Jumamosi, 7 Septemba 2024

Maswali na majibu Jumapili.9/9/2024

   DARASA LA
BIBLIA MASWALI NA MAJIBU  

Karibu katika Kipindi Kipya kitakakuinjia kwenye Group letu la Maombi Kila Jumatatu Asubuhi Lengo Ni Wewe Kuendelea Kuzidi kujifunza Maswali na Majibu mbalimbali 
Hakikisha unaandika maana usije ukaniambia nirushe swali ambalo lilishapita kuanzia Leo Anza Kufatilia.
Naitwa Pastor Richard 

TUMEANZA NA HAYA MASWALI:    

 Swali:1
Nini Kitanizuia nisibatizwe kwa maji mengi..?
Ni kitabu ngani kinasema hivyo na Ni nani aliyesema maneno hayo..?

Jibu;Matendo;8:36

              Swali:2
Biblia haikuandikwa mambo yote ingeandikwa kitabu kisengetosha..?
Kitabu ngani kinasema  maneno haya.
A.Mwanzo
B.Hesabu
C.Luka
D.Yohana 21:25✅
E.Zaburi.

             Swali: 3
Utatu mtakatifu ulifunuliwa au ulitambulishwa lini kwetu mpaka Tukaujua..?

Jibu;Kipindi cha Ubatizo wa Yesu. 
Mathayo;3;16-17


       Swali:4
Swali la Kwanza Toka Dunia iumbwe  liliulizwa na nani..? Aliliuliza Akiwa  Wapi..?

Mwanzo:3:1



MASWALI NA MAJIBU JUMAPILI TAR.15/9/2024

🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🎈
SWALI;1

1:Yesu alipoletwa Hekaluni akiwa mtoto mchanga, ni nani aliyemtambua kuwa ndiye Masihi?

Jibu: Simeoni ( Luka 2:22-38 ).


SWALI:2

2. Ni mgombea gani ambaye hakuchaguliwa kwa wadhifa wa mtume baada ya Yuda Iskariote kujiua, kulingana na Matendo ya Mitume?

Jibu: Yusufu Barsaba (Matendo 1:24–25).


SWALI:3

3. Ni vikapu vingapi vilivyobaki baada ya Yesu kuwalisha wale 5,000?

Jibu: Vikapu 12 (Marko 8:19).


SWALI:4

4. Katika mfano unaopatikana katika Injili tatu kati ya nne, Yesu alilinganisha mbegu ya haradali na nini?

Jibu:  Ufalme wa Mungu ( Mt. 21:43 ).


SWALI:5

5: Musa alikuwa na umri gani alipokufa, kulingana na kitabu cha Kumbukumbu la Torati?

Jibu: Miaka 120 (Kumbukumbu la Torati 34:5-7).


SWALI:6

6: Ni kijiji gani kilikuwa mahali pa kupaa kwa Yesu, kulingana na Luka?

Jibu: Bethania ( Marko 16:19).


SWALI:7

7. Ni nani anayefasiri maono ya Danieli ya kondoo mume na beberu katika Kitabu cha Danieli?

Jibu: Malaika Mkuu Gabrieli ( Danieli 8:5-7 ).



TAR.22/9/2024 JUMAPILI 


SWALI:88:Ni yupi kati ya mke wa Mfalme Ahabu, aliyetupwa kutoka dirishani na kukanyagwa kwa miguu?

Jibu: Malkia Yezebeli (1 Wafalme: 31).



 

 Nifanye nini ili niokolewe?

  •  Unapaswa kuamini kwamba Yesu alidhabihu uhai wake kwa ajili ya dhambi zetu. (Matendo 16:30, 31; 1 Yohana 2:2) Hilo linamaanisha kuamini kwamba Yesu alikuwa mtu halisi na kwamba mambo yote ambayo simulizi la Biblia linasema kumhusu ni sahihi.

  •  Jifunze kile ambacho Biblia inafundisha hasa. (2 Timotheo 3:15) Biblia inasema kwamba mtume Paulo na Sila walimwambia hivi mlinzi wa jela: “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokolewa, wewe na watu wa nyumba yako.” Kisha, baada ya hapo, walianza kumfundisha mlinzi huyo wa jela “neno la Yehova.” a (Matendo 16:31, 32) Hilo linaonyesha kwamba mlinzi huyo wa jela hangeweza kumwamini Yesu bila kuwa na ujuzi wa msingi wa Neno la Mungu. Alihitaji kuwa na ujuzi sahihi wa Maandiko.—1 Timotheo 2:3, 4.

  •  Tubu. (Matendo 3:19) Pia, lazima utubu, au uhuzunishwe sana, kuhusu mwenendo na mtazamo mbaya uliokuwa nao. Wengine wataona toba yako kadiri unavyoacha mazoea yanayomchukiza Mungu na unapofanya “matendo yanayoonyesha toba.”—Matendo 26:20.

  •  Ubatizo. (Mathayo 28:19) Yesu alisema kwamba wale ambao watakuwa wanafunzi wake wanapaswa kubatizwa. Mlinzi wa jela aliyetajwa hapo awali alibatizwa. (Matendo 16:33) Vivyo hivyo, baada ya mtume Petro kufundisha umati mkubwa ukweli kumhusu Yesu, “wale waliokubali neno lake kwa furaha wakabatizwa.”—Matendo 2:40, 41.

  •  Tii maagizo ya Yesu. (Waebrania 5:9) Wale ambao ‘wanashika mambo yote’ ambayo Yesu aliamuru wanaonyesha kupitia maisha yao kwamba wao ni wafuasi wake. (Mathayo 28:20) Wanakuwa “watendaji wa neno, na si wasikiaji tu.”—Yakobo 1:22.

  •  Vumilia mpaka mwisho. (Marko 13:13) Wanafunzi wa Yesu ‘wanahitaji uvumilivu’ ili         


3:Mtu Akianguka kwenye dhambi na alikuwa Ameokoka shetani humpiga mara mbili yake
Kitabu ngani kinasema hivi.

Jibu; Waebrania;6;4-6




4:Biblia Ni nini?

Jibu la Biblia

 Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vitakatifu. Iliandikwa katika kipindi cha miaka 1,600 hivi. Biblia ina ujumbe kutoka kwa Mungu—“neno la Mungu.”—1 Wathesalonike 2:13.

Tar.7/10/2024

5:TUNAJIFUNZA NINI KWA ABIGAIL
Baadhi ya wanawake wanaotajwa kwenye Biblia

Wanawake Katika Biblia—Tunaweza Kujifunza Nini Kutoka Kwao?


Jibu la Biblia

 Katika Biblia, tunasoma kuhusu wanawake wengi ambao maisha yao yanatufundisha masomo yenye thamani. (Waroma 15:4; 2 Timotheo 3:16, 17) Makala hii inazungumzia kwa ufupi tu baadhi ya wanawake wanaotajwa katika Biblia. Wengi wao ni mifano mizuri ya kuiga. Wengine ni mifano ya kuonya.—1 Wakorintho 10:11; Waebrania 6:12.



Abigaili

  Abigaili

 Abigaili alikuwa nani? Alikuwa mke wa mwanamume mkatili aliyeitwa Nabali. Hata hivyo, Abigaili alikuwa mwenye busara na mnyenyekevu, na pia alikuwa mrembo kimwili na kiroho.—1 Samweli 25:3.

 Alifanya nini? Abigaili alitenda kwa hekima na busara ili kuzuia msiba. Yeye na Nabali waliishi katika eneo ambalo Daudi, mfalme mtarajiwa wa Israeli, alikuwa akijificha. Daudi na wanaume wake walipokuwa huko, walilinda makundi ya kondoo ya Nabali yasiibiwe. Lakini Daudi alipowatuma wajumbe kumwomba Nabali chakula, Nabali aliwatukana na kukataa. Daudi alikasirika sana. Kwa hiyo, yeye na wanaume wake wakapanga kwenda kumuua Nabali na wanaume wote wa nyumba yake.—1 Samweli 25:10-12, 22.

 Abigaili alitenda upesi aliposikia kile ambacho mume wake alikuwa amefanya. Aliwapa watumishi wake chakula wampelekee Daudi na wanaume wake, naye pia akawafuata ili kumwomba Daudi awaonyeshe rehema. (1 Samweli 25:14-19, 24-31) Daudi alipoona zawadi yake, unyenyekevu wake, na aliposikia ushauri wake wenye hekima, alitambua kwamba Mungu alimtumia ili kumzuia asimuue Nabali na wanaume wake. (1 Samweli 25:32, 33) Muda mfupi baada ya hapo, Nabali alikufa, naye Abigaili akawa mke wa Daudi.—1 Samweli 25:37-41.

 Tunajifunza nini kutoka kwa Abigaili? Ingawa alikuwa mrembo na tajiri, Abigaili alikuwa na maoni yenye usawaziko kujihusu. Ili kudumisha amani, alikuwa tayari kuomba msamaha kwa jambo ambalo halikuwa kosa lake. Alishughulikia hali yenye kutisha kwa utulivu, busara, ujasiri, na alitumia nguvu zake za kufikiri.

  •  Ili kupata habari zaidi kumhusu Abigaili, ona makala yenye kichwa, “Alitenda kwa Busara.”

Debora

  

Jumapili Tar.13-10-2024

MASWALI YA BIBLIA

SWALI;

1; Ni Mwanamke Ngani Wa Kwanza Kujifungua Akafa Akijifungua Mtoto Kwenye Biblia Mtaje Jina...?


JIBU; Anaitwa Raheli Mke wa Yakobo.
Alikufa akiwa anamzaa Benjamini.

Mwanzo:35:16-19


Swali;
Dini Zote Ni Sawa Zinamwabudu Mungu wa Kweli..?

Hapana Dini zote Si Sawa.

Kutoka:20:3 Kunawanao Amini Miungu

Kutoka:32:8 Kuna Wanaoamini Mungu wa kweli.


Swali: Ni nani aliyekuambia upo uchi..?
Mungu Aliliuliza 

Mwanzo:3:11



MASWALI YA BIBLIA NA MAJIBU.


1:Inakuwaje Tunapokufa?


Jibu la Biblia

Biblia inasema: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe.” (Mhubiri 9:5; Zaburi 146:4) Kwa hiyo, tunapokufa, hatupo. Wafu hawafikiri, hawatendi, wala kuhisi chochote.


2:SWALI: Huyu Yeshuruni  ni nani kwenye biblia?. Na kwanini alinenepa na kumdharau mwamba wa wokovu wake (Kumb.32:15)?.


JIBU: Yeshuruni ni jina lingine la Taifa la Israeli lililotumika katika biblia ya kiyahudi hususani katika mashahiri,..Neno hili linaonekana mara 4 katika biblia soma (Kumbukumbu 32:15, 33:26, 33:5 na Isaya 44:2).




1:Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?

Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha “Mungu Mtawala”

2:Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?

Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa.

“Nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (1Kor 11:2; 15:3).

“Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (2Tim 1:14; 2:2).

Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia Biblia, tunaachana na asili ya Kanisa.

“Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (2Thes 2:15; 3:6).

3;Maandiko Matakatifu ndiyo nini?

Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la “Biblia”, yaani “Vitabu”.

Hao “wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA 

Karibu Kipindi cha Maswali Ya Biblia Kinachotusaindia Kujifunza Biblia 
Ķaribu Sana Mimi Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Swali:1
   Mbinguni kukoje?Unaweza Kutupa picha Sawasawa na Andiko..?

 Jibu
Mbinguni Ni Makao ya kiroho yana utendaji mwingi sana. Yana mamia ya mamilioni ya viumbe wa roho ‘wanaolitenda neno lake Mungu’​ Soma hivi vitabu
—Zaburi 103:20, 21; Danieli 7:​10.

     "UFAFANUZI ZAIDI MAANDIKO"

 Biblia inafafanua mbinguni kuwa mahali palipo na nuru nyingi sana. (1 Timotheo 6:​15, 16) 

Nabii Ezekieli alipokea maono ya kimbingu yaliyokuwa na “mwangaza” uliong’aa sana, naye Danieli aliona maono ya mbinguni yaliyokuwa na “mto wa moto.” (Ezekieli 1:26-28; Danieli 7:9, 10)

 Mbinguni ni mahali patakatifu, au safi, na maridadi.​—Zaburi 96:6; Isaya 63:15; Ufunuo 4:​2, 3.


2:SWALI 
Je, Yesu aliishi mbinguni kabla ya kuzaliwa duniani?

JIBU LA SWALI 
 Ndiyo. Yesu alikuwa kiumbe wa roho mbinguni kabla ya kuzaliwa akiwa mwanadamu duniani. Yesu mwenyewe alisema hivi: “[Nimeshuka] kutoka mbinguni.”—Yohana 6:38; 8:23.

 Mungu alimuumba Yesu kabla ya kuumba kitu kingine chochote. Biblia inasema hivi kumhusu Yesu:

 “Yeye ndiye . . . mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”—Wakolosai 1:15.

 Yeye ndiye “mwanzo wa uumbaji wa Mungu.”—Ufunuo 3:14.

 Yesu alitimiza unabii kumhusu yule “ambaye asili yake ni ya tangu nyakati za kale, tangu siku za zamani za kale.
”Mika 5:2; Mathayo 2:4-6.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni