Jumamosi, 23 Desemba 2023

SOMO: KUSUDI LA KUZALIWA YESU

KUSUDI LA KUZALIWA KWA YESUKUSUDI LA KUZALIWA KWA  YESU

 



(Mathayo 1:18-21)

Mambo utakayojifunza

1.Kusudi la kuzaliwa kwa Yesu

2.Namna tunavyopswa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu

UTANGULIZI

Watu wengi wakristo na wasio wakristo wamekuwa wakifanya sherehe katika sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu maarufu kama krismasi (Christmass).

Watu wengi wakristo na wasio wakristo wamekuwa wakisherehekea vibaya sikukuu hii kutokana na kutofahamu hasa lengo la kuzaliwa kwa Yesu au lengo la Yesu kuja hapa ulimwenguni.

Watu wengi wamekuwa wakiweka nguvu nyingi katika manunuzi ya vitu mbalimbali kama mavazi na chakula  pamoja na kwenda kutalii sehemu mbalimbali, sio vibaya kufanya hayo yote nyakati za sherehe ila kabla ya kuwekeza nguvu nyingi katika mambo hayo ni vema uwe na ufahamu kuhusu sherehe hii kiini chake ni nini, ukifahamu lengo la Yesu kuja hapa duniani naamini hautasherehekea kimakosa.

N.B Tunaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25 mwezi wa 12 kila mwaka haimaanishi kuwa Yesu alizaliwa tarehe hiyo ila tunaitumia siku hiyo kukumbuka au kama kumbukumbu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu kwa kumtoa mwanawe wa pekee kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu.

KUSUDI LA KUZALIWA KWA YESU

(Mathayo 1:21)

“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.”

Kutokana na andiko hilo tunapata kufahamu kuwa kusudi la Yesu kuja hapa ulimwenguni ni ili “AWAOKOE WATU WAKE NA DHAMBI ZAO”

 

(Luka 10:19)

“Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

Kutokana na fungu hilo tunapata kufahamu kuwa Yesu “ALIKUJA KUTAFUTA NA KUOKOA KILE KILICHOPOTEA”

 

Kwa kuwa Yesu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea ndio maana malaika wa Mungu wanasherehekea pale mwenye dhambi mmoja anapotubu au anapomwamini Yesu.

 

“Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.”

(Luka 15:7)

 

NAMNA TUNAVYPASWA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KUZALIWA KWA YESU (CHRISTMASS)

1.     Tunapaswa kuwaambia wengine habari za Yesu ili waokoke (tunapaswa kuhubiri injili)

(Mathayo 28:19-20)

“19. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20. na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

 

Kwa kuwa kusudi la kuzaliwa kwa Yesu ni kuwaokoa wanadamu, tunapaswa kusherehekea sikukuu hii kwa kuwashuhudia wengine au kuwaambia wengine habari za Yesu au kuhubiri injili.

 

2.     Tunapaswa kutoa fedha zetu au vifaa mbalimbali vitakavyosababisha injili iwafikie wale ambao hawajamwamini Yesu.

(Warumi 10:14-15)

“14. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? 15. Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”

 

Sisi ambao tayari tumemwamini Yesu tunapaswa kutoa fedha zetu ili injili ihubiriwe, tunapaswa kununua vifaa vya kuhubiria injili na kuwapa wahubiri au kuvitoa makanisani ili injili izidi kuhubiriwa pia tunapaswa kuwasafirisha wahubiri wa injili ili waende kwenye umisheni.

 

Biblia imeweka wazi kuwa hakuna askari aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe, askari anahitaji kupelekwa.

“Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe?” (1 Wakoritho 9:7a)

 

3.     Tunapaswa kumpa Mungu vilivyo bora .

(Mathayo 2:11)

Mamajusi walipokuja kumtazama Yesu walimtolea Yesu tunu, uvumba, dhahabu na manemane.

Tunaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu tunapswa kukumbuka kuwa Yesu alitolewa na Mungu kama zawadi ya Mungu kwa ulimwengu ili wanadamu waokolewe, kama Mungu alitoa kilicho bora 


Biblia Inasema Nini Kuhusu Krismasi?

Jibu la Biblia

 Biblia haitaji tarehe ambayo Yesu alizaliwa, wala haisemi kwamba tusherehekee siku yake ya kuzaliwa. Kama vile kitabu McClintock and Strong’s Cyclopedia kinavyosema: “Mwadhimisho wa Krismasi haukuagizwa na Mungu, wala hautokani na AG [Agano Jipya].”

 Kinyume cha hilo, historia ya Krismasi inafunua kwamba inatokana na sherehe za kipagani. Biblia inaonyesha kwamba tunamchukiza Mungu ikiwa tunamwabudu katika njia ambayo yeye hakubali.—Kutoka 32:5-7.

Historia ya desturi za Krismasi

  1.  Kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu: “Wakristo wa karne ya kwanza hawakusherehekea siku ya kuzaliwa kwa [Yesu] kwa sababu waliiona sherehe ya kuzaliwa kwa mtu yeyote kuwa desturi ya wapagani.”—The World Book Encyclopedia.

  2.  Desemba 25: Hakuna uthibitisho wowote kwamba Yesu alizaliwa tarehe hiyo. Huenda viongozi wa Kanisa walichagua tarehe hiyo ili ipatane na sherehe za kipagani zilizofanywa wakati wa au karibu na majira ya baridi kali.

  3.  Kupeana zawadi, sherehe, karamu: Kitabu The Encyclopedia Americana kinasema: “Desturi nyingi za kujifurahisha zinazofuatwa wakati wa Krismasi zinatokana na Saturnalia, sherehe ya Waroma iliyofanywa katikati ya mwezi wa Desemba. Kwa mfano, karamu zenye madoido mengi, kupeana zawadi, na kuwasha mishumaa zilitokana na sherehe hii.” Kitabu Encyclopædia Britannica kinasema kwamba “hakuna kazi wala biashara iliyofanywa” wakati wa Saturnalia.

  4.  Taa za Krismasi: Kitabu The Encyclopedia of Religion kinasema kwamba wazungu walirembesha nyumba zao kwa “taa na mimea ya kijani-kibichi ya kila aina” ili kusherehekea majira ya baridi kali na ili kuwazuia roho waovu.

  5.  Mlimbo, mholi: Kwa kawaida mimea hiyo hutumiwa kama mapambo wakati wa Krismasi. “Wadruidi (makasisi Waselti) walisema kwamba mlimbo ulikuwa na nguvu za kimuujiza. Mholi, mmea ambao haunyauki, uliabudiwa kama ahadi ya kurudi kwa jua.”—The Encyclopedia Americana.

  6.  Mti wa Krismasi: “Kuabudu miti lilikuwa jambo la kawaida kati ya wapagani wa Ulaya na waliendelea na zoea hilo baada ya kuwa Wakristo.” Kati ya mazoea yaliyobaki ya ibada hiyo ya miti ni desturi ya “kuweka mti wa Krismasi kwenye mwingilio au ndani ya nyumba wakati wa sikukuu zinazofanywa katikati ya majira ya baridi kali.”​—Encyclopædia Britannica.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni