Jumatano, 29 Aprili 2026

SOMO;SIRI NA NGUVU YA KUTOA SADAKA

 SOMO: SIRI NA NGUVU YA UTA KIROHO KATIKA SADAKA

UTANGULIZI

​Kutoa si sheria ya kidini, bali ni kanuni ya ufalme wa Mungu na kielelezo cha upendo wa mwamini kwa Muumba wake. Unapookoka, unahamishwa kutoka kwenye mfumo wa ulimwengu (wa kujilimbikizia) kwenda kwenye mfumo wa Mungu (wa kutoa ili ubarikiwe).


1. AINA ZA SADAKA ANAZOPASWA KUTOA MWAMINI ALIYEOKOKA NA MKRISTO 

Siyo Kila Sadaka Uliyeokoka Unatakiwa Utoe Hapana hizi ni Sadaka Za Lazima Utoe Kukamilisha Muuganiko wako Na Mungu Katika Ushirika wako wa Nafsi ya Uungu Mungu Baba Mungu Mwana Mungu Roho. Cha Kutambua Mpendwa Kutoa Kwa Mungu Wako Ni Sheria Unatoa Kumuonesha Unavyompenda Kiukweli Mungu Ukimpenda Utatamani Injili yake iende mbele Support Vyombo Viwanja Viti Makazi Ya Wachungaji Nk. 

  • 1;​Zaka (Fungu la Kumi): Hii ni asilimia kumi (10%) ya mapato yako yote (mshahara, faida ya biashara, au zawadi). Kimaandiko, hii si hiari bali ni stahiki ya Mungu.

    • Andiko: Malaki 3:10 – "Leteni zaka kamili ghalani... mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi."

  • 2:;​Sadaka ya Shukrani: Hutolewa pale unapoguswa na wema wa Mungu baada ya kuvushwa kwenye jaribu, kuponywa, au kupata mafanikio fulani.

    • Andiko: Zaburi 116:17 – "Nitakutolea dhabihu ya kushukuru, na kulitangaza jina la Bwana."

  • ​3:Sadaka ya Hiari ya Kila Siku: Hii ndiyo sadaka tunayotoa kila tunapokwenda mbele za Mungu kwenye ibada kama ishara ya heshima.

    • Andiko: Kumbukumbu la Torati 16:16 – "Wala wasitokee mbele za Bwana mikono mitupu."

  • 4:​Sadaka kwa Wahitaji (Kutoa Sadaka): Huu ni msaada kwa mayatima, wajane, na maskini.nk  Hii inamgusa Mungu moyo kwa namna ya pekee sana.

Hii Ukitoa Siyo ndio umetoa zaka Fungu la Kumi ni Kosa kubwa kulipeleka Kwa Wahitaji Sadaka Ya Wahitaji ibaki kuwa ya wahitaji
    • Andiko: Mithali 19:17 – "Amhurumiye maskini amkopesha Bwana; naye atamlipa kwa tendo lake jema.".

  • ​5:Malimbuko: Hii ni sadaka ya kwanza kabisa ya mazao yako au mshahara wa kwanza wa kazi mpya au ongezeko la mshahara au Mauzo ya Kwanza Kabisa

    • Andiko: Mithali 3:9 – "Mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote."

2. UMUHIMU NA FAIDA ZA KUTOA SADAKA



  1. Inamfungia Mlango Mharibifu: Zaka na sadaka zinafanya kazi ya ulinzi juu ya kazi za mikono yako ili usipate hasara zisizoeleweka.

  1. Inafungua Madirisha ya Mbinguni: Kutoa kunaachia baraka ambazo akili ya kibinadamu haiwezi kuzitafuta, ikiwemo kibali na fursa mpya.

  1. Inajenga Uhusiano wa Karibu na Mungu: Unapotoa, unaweka moyo wako kwa Mungu. Huwezi kumtolea Mungu na bado ukabaki kuwa mbali naye kiroho.

  1. Inaleta Furaha ya Ndani: Kuna baraka kubwa na amani inayokuja kwa kutoa kuliko kupokea.

3. MIFANO YA WATU KWENYE BIBLIA WALIOTOA


  • Ibrahimu: Alikuwa wa kwanza kutoa zaka kwa Melkizedeki. Matokeo yake, Mungu alimbariki na kumfanya kuwa baba wa mataifa mengi (Mwanzo 14:20).

  • Mjane wa Sarepta: Alitoa chakula chake cha mwisho kwa Nabii Eliya wakati wa njaa. Matokeo yake, unga na mafuta yake hayakuisha hadi njaa ilipoisha (1 Wafalme 17:15-16).

  • Kanisa la Kwanza: Waumini walikuwa wakitoa mali zao na kuwapa mitume ili kusaidia kazi ya Mungu. Matokeo yake, hapakuwa na mtu mhitaji miongoni mwao (Matendo 4:34-35).

  • Kornelio: Alikuwa mtu wa maombi na kutoa sadaka nyingi kwa watu. Sadaka zake zilifika mbele za Mungu kama kumbukumbu, na kusababisha wokovu uingie nyumbani kwake (Matendo 10:2-4).

        ​HITIMISHO


​Ndugu mpendwa, elewa kuwa Mungu hahitaji fedha zako kwa sababu Yeye ni masikini—Yeye ndiye mmiliki wa dhahabu na fedha zote. Anachotafuta ni Utii na Moyo wako. Unapotoa, usitoe kwa sababu ya sheria, bali toa kwa sababu unampenda Mungu anayekupa pumzi na nguvu ya kutafuta mali. Kumbuka, mkono wa mtoaji upo juu ya mkono wa mpokeaji siku zote. Anza kutoa leo kwa imani, na utaona milango ya mbinguni ikifunguka kwa ajili yako!


        WITO

Niulize Swali Juu Ya Utoaji Inbox Nikupe Elimu nakukusaidia Vizuri Eneo la Utoaji

WhatsApp Yangu Pastor Richard Wa Morogoro +255710889892

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni