Naitwa Pastor Richard
Nipo Morogoro Veta Dakawa
MAOMBI NI NINI..?
Maombi ni Pumzi Ya Mtu aliyeokoka au mkristo yoyote maisha yake ya kiroho na mwili yanatengemea Maombi Sana ili Aweze Kujiweka Sawa.
MAOMBI Ni Namna Mtu Anavyoweza Kwenda Katika Ulimwengu Wa Roho Kuyaweka Sawa mambo yake anayoona hayaendi Sawa.
SABABU YA SISI KUOMBA KAMA WANA WA MUNGU NI HIZI.
. Zifuatazo ni sababu kuu zinazopelekea watoto wa Mungu kufanya maombi;
1. Maombi ni uchaguzi wa Mungu wa kuzuia nguvu na kazi za shetani (Mathayo 6:13; Waefeso 6:12, 18).
2. Maombi hutupatia msaada wa Mungu katika kila hali (Zaburi 3:3-4; Zaburi 34:4, 6).
3. Maombi yanaondoa vikwazo au vipingamizi vyote (Marko 11:23-24).
4. Maombi ni njia ya kupata amani tunapokabiliwa na hali ya kutisha na kukatisha tama (Wafilipi 4:4-7).
5. Maombi hugeuza mioyo na tabia ya watu wengine (Nehemia 2:4-8).
6. Maombi ni njia ya uponyaji wa kimwili na kiroho (Yakobo 5:14-15).
7. Maombi huleta msukumo wa kiroho na kumtia mtu nguvu wakati mtu fulani anapokabiliwa na hali ya kushindwa (Wakolosai 1:9-11).
MAOMBI NDIYO NJIA PEKEE YA KUDAI HAKI ZAKO NA KUMKUMBUSHA MUNGU.
Isaya 43:26
[26]Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
KWA HAYA NADHANI UMEELEWA KWANINI UNATAKIWA UOMBE NA SIYO KUWA UNASOMA KUOMBA HUOMBI Fanya mazoezi ya kuomba ujue ili udai haki zako mwenyewe Umweleze Bwana.
@Pastor Richard 2024 Hatutembei Kinyoge Sisi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni