanaotajwa kwenye Biblia

Wanawake Katika Biblia—Tunaweza Kujifunza Nini Kutoka Kwao?


Jibu la Biblia

 Katika Biblia, tunasoma kuhusu wanawake wengi ambao maisha yao yanatufundisha masomo yenye thamani. (Waroma 15:4; 2 Timotheo 3:16, 17) Makala hii inazungumzia kwa ufupi tu baadhi ya wanawake wanaotajwa katika Biblia. Wengi wao ni mifano mizuri ya kuiga. Wengine ni mifano ya kuonya.—1 Wakorintho 10:11; Waebrania 6:12.



Abigaili

  Abigaili

 Abigaili alikuwa nani? Alikuwa mke wa mwanamume mkatili aliyeitwa Nabali. Hata hivyo, Abigaili alikuwa mwenye busara na mnyenyekevu, na pia alikuwa mrembo kimwili na kiroho.—1 Samweli 25:3.

 Alifanya nini? Abigaili alitenda kwa hekima na busara ili kuzuia msiba. Yeye na Nabali waliishi katika eneo ambalo Daudi, mfalme mtarajiwa wa Israeli, alikuwa akijificha. Daudi na wanaume wake walipokuwa huko, walilinda makundi ya kondoo ya Nabali yasiibiwe. Lakini Daudi alipowatuma wajumbe kumwomba Nabali chakula, Nabali aliwatukana na kukataa. Daudi alikasirika sana. Kwa hiyo, yeye na wanaume wake wakapanga kwenda kumuua Nabali na wanaume wote wa nyumba yake.—1 Samweli 25:10-12, 22.

 Abigaili alitenda upesi aliposikia kile ambacho mume wake alikuwa amefanya. Aliwapa watumishi wake chakula wampelekee Daudi na wanaume wake, naye pia akawafuata ili kumwomba Daudi awaonyeshe rehema. (1 Samweli 25:14-19, 24-31) Daudi alipoona zawadi yake, unyenyekevu wake, na aliposikia ushauri wake wenye hekima, alitambua kwamba Mungu alimtumia ili kumzuia asimuue Nabali na wanaume wake. (1 Samweli 25:32, 33) Muda mfupi baada ya hapo, Nabali alikufa, naye Abigaili akawa mke wa Daudi.—1 Samweli 25:37-41.

 Tunajifunza nini kutoka kwa Abigaili? Ingawa alikuwa mrembo na tajiri, Abigaili alikuwa na maoni yenye usawaziko kujihusu. Ili kudumisha amani, alikuwa tayari kuomba msamaha kwa jambo ambalo halikuwa kosa lake. Alishughulikia hali yenye kutisha kwa utulivu, busara, ujasiri, na alitumia nguvu zake za kufikiri.

  •  Ili kupata habari zaidi kumhusu Abigaili, ona makala yenye kichwa, “Alitenda kwa Busara.”

Debora

  

Jumapili Tar.13-10-2024

MASWALI YA BIBLIA

SWALI;

1; Ni Mwanamke Ngani Wa Kwanza Kujifungua Akafa Akijifungua Mtoto Kwenye Biblia Mtaje Jina...?


JIBU; Anaitwa Raheli Mke wa Yakobo.
Alikufa akiwa anamzaa Benjamini.

Mwanzo:35:16-19


Swali;
Dini Zote Ni Sawa Zinamwabudu Mungu wa Kweli..?

Hapana Dini zote Si Sawa.

Kutoka:20:3 Kunawanao Amini Miungu

Kutoka:32:8 Kuna Wanaoamini Mungu wa kweli.


Swali: Ni nani aliyekuambia upo uchi..?
Mungu Aliliuliza 

Mwanzo:3:11



MASWALI YA BIBLIA NA MAJIBU.


1:Inakuwaje Tunapokufa?


Jibu la Biblia

Biblia inasema: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” (Mhubiri 9:5; Zaburi 146:4) Kwa hiyo, tunapokufa, hatupo. Wafu hawafikiri, hawatendi, wala kuhisi chochote.


2:SWALI: Huyu Yeshuruni  ni nani kwenye biblia?. Na kwanini alinenepa na kumdharau mwamba wa wokovu wake (Kumb.32:15)?.


JIBU: Yeshuruni ni jina lingine la Taifa la Israeli lililotumika katika biblia ya kiyahudi hususani katika mashahiri,..Neno hili linaonekana mara 4 katika biblia soma (Kumbukumbu 32:15, 33:26, 33:5 na Isaya 44:2).




1:Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?

Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha “Mungu Mtawala”

2:Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?

Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa.

“Nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (1Kor 11:2; 15:3).

“Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Tim 1:14; 2:2).

Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia Biblia, tunaachana na asili ya Kanisa.

“Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (2Thes 2:15; 3:6).

3;Maandiko Matakatifu ndiyo nini?

Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la “Biblia”, yaani “Vitabu”.

Hao “wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA 

Karibu Kipindi cha Maswali Ya Biblia Kinachotusaindia Kujifunza Biblia 
ΔΆaribu Sana Mimi Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Swali:1
   Mbinguni kukoje?Unaweza Kutupa picha Sawasawa na Andiko..?

 Jibu
Mbinguni Ni Makao ya kiroho yana utendaji mwingi sana. Yana mamia ya mamilioni ya viumbe wa roho ‘wanaolitenda neno lake Mungu’​ Soma hivi vitabu
—Zaburi 103:20, 21; Danieli 7:​10.

     "UFAFANUZI ZAIDI MAANDIKO"

 Biblia inafafanua mbinguni kuwa mahali palipo na nuru nyingi sana. (1 Timotheo 6:​15, 16) 

Nabii Ezekieli alipokea maono ya kimbingu yaliyokuwa na “mwangaza” uliong’aa sana, naye Danieli aliona maono ya mbinguni yaliyokuwa na “mto wa moto.” (Ezekieli 1:26-28; Danieli 7:9, 10)

 Mbinguni ni mahali patakatifu, au safi, na maridadi.​—Zaburi 96:6; Isaya 63:15; Ufunuo 4:​2, 3.


2:SWALI 
Je, Yesu aliishi mbinguni kabla ya kuzaliwa duniani?

JIBU LA SWALI 
 Ndiyo. Yesu alikuwa kiumbe wa roho mbinguni kabla ya kuzaliwa akiwa mwanadamu duniani. Yesu mwenyewe alisema hivi: “[Nimeshuka] kutoka mbinguni.”—Yohana 6:38; 8:23.

 Mungu alimuumba Yesu kabla ya kuumba kitu kingine chochote. Biblia inasema hivi kumhusu Yesu:

 “Yeye ndiye . . . mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”—Wakolosai 1:15.

 Yeye ndiye “mwanzo wa uumbaji wa Mungu.”—Ufunuo 3:14.

 Yesu alitimiza unabii kumhusu yule “ambaye asili yake ni ya tangu nyakati za kale, tangu siku za zamani za kale.
”Mika 5:2; Mathayo 2:4-6.




SOMO: HAYA UKIYAONA UJUE HAMUOWANI.

     .... πŸ‘ŠDARASA LA UCHUMBA πŸ‘Š...... :::::::::::::::::::;;;;;;;;;...... :::::::....... :::::.... ::::::::. 
SOMO:UKIYAONA HAYA KWENYE UCHUMBA HAMUOWANI KWA NDOA TENA UJUE HILO.

Kuna Vitu ukiviona kwenye mahusiano vinakupa dalili zote upo tu unapoteza muda ni bora ukavunja mahusiano yasiyoeleweka ukaanzisha yanayoeleweka hata kama unampenda vipi.
Haya yanaenda Kukupa Ufahamu kuwa mtaowana au mnapotezeana muda tu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Mithali;12:1-5

Kumbukumbu la Torati 32:2 
 Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.
🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳
1:MkIONA HAMNA MAWASILIANO AU KUONGELEA MASWALA YA KUISHI PAMOJA
.
Watu wanaotamani kuishi pamoja huwa lazima mtazungumzia maisha yenu familia na mtakapoishi watoto mtakaozaa pia hata kama mtu awe bize kiasi ngani atakutafuta tu hata Sms atakutumia.

2:MKIONA MMEKAA PAMOJA KAMA MKE NA MME HALAFU HAMJULIKANI POPOTE UJUE HAMTAOWANA TENA.

Kiuhalisia mtu huwa anatamani Sana muishi wote mkiwa hamjaanza kukaa nae sababu kila mmoja anakuwa majukumu yale hajayaona Safari ya ndoa hajaanza akishaanza kukaa nawewe Ni ngumu kumwambia akakutolee mahari mfunge ndoa ndiyo maana wengi hubariki wanakuwa wamezaa na wameshaanzeeka miaka 7 au kumi ndio wanabariki. Bint au kijana ukiwa unataka ndoa epuka hii.

3:MKIKAA MIAKA 4,5,6,7,nakuendelea HAMJULIKANI 

Watu wanaotaka Kuanza Familia Wanahami wa hayo maisha kwa hiyo hutamani mambo yaende haraka haraka hawataki kusubirishwa au kukalishwa Ukiona umekalishwa miaka na miaka Hamtaowana ninyi.

4;MKISHAANZA TABIA YA KUZINI AU UKARIBU ULIOPITILIZA AU KUTANGAZA UCHUMBA WENU.

Mahusiano yanaitaji Umakini na Ulizi Wa Mungu ukianza kwa kuzini unafukuza Roho wa Mungu unafungulia roho za shetani zitakazokutumikisha kishetani shetani hata ufahamu wako utakamatwa unaanza kuishi dhambi na kuihararisha mwenyewe Kuzini unaona kawaida matokeo yake ni makubwa Sana.


5:MKIOWANA MAHUSIANO HAMNA MLEZI WA KIROHO .

Ukiwa huna mlezi wa Kiroho maana yake hata fungu la kumi mwizi Pia maana yake huna wa kukushauri na kukuongoza unakuwa unaendesha mahusiano kwa akili zako.

Jitaidi uwe na mlezi wa kiroho na utoe fungu la kumi kwa Baba huyo wa kiroho kwa kufata utaratibu wa Madhabahu yake


Shika haya yakusaindie Nakukaribisha Kwenye Group la Maombi na Mafundisho Uendelee kupata Elimu hii kwenye kipindi cha Darasa la Uchumba Tuma ujumbe WhatsApp uombe kuungwa na ujibu maswali utakayoulizwa Kwa Usahihi +255759861768

SOMO;MADHARA YA KUZALIWA NJE YA NDOA.

     πŸ‘ŠDARASA LA NENO LA MUNGUπŸ‘Š

SOMO;MADHARA MATATU MAKUBWA KWA MTOTO ALIYEZALIWA NJE YA NDOA.


Ninakukaribisha tujifunze madhara ya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa asipokombolewa huwa ni yapi hili ni darasa litatusaindia sisi tuliozaa nje ya ndoa na Tunaofikiria tuzae nje ya ndoa ili ibaki uchanguzi kwako mimi ninakupa ufahamu tu mwenye kufanya maamuzi ni wewe na inawezekana nawewe ni mtoto wa uzinifu uliyepatikana kwa dhambi ya uzinifu utajifunza kitu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro wilaya ya Kilosa Kata Ya Mbigiri Kijiji cha Mateteni. 


MAMBO YAFATAYO NI MADHARA YANAYOMPATA MTOTO ALIYEZALIWA KWENYE UZINIFU. 


1.ATAKUWA NA HATIA YA KUADAMWA Roho Za Matukio Yenye mikosi.

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Zaburi 51:5
[5]Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; 
Mama yangu alinichukua mimba hatiani. 

Kuna mikosi unayoipitia kwa sababu ya tumbo lilokuzaa au upatikanaji wako haukuwa wa Kimungu kwa hiyo ulijisajiri kwenye roho za maovu toka tumboni mwa mama yako na ule uovu unakutesa mpaka sasa.


2.UTAKUWA NA ROHO YA KUZINI NDANI YA DAMU YAKO UTAJITAIDI KUACHA HUWEZI.

SOMA πŸ‘‰Zaburi;38;3 Mithali.6;29
Hii dhambi hukaa kwenye damu na mtu inakuwa kwake kama kawaida lakini inamtenga na Mungu kabisa.

3.UKIJA KUKUA UTAKUWA HUOLEWI AU HUOWI ZAIDI UTAENDESHWA NA Roho ya Kuzalisha/Kuzaa nje ya ndoa.

Soma.Ezekiel.23 hii hadithi ya mabint wa wawili mtu na dada yake walikuwa wakibadilisha wanaume tu toka wakiwa na miaka 17 walianza kuzini mpaka kuwa wakubwa walitembea mpaka na mawazili wabuge nk.

Ila ukija kutazama utaona walizaliwa kwenye uzinifu.


Nataka Nikuambie Unapaswa ujikomboe na umkomboe mtoto uliyemzaa kwenye dhambi ya uzinifu 
.
KARIBU KWENYE  GROUP LA MAOMBI NA MAFUNDISHO MBALIMBALI MFATE WhatsApp PastorRichard+255759861768 Muombe Akuunge.

Jumatatu, 2 Septemba 2024

SOMO;MAMBO MATATU YAJUE NDANI YA NDOA

πŸ‘πŸΏDARASA LA WANANDOA πŸ‘πŸΏ


SOMO; MAMBO MATATU YAFANYE KWENYE NDOA YAKO 

1;HAKIKISHA UNAKUWA MSAFI 

Katika mavazi katika nyumba yako katika chumba chako nakitanda chako katika mwili wako Usafi ni eneo linalomfanya mwanaume akupende hakikisha nguo za Wanao unasafisha na kuiweka vizuro nyumba yako.


2;KUWA MWANAMKE MWENYE KAULI NZURI NA MWENYE KUMUOMBEA MUMEO

Hakikisha mumeo unakuwa makini na msikivu anapoongea Usimkatishe Katikati ya mazungumzo pia hakikisha kama Amezungumza kauli imekukwanza shuka chini baadae Sasa unaweza kumweleza kwa utaratibu alipokosea.

3:UWE NA UPENDO. 
Ipende familia yako mpende mumeo wapende watoto wako ipende nyumba yako hakikisha unakuwa pamoja na mumeo katika magumu ay vipindi vigumu. 


HAYA NI YA MSINGI UYAJUE NDANI YA NDOA.


@Pastor Richard 
2024