Ukijiona wewe kila ukikaa unaijiwa na mawazo mabaya au kuwaza kuacha Kufanya Biashara au Kuacha Kazi au kumuwazia mabaya mwigine hiyo huwa ni njia moja wapo ya shetani na mapepo kukuingia nakukufanya ukate tamaa kabisa
OMBA HIVI
Shika kichwa chako pembeni mwa masikio.
1.Ninavunja nakubomoa Kila Wazo mbaya ndani yangu mawazo ya kipepo mawazo ya kukata tamaa au kurudi nyuma katika mipango yangu nakataa nafuta kuwaza vibaya ndani yangu kwa Jina la Yesu.Amen
Rudia x 4 Kuomba.
Soma hii mistari
👇👇👇👇👇
Zaburi 139:23
[23]Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu,
Unijaribu, uyajue mawazo yangu;
Ruhusu Mungu Aongoze Mawazo yako
Moyo wako akuchunguze.
👇👇👇👇👇
Ayubu 20:2
[2]Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu,
Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.
Usiwe na haraka haraka kufanyia kazi kila unalowaza maana wazo huleta matokeo.
OMBA na UJIWEKE UWE KARIBU NA MUNGU KWA MAOMBI MTAFUTE BWANA.
Soma hii mistari kisha tafakari.
👇👇👇🗣🗣🗣🗣🗣
Isaya 55:6-8
[6]Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,
Mwiteni, maadamu Anapatikana.
[7]Mtu mbaya na aache njia yake,
Na mtu asiye haki aache mawazo yake;
Na amrudie BWANA,
Naye atamrehemu;
Na arejee kwa Mungu wetu,
Naye atamsamehe kabisa.
[8]Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Kanisa la Holy Spirit church MOTO WA YESU
SHARE MAOMBI HAYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni