SOMO: HATARI YA KUKATALIWA NA BWANA
Lengo: Kuelewa sababu zinazomfanya Mungu amuondoe mtu kwenye nafasi yake na jinsi ya kujirekebisha.
REJEA KUU ZA BIBLIA:SOMAππΎππΎππΎ
- 1 Samweli 15:23, 26: "Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme."
- Hosea 4:6: "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe..."
UTANGULIZI: Siri ya Sauli
Watu wengi leo wanaishi kama Mfalme Sauli; wanaendelea na huduma, vyeo, na kazi zao huku rohoni wakiwa tayari wameshapoteza kibali cha Mungu (Kukataliwa). Sauli alijiona ana elimu, cheo, na nguvu, akasahau kuwa chanzo cha vyote ni utii kwa Mungu kupitia nabii wake, Samweli.
SABABU ZINAZOFANYA MUNGU AKUKATAE
- Kukataa Maelekezo ya Baba wa Kiroho
- Mungu huweka mamlaka duniani ili kutuongoza. Sauli aliamua kufanya "ibada" yake mwenyewe badala ya kusubiri maelekezo ya Samweli. “Kutii ni bora kuliko dhabihu.” (1 Samweli 15:22)
- Kupuuza Maarifa na Neno la Mungu
- Watu wengi wanapenda maombi na miujiza, lakini wanachukia mafundisho. Ukikataa kujifunza Neno, unakataa maarifa ya Mungu, na matokeo yake ni kukataliwa.
“Kutii ni bora kuliko dhabihu.” (1 Samweli 15:22)
- Kiburi cha Cheo na Mafanikio
- Unapofika mahali unajiona huwezi kuambiwa kitu kisa una pesa, elimu, au cheo, unajitengenezea mazingira ya kuanguka. Mungu huwapinga wenye kibali bali huwapa neema wanyenyekevu.
- Kuwa Mtoto Mtiifu: Utii ni kipimo cha upendo wako kwa Mungu.
TUFANYE NINI ILI KUREJESHA KIBALI?
Ili usikataliwe na Bwana, unapaswa kuzingatia misingi hii:
- Heshimu Mamlaka ya Kiroho: Fuata maelekezo ya Baba yako wa kiroho aliyewekwa na Mungu juu yako; yeye ni kinywa cha Bwana kwako.
- Tafuta Kujitambua: Jua kusudi la kuumbwa kwako. Usiishi tu, bali ishi kwa sababu (Purpose).
- Penda Neno: Usiwe mkristo wa 'kudekezwa' na maombi tu, simama kwenye zamu yako kwa kujifunza Biblia.
TAHADHARI YA MWISHO
Mungu ana watu wengi na Huwa Hadekewi. Ukikataa kuitumia nafasi yako kwa utii, Mungu atamuinua mwingine kama alivyomuinua Daudi baada ya Sauli kukataliwa.
"HITIMISHO"
Simama kwenye zamu yako kwa unyenyekevu, maana kiongozi wako wa kiroho ndiye aliyebeba maono na baraka ambazo Mungu amezikusudia kwako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni