SOMO;MAOMBI YA USIKU
Kila Siku uendapo kulala Omba usiwe unalala bila maombi
haya maombi nimeelekeza kukusaindia lakini huzuiliwi ukimaliza haya usiku unaendelea na maombi yako mengine Roho Mtakatifu anavyokuwa anakuongoza.
Karibu
Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro wilaya ya Kilosa Kata Ya Mbigiri Kijiji cha Mateteni
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania (H.S.C.T)
Mstari wa kusimama nao.
Mithali:3:24-26
MiSTARI YA KUTAFAKARI
Soma;Mithali:3:21-35
πππ€π€πππππ
Mambo ya Kuzingatia Katika Haya Maombi ya Usiku.
1.Tembea Tembea au Simama au Piga magoti mbele ya Kitanda.
2.Tamka maneno yaeleweke na yasikike.
3.Tumia Sauti ya kawaida lakini iwe yenye mkanzo na unyenyekevu .
4.Utaomba Kila Siku Kabla hujalala .
5.Utafata maelekezo ya kila ombi lilivyoobgozwa.
Rudia×2
2.Bwana Kama Siyo wema wako kwangu Natambua nisigekuwa hai Wema wako unizunguke kila ubaya unaotumwa Usiku wa Leo Kwangu naomba upague Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia×2
3.Tumaini langu ni wewe Bwana Ulizi wangu ni wewe Bwana hata nathubutu Kusema Mwili wangu ni mali yako niuleta mikononi mwako usiku wa leo unlined Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×4
4.Damu Ya Yesu Ikanifunike Na ikazigire eneo la nyuma yangu Na chumba changu chote Nafunika kwa Damu Ya Yesu Naomba Nikiamini Katika jina la Yesu.Amen
Rudia ×2
5.Ninavunja, ninabomoa kila nguvu za ndoto mbaya kila nguvu za kipepo kila nguvu za uchovu wa Maombi Ninazibomoa ishara zote za kipepo Natengeneza ishara zote za Ki Mungu Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×1
6.Baba Yangu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe mapenzi yako yafanyike usiku wa leo Unikinge kila mishale za yule muovu zisinipate Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×5
7 .Nafungua mlango wa Baraka Kwangu Katika Aridhi hii ya____(Taja ulipo) mfano. Aridhi ya mateteni Nikaimiliki kuanzia afya uchumi na hata kibali kupitia aridhi hii Nikuone ukinibariki Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×3
8.Bwana Yesu Nakupenda Kama ulivyonipenda ukafa kwa ajili yangu nautambua upendo wako kwangu nami ninaomba usichoke kunipenda na kunipigania kwa kila vita inayosimama katika ulimwengu wa roho ambao kwangu mimi siwezi kuuno wewe unaweza kuuona Usipumzike kwa ajili ya utetezi wa roho yangu maisha yangu huduma yangu Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×6
9.Ushukuriwe Mfalme wa Amani Kwa Kunitangazia Amani na furaha ndani yangu nilikuwa sina Amani wala Furaha kutokana na changamoto za Kidunia Lakini Leo Umezibemba Zote shida zangu magonjwa yangu uchumi wangu nk ndiyo maana Ninakushuru Sana tena Sana Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×4
10:Nayafunika mahitaji yangu maombi yangu kwa ulizi wa Damu Ya Yesu Mnazaret Yeye nimemkabidhi naye amepokea mahitaji yangu yakadhibitike nakutendeka kama nilivyoomba Katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×1
@2023 Pastor Richard
Share Maombi haya Kwa Magroup yako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni