.
AGIZO LA KI MUNGU TUTAANZISHA MADHABAHU YA NYUMBANI KUANZIA LEO FATA MAELEKEZO KATIKA SOMO HILI
1. UTANGULIZI
Ibada ya nyumbani si mkutano wa kidini tu, bali ni kitendo cha kuweka wakfu nyumba na maisha ya kila siku chini ya mamlaka ya Mungu. Ni mahali ambapo familia inakutana na Mungu wao nje ya mazingira ya kanisani.. Ni Muhimu Nyumbani Tuwe na Ibada Familia Tuwe Tunakusanyika kabla Ya Kulala Tusali Pamoja Tutege Muda maalumu kuimarisha Madhabahu ya Nyumbani Tutakuwa Tunatoa na Sadaka Na Kila Jumapili Jioni KIONGOZI Atanipigia Naiombea Madhabahu Hiyo ya Nyumbani.
NENO LINADHIBITISHA
Zaburi 127:1 — "Bwana asipoijenga nyumba, waijengao wafanya kazi bure."
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
ZINGATIA HAYA;
1:Tutatenga Muda Wa Ibada Maalumu Tutumie Muda mfupi Sana Dakika 15 au 10
2;Kiongozi Wa Maombi Ni Wewe Mwanangu uliye Kwenye Group Unapoishi Anzisha IBADA ya Familia.
3:Kila Jumapili Kiongozi Atanipigia Anaweka Raoud Spika Naiombea Madhabahu ya Familia na Wana familia Wote Kwa Muda Wenu Huko Wa Maombi.
.
4:Ibada Tutakuwa Tunatoa Sadaka Tunazikusanya Ili Watoto wazoe kutoa na Jumapili Ninapomaliza Kuwaombea Tutatoa Nitaombea na Mahitaji Yenu ya Ki familia.
5;Kukiwa na SHIDA Kiongozi utanipigia kwa ushauri na Maelekezo ya KIROHO Usiwe Mbali na Askofu Richard Kila hatua ili kuimarisha Familia Zetu Pigs+255759861768 au +255710889892 Kiongozi Tu utanipigia kuwasilisha shida za familia mtakaomba.
2. UMUHIMU WA IBADA YA NYUMBANI KATIKA FAMILIA ZETU
➖Urithi wa Kiroho:✍🏾 Ni darasa la kwanza kwa watoto na vijana kujifunza kumcha Mungu (Kumbukumbu la Torati 6:6-7).
➖Ulinzi wa Kiroho:✍🏾 Inatengeneza mazingira ya uwepo wa Mungu yanayozuia roho za uharibifu kuingia kwenye familia.
➖Umoja wa Familia✍🏾: Inasaidia kuondoa migogoro na kuleta upendo kwani familia inayoomba pamoja, hukaa pamoja.
➖Kukua kwa Kanisa: ✍🏾Kanisa imara linajengwa na familia imara. Nyumba ikiwa na moto wa maombi, kanisa litawaka moto.pia tutaweka ukuta Wa moto hatutasumbuliwa.
3. FAIDA ZA IBADA YA MAJUMBANI
➖Amani na Furaha:✍🏾 Uwepo wa Mungu unapoingia ndani ya nyumba, huzuni na hofu vinaondoka (Zaburi 16:11).
➖Maelekezo ya Kiungu: ✍🏾Mungu anapata nafasi ya kusema na familia kuhusu maamuzi yao ya kila siku (Biashara, Masomo, Afya).
➖Kujenga Imani: ✍🏾Kupitia kusoma neno, waumini wanakuwa na ufahamu wa kina wa maandiko.
➖Uponyaji na Baraka:✍🏾 Ni mahali ambapo wagonjwa ndani ya nyumba wanaweza kuombewa na baraka za kiuchumi kutamkwa.
4. NAMNA YA KUIFANYA IBADA YA MAJUMBANI (MIONGOZO RAHISI KWENDA NAYO)
Ili kuifanya ibada hii iwe endelevu na isichoshe, waumini wanashauriwa kufuata hatua hizi:
➖Chagua Muda Maalum: ✍🏾Panga muda ambao kila mtu yupo nyumbani (asubuhi na mapema au kabla ya kulala).
➖Usiwe na Muda Mrefu Sana: ✍🏾Dakika 15 hadi 30 zinatosha ili kuwafanya watoto na watu wenye ratiba ngumu wasichoke.
➖Shirikisha Kila Mtu:✍🏾 Badilishana majukumu; leo baba aongoze, kesho mama, keshokutwa kijana au mtoto. Hii inajenga ujasiri Katika Familia Yako
UTARATIBU WA IBADA YA MAJUMBANI TUTAKAVYOOMBA
Tutaenda Na Utaratibu huu Wa kuendesha ibada zetu. baada ya Kukusanyana
➖Sifa na Kuabudu:✍🏾 Wimbo mmoja au miwili ya kumtukuza Mungu.
➖Neno la Mungu: ✍🏾Soma kifungu kimoja cha Biblia na kutoa maelezo mafupi (Sio mahubiri marefu).
➖Shuhuda/Mahitaji:✍🏾 Ulizana kama kuna mwenye hitaji au jambo la kumshukuru Mungu muombeane Mahitaji kila Mtu aandike Kwenye karatasi.
Jumapili ninapowaombea mnayashika nayaombea.
➖Maombi: ✍🏾Ombea familia, Kanisa, Taifa, na kazi za mikono yenu na Mchungaji
➖Baraka: ✍🏾Kiongozi anatamka baraka juu ya nyumba.
5. MISTARI YA BIBLIA YA KUTUMIA KATIKA IBADA YA MAJUMBANI
➖Joshua 24:15 — "Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Bwana."
➖Mathayo 18:20 — "Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao."
.
➖Mithali 22:6 — "Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee."
➖Matendo 2:46-47 — "Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba..."
➖Wakolosai 3:16 — "Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni..."
HITIMISHO
Ibada ya nyumbani ndiyo "Betheli" (Nyumba ya Mungu) ndogo. Ukianza leo, utaona mabadiliko makubwa katika tabia za watoto wako na ustawi wa nyumba yako. Mungu Akubariki Mtoto Wa Mungu Kwa Kulichukua Kwa Uzito Kuanza rasimi ibada ya familia leo.
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania
Madhabahu Ya Moto Wa Yesu
Nipo Morogoro Vera Dakawa
Ndiye Kiongozi na Muasisi Wa Magroup yote matatu Maombi na Mafundisho Madhabahu ya Kwenye Group imekuwa Baraka Kwa Wengi Sana.
WhatsApp Yangu +255710889892
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni