SOMO MAJINA YA MALAIKA NA MAKUNDI NA KAZI ZAO
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Nipo Morogoro Veta Dakawa
Karibu Elimu hii nzuri Ya Kuwajua MAKUNDI ya Malaika Mbiguni Kuna Malaika Wengi Sana Ambao Kwenye Biblia Hawakujitambulisha au Kutajwa Ambao Wapo Wanatenda Kazi Na Mungu.
Ni Jukumu la Kila Mkristo Kuwajua Malaika hata namna ya kazi zao nakuwatumia
Leo nakutajia MAKUNDI Yao na kazi zao kule mbiguni
1;Malaika Mikaeli (Michael)
Jina lake lina maana ya "Nani aliye kama Mungu?". Yeye anajulikana kama mkuu wa majeshi ya mbinguni na mlinzi wa watu wa Mungu.
- Kazi yake: Kupigana vita vya kiroho dhidi ya shetani na kulinda taifa la Mungu.
- Mistari ya Biblia:
- Danieli 10:13: "Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia..."
- Yuda 1:9: "Lakini Mikaeli, mkuu wa malaika, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa..."
- Ufunuo 12:7: "Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka..."
2. Malaika Gabrieli (Gabriel)
Jina lake lina maana ya "Mungu ni nguvu yangu" au "Shujaa wa Mungu". Yeye ni mjumbe mkuu wa habari njema na mafunuo.
- Kazi yake: Kufikisha jumbe muhimu za Mungu kwa wanadamu na kufafanua maono.
- Mistari ya Biblia:
- Danieli 8:16: "Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfamulishe mtu huyu maono haya."
- Luka 1:19: "Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nalitumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema."
- Luka 1:26-27: "Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa bikira mmoja..."
Makundi ya Malaika na Kazi Zao (Kulingana na Maandiko)
Ingawa Biblia haitaji majina mengine mengi, inataja makundi yenye kazi maalum:.
A. Makerubi (Cherubim)
- Kazi: Walinzi wa utakatifu wa Mungu na kiti chake cha enzi.
- Mstari: Mwanzo 3:24 – "Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni..."
B. Maserafi (Seraphim)
- Kazi: Kumwabudu na kumtukuza Mungu daima mbele ya kiti chake cha enzi.
- Mstari: Isaya 6:2-3 – "Juu yake walisimama maserafi... wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi..."
C. Malaika Walinzi/Watumishi
- Kazi: Kuwalinda waaminifu na kuwatumikia wale watakaourithi wokovu.
- Mistari: *
- Zaburi 91:11: "Kwa kuwa atakuagizia malaika zake, wakulinde katika njia zako zote."
- Waebrania 1:14: "Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?".
Tuma Elimu hii kwa watu Wengi na ma group Waunge Wanaopenda kujifunza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni