Jumanne, 18 Juni 2024

SOMO:NDOA KUGOMBANA NDANI YA NDOA

      "DARASA LA WANANDOA "
 $$$===================$$$

SOMO: NDOA KUGOMBANA NDANI CHANZO BIBLIA INASEMA:

Ndoa nyigi zinapitia changamoto hii ndani ya ndoa eidha ndoa nyigi zilifungishwa bila mafunzo au Wanandoa kutoka nje msingi unaowapasa kuishi Kama Wanandoa wa Kikristo.

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa ndiye ninayekuandalia Somo hili nzuri  kwa msaada wa Roho Mtakatifu. 


Ndoa Zilizo nyingi husababishwa na wao wenyewe Wanandoa kugombana.

HAYA NDIYO HUSABABISHA UGOMVI NDANI MKAKOSANA:


1:MWANAUME ASIYEISHI KWA AKILI NA MKEWE.

Andiko 1Petro;3;7

1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe. 


Mwanaume Anaweza Kusababisha Magomvi ndani ya ndoa  na Kuifanya ndoa yake ikayumba au kukosa mwelekeo watoto wakatawanyika na kuigawa  familia yake kwa kukosa Akili ya kuishi na mkewe ndani ya ndoa

Mwanaume unatakiwa Uishi kwa Akili Sana na mkeo na ufahamu wako uwe juu kuliko mkeo ili kumuongoza vyema katika njia sahihi yenye kumpendeza Bwana.

Ndoa nyigi zilizovunjika mwanaume alichangia kwa kukosa akili yake kuituliza.



2:MWANAMKE MGOMVI MWENYE KUONGEA SANA KUGOMBA SANA.

Andiko Mithali;21:9


Mithali 21:9
[9]Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, 
Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi. 

Ukikosea Kuowa ukaowa mwanamke anayependa maugomvi Kukuza jambo huyu ndani ya ndoa ukimkosea Jambo atalifanya kubwa  Mwanamke Mwenye magomvi huvunja ndoa yake.

Ndoa nyingi zilizovunjika ugomvi ulichangia uliosababishwa na mwanamke akavunja ndoa.

Cha ajabu mwanamke wa hivyo Akiachwa Anaanza kumbuka mume wake na kuanza kuhagaika kwenye maombi.

Elimu ya ndoa hana halafu anatafuta kuombewa akiamini uchawi kumbe Unatakiwa yatafute mafundisho tu ya ndoa na Neno la Mungu yakuponye siyo kuombewa.


     NISHAURI WANANDOA 
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Ninachota kusema Biblia ndiyo msingi wetu wa kila kitu 

Imesema Mwanamke Ijenge ndoa kwa hekima ukitumia mikono yako kazi zako kuleta mabadiliko ndani ya ndoa wewe unaenda kujenga kwenu baadala ya kwenye ndoa.


Mwanaume Biblia imekuambia Tumia Akili ipasavyo unapofanya jambo kwa mkeo au kuishi naye wewe unataka uligane naye akili yako ilale haijishughulishi kutengeneza ndoa yako unaenda kutengeneza kwenu.


Tembea katika misingi ya Biblia ndoa yako itapona.


Kama Hujaungwa Kwenye Group la Maombi na Mafundisho Muombe Pastor Richard Akuunge +255759861768



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni