SEMINA ZA NDOA
SEMINA ZA NDOA
JE NI NINI HATIMA YA NDOA YAKO?
Utangulizi: PANGA KUMALIZA VIZURI
Andiko: Mhubiri 7:7-8
Heri Mwisho wa neno kuliko mwanzo wake.
Ndoa chanzo chake ni Rohoni.Muasisi wake ni mungu .Yoh.4:24 Mungu ni Roho
Tunaishi katika ndoa (a)Kwa Hekima Mith.14:1
(b)Kwa Akili 1Pet 3:7
(c)Kwa Kutii Efe .5:22-24
(d)Kwa Upendo Efe .5:25 -29
(e)Kwa kuheshimiana Ebr.13:4;1Pet. 3:7b;Efe.5:33b Staha.
Tena tukumbuke –Mpango halisi wa mungu kuhusu wanandoa ni huu:-
(i) Mke awe msaada kwa mumewe. Mwa 2 ;18
(ii)Mume amfurahie mke wa ujana siku zote.Ndoa iwe ni mahali pa furaha Mhu.9:9
(iiiMapendo yawe ni ya siku zote.Kusiwepo na kuchukizana –chuki Mith 5:18-19
Ndoa zetu tujitaidi ziwe na
(i)Sifa njema Mhu .7:1;2 Kor.6:3-4;Tujipatie sifa njema
(ii)Ndoa zetu ziwe mfano mzuri /kielelezo chema kwa
(a)Watoto wetu
(b)Waaminio
(c)Wayahudi 1kor 10;32 1tim .4:12.katika usemi,mwenendo ,imani ,upendo,na usafi .
(d) Wayunani
(e)Maisha yatu ya ndoa kumpa mungu utukufu.1kor.10:31
Tunaweza kuiga mfano mzuri wa ndoa za wazee wetu kama adamu, Ibrahimu, Isaka, Nuhu, Ayubu n.k. Ebr.13:7. Walimaliza vizuri tunaona jamopa na magumu mengi, lakini walikuwa na mwisho mzuri. Tuiige imani yao.
02. NDOA INA VITATU VYA AWALI. Ambavyo kila mwanandoa akivishinda__aandelea mbele kwa ushindi na ndoa hiyo inakua na kumaliza vyema.
KITUTA CHA KWANZA
Kumfahamu mwenzi wako wa ndoa.
Katika KITUTA hiki kunapatikana darasa la kuchukuliana na kuelekezana.
Jambo kubwa katika darasa hili ni wanandoa wote kuwa:-
(a) Wa kweli kila mtu kwa mwenziwe.
(b) Wa wazi bila kufichana kitu.
(c) Wanyenyekevu kila mmoja kwa mwenzake.
Kwenye Eneo hili, mke atumie HEKIMA yake aliyopewa na Mungu Mith. 14:1 na BUSARA Mith. 19 :14.
Kusiwepo na kukosoana wala kudharauliana ama kulaumiana bali uvumilivu na kuelimisha kuwe na nafasi ya kwanza haswa katika HAKI za mtu katika TENDO la NDOA. IKor.7:2-5,
Mara nyingi wanaondoa wachanga si wastadi wa TENDO la NDOA maana hawana ujuzi wala uzoefu ; wala hawajui kujizuia au kungojana ili wapate kufikia shibe ya raha yao kwa pamoja .
Vile vile hawajui hata namna (style)mbalimbali za tendo la ndoa ambazo ziko kama 9na 4 maalum ambapo mke ni mjamzito (mgo –solo –mago –ina –wima –kichu –juu –mapa –kuge ,kistu )INAHITAJI MOYO WA UNYENYEKEVU :ili wanandoa hawa wapate kujifnza na kupata uzoefu (experience) .Inahitaji kocha nao watajipa uzoefu wao kwa kungojana na kuchukuliana hadi waufikie ujuzi wa TENDO la NDOA katika hali ya kutoshelezana.
Inawezekana mtu kufanya tendo la ndoa kwa dakika 5,au 10 au 20au 30 kwa ustadi akamtosheleza mwenzake – lakini inatofautiana mtu na mtu – pia inatofautiana katika maumbile, kwa mfano:-
- Wanawake wanene wana namna yao na kiwango chao mpaka wafikie kutosheka
- Wanawake wembamba nao wana namna yao hadi kufikia kilele
- Na wale wa umbo la kati wana jinsi yao ili kufikia kilele
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni