Jumamosi, 7 Septemba 2024

SOMO: HAYA UKIYAONA UJUE HAMUOWANI.

     .... 👊DARASA LA UCHUMBA 👊...... :::::::::::::::::::;;;;;;;;;...... :::::::....... :::::.... ::::::::. 
SOMO:UKIYAONA HAYA KWENYE UCHUMBA HAMUOWANI KWA NDOA TENA UJUE HILO.

Kuna Vitu ukiviona kwenye mahusiano vinakupa dalili zote upo tu unapoteza muda ni bora ukavunja mahusiano yasiyoeleweka ukaanzisha yanayoeleweka hata kama unampenda vipi.
Haya yanaenda Kukupa Ufahamu kuwa mtaowana au mnapotezeana muda tu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Mithali;12:1-5

Kumbukumbu la Torati 32:2 
 Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.
🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳
1:MkIONA HAMNA MAWASILIANO AU KUONGELEA MASWALA YA KUISHI PAMOJA
.
Watu wanaotamani kuishi pamoja huwa lazima mtazungumzia maisha yenu familia na mtakapoishi watoto mtakaozaa pia hata kama mtu awe bize kiasi ngani atakutafuta tu hata Sms atakutumia.

2:MKIONA MMEKAA PAMOJA KAMA MKE NA MME HALAFU HAMJULIKANI POPOTE UJUE HAMTAOWANA TENA.

Kiuhalisia mtu huwa anatamani Sana muishi wote mkiwa hamjaanza kukaa nae sababu kila mmoja anakuwa majukumu yale hajayaona Safari ya ndoa hajaanza akishaanza kukaa nawewe Ni ngumu kumwambia akakutolee mahari mfunge ndoa ndiyo maana wengi hubariki wanakuwa wamezaa na wameshaanzeeka miaka 7 au kumi ndio wanabariki. Bint au kijana ukiwa unataka ndoa epuka hii.

3:MKIKAA MIAKA 4,5,6,7,nakuendelea HAMJULIKANI 

Watu wanaotaka Kuanza Familia Wanahami wa hayo maisha kwa hiyo hutamani mambo yaende haraka haraka hawataki kusubirishwa au kukalishwa Ukiona umekalishwa miaka na miaka Hamtaowana ninyi.

4;MKISHAANZA TABIA YA KUZINI AU UKARIBU ULIOPITILIZA AU KUTANGAZA UCHUMBA WENU.

Mahusiano yanaitaji Umakini na Ulizi Wa Mungu ukianza kwa kuzini unafukuza Roho wa Mungu unafungulia roho za shetani zitakazokutumikisha kishetani shetani hata ufahamu wako utakamatwa unaanza kuishi dhambi na kuihararisha mwenyewe Kuzini unaona kawaida matokeo yake ni makubwa Sana.


5:MKIOWANA MAHUSIANO HAMNA MLEZI WA KIROHO .

Ukiwa huna mlezi wa Kiroho maana yake hata fungu la kumi mwizi Pia maana yake huna wa kukushauri na kukuongoza unakuwa unaendesha mahusiano kwa akili zako.

Jitaidi uwe na mlezi wa kiroho na utoe fungu la kumi kwa Baba huyo wa kiroho kwa kufata utaratibu wa Madhabahu yake


Shika haya yakusaindie Nakukaribisha Kwenye Group la Maombi na Mafundisho Uendelee kupata Elimu hii kwenye kipindi cha Darasa la Uchumba Tuma ujumbe WhatsApp uombe kuungwa na ujibu maswali utakayoulizwa Kwa Usahihi +255759861768

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni