Alhamisi, 20 Juni 2024

SOMO; VILIMA VITATU NDANI NDOA VYA KUVUKA

SOMO: VILIMA VITATU NDANI YA NDOA VYA KUVUKA.

Nimeamua Somo hili nilipe kichwa cha Somo kinachosema Vilima ndani ya ndoa ambavyo kila mwanandoa aliyemo huwa lazima Avishinde hivi ili kuifanya ndoa yake izidi Kuwa na Furaha na Amani

Mwanandoa na Unayetarajia muingie kwenye ndoa Fatana na Mimi Katika Darasa hili.

Mwaadaaji ni Mimi Mwalimu Wa Wanandoa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 


         VILIMA NI NINI?
Ni vitu vya kuvuka ili ufike hatua nyigine ndani ya ndoa

VITU HIVI HAKIKISHA UNAVIVUKA  NDANI YA NDOA.

      MLIMA WA KWANZA;
      =====$$$=====$$$$
1;MJUE VIZURI MWEZAKO 

Mkeo au Mmeo Unatakiwa umjue na ujue Madhaifu yake na Mapungufu alimonyo Uelewe Namna utakavyomchukulia na kuyabembelea madhaifu na siri zake.

1 Wakorintho 11:3
[3]Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. 

MAMBO MATATU YAWE SILAHA YA KUVUKA.

1:Mpende Sana Na Udhaifu wake alionao.

2:Usimuumize au Kumdharau kwa alivyo.

3:Vumilia Hatua Zake Usitoke nje hata kama yeye anatabia hiyo usiinge.

Wewe Mshukuru Mungu Kwa Zawadi hiyo.
Mfanye Awe mtu anayempenda Mungu na Aliyekaribu na Mungu.

  MFUNDISHE HAYA
=================
1;Utoaji: mweleze Baraka na Umhimu wa kutoa zaka na kuwa waaminifu wa Fungu la kumi.

2:Ibada: Mfundishe Na Kuweka Utaratibu wa Kufanya ibaada kabla hamjalala.

3:Ushirikiano; Mfundishe Awe Mwenye kufanya mambo kwa umoja na umuondolee ubinafsi wa vitu mbalimbali alivyo navyo.

4:Tengenezeni Mipango Mikakati maisha yenu ya kiroho na Ya Kimwili yawe yenye mafanikio.

               3 Yohana 1:2
[2]Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 


TENGENEZENI PEMBE TATU KATIKA MAFANIKIO YENU NDANI YA NDOA

●Pembe ya Kwanza Muwekeni Mungu.

1:MUNGU: mtu yeyote mwenye Mungu ndani yake atakuwa mwaminifu mwenye upendo mwenye kujielewa atailea ndoa yake

●Pembe ya Pili Muweke Mkeo

2:MKE: Muweke mkeo usiweke wapenzi wa zamani au wazazi 

Mke wako ndiye mjenzi wako wa ndoa yenu.

●Pembe ya Tatu Muweke Mmeo.

3:MUME: Muweke mmeo sababu ndiye kiongozi na dereva wako ndani ya ndoa 


Mafanikio yatakuja ukipangilia hivi nilivyokuwekea.


   .MLIMA WA PILI .
  ================

2;TENDO LA NDOA:

Tendo la ndoa ni kitendo cha kukutana kwa jinsia mbili ya kike na kiume Hii ndiyo huleta muuganiko wa ndoa na Tafsiri ya Mwili mmoja.

Mwanzo 2:23
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. 

Mwanandoa ni Haki Yake Kupata Tendo la ndoa Bila Kuwekewa mpaka au kunyimana.

Japo ndoa nyingi Huingia kufanya tendo la ndoa pasipo na uzoefu au kufanya maandalizi ;

Tendo la ndoa Linaitaji Utulivu wa akili na Usifanye Tendo la ndoa kwa kulazimisha.

Andiko;

1 Wakorintho 7:5
[5]Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 


STAYLE ZA UFANISI WA TENDO LA NDOA.

Kuna stayle nyingi Sana Katika Tendo la Ndoa na Kila stayle ina Eneo lake la kutumika ndani ya ndoa uwapo na mwezi wako.

1:Stayle Za Kufanya Tendo la ndoa ukiwa unaitaji mtoto

●.hapa unatakiwa ufanye Tendo la ndoa katika Mikao Inayomfanya mkeo au wote wawili kutoshelezana na Kufikia kileleni haraka kwa mkeo.
●Fanya Tendo la ndoa Mkiwa hamjagombana kila mmoja afurahie tendo la ndoa 

●Usifate Kalenda Mimba huweza kuingia hata bila Kalenda.


2 STAYLE YA KUJENGA AKILI NA KINGA YA MWILI.

Hii unatakiwa ufanye Tendo la ndoa Akili inapoelemewa  na vitu au kuzidiwa inafanya akili ijitengeneze katika uharaka tena wa kutatua vitu.

●Hii huwa Ni mtindo wa stayle Ambayo mkeo au mumeo itamchelewesha kufika kileleni  yaitaji ufanye mara kwa mara ili kuziimarisha Akili zako.


FAIDA YA TENDO 

1:Utapata watoto

2;Utafungulia Baraka mbalimbali 

3;Huondoa magonjwa mbalimbali 

4;Huongeza muonekano na mvuto kwa mwanamke.
Nk

     HISIA ZINATOFAUTIANA
.
●Mwanamke mnene hisia zao zinatofautiana na wengine

Nao Wanaitaji Uweze Kupata Uzoefu Umjue Vizuri na hata ushikaji mimba kwake hutofautiana na wengine.



●Mwanamke Mwembamba hisia zake kwenye Mwili wake ni tofauti na mnene.

Ni vyema mwanaume Aliye naye kumwelewa ili usifanye tendo la ndoa kwa kulazimisha naye.

●Mwanamke WA Kati hisia zake tofauti na za wengine hata kushika kwake mimba tofauti na wengine.


Nimegusia haya ili mwanandoa Ajue wanawake wameumbiwa Hisia Tofauti katika Tendo la ndoa Tofauti na mwanaume.

Kuzichochea hisia Zitatengemea na Mwanamke uliye naye ndani ya ndoa 

MAMBO YA KUZINGATIA 

1:Fanya usafi kila baada ya Kutoshelezana.

2:Fanyeni maandalizi ya kihisia kuvutana katika tukio hilo.

3:Ombeeni Tendo la ndoa 


Ndoa nyingi zimevunjika kupitia Tendo la ndoa kulifanya bila maandalizi ya kihisia au kutokumjua mkeo hisia zake ukajua wanawake wote wako na hisia zinafanana kumbe hapana.

Jifunze kila siku kwenye Tendo la ndoa ili uwe bora na mwepesi katika eneo hili.


          MLIMA WA TATU

3:LINDA PATANO LA KIAPO CHENU CHA NDOA

Hiki ni kipengele mhimu simamia na kulinda makubaliano Yenu.

Wanandoa Wengi Wanapopita katika vile vipindi vitatu ndani ya ndoa utaona wanaanza kugombana hasa wanapokuja kufanikiwa 

Mwanamke au mwanaume simamia Patano la ndoa Yenu.


Ndoa hujengwa na nyinyi wawili msipende kutoa siri zenu za ndani hakikisheni usalama wa ndoa Yenu.


TUFANYE NINI SASA 

Tunapaswa Tuvuke Milima hii Ili kufikia Ushindi ndani ya ndoa zetu.

WITO
Shirikisha jumbe huu na watu wengine

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni