Jumamosi, 21 Februari 2026

MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA 2026

MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA

Naitwa Pastor Richard 

Karibu kipindi cha maswali na majibu


1:SWALI LA KWANZA. Baada ya Yesu kufufuka alikaa na wanafunzi wake siku ngapi kabla ya kupaa kwenda mbinguni?. N.b weka andiko ku sapoti jibu lako

JIBU:   Alikaa na wanafunzi wake muda wa siku Arobaini(40). Matendo ya Mitume 1:3  wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, *akiwatokea muda wa siku arobaini*, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.


2:SWALI LA PILI. Tukio la Yesu kupaa kwenda mbinguni lilitukia eneo gani?. N.b weka andiko ku sapoti jibu lako

JIBU:    Mlima wa mzeituni. Matendo ya Mitume 1:12 [12]Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.


3:SWALI LA TATU. Ni wanafunzi wangapi waliopokea Roho Mtakatifu ile siku ya pentekoste? N.b weka andiko ku sapoti jibu lako

JIBU: Wanafunzi miq na ishirini (120). Matendo ya Mitume 1:15 [15]Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu ( *jumla ya majina ilipata mia na ishirini*), akasema,



4:SWALI LA NNE. Je! Malaika wote wana mabawa?

A) ndio

B) hapana✅

N.b weka andiko ku sapoti jibu lako

JIBU: Hapana Waebrania 1:13-14 [13]Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume. Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? [14]Je! Hao wote *si roho watumikao*, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Malaika ni roho (A spirit being does not need wings in order to fly)


5;SWALI LA TANO. Taja majina ya wanafunzi wawili wa Yesu waliopigiwa kura kuchukua nafasi ya utume ya Yuda Iskarioti aliyemsaliti Yesu N.b weka na andiko kusapoti jibu lako

JIBU:   Yusufu na Mathiya

Matendo ya Mitume 1:23 [23]Wakaweka wawili, *Yusufu*, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na *Mathiya*.


6;SWALI LA SITA. Mwandishi wa sura ya kwanza ya kitabu cha Matendo ya mitume ni;

A) Petro

B) Luka 

C) Theofilo

D) Mariamu mama yake Yesu

N.b weka na andiko ku sapoti jibu lako


JIBU:   Luka. Kwa sababu ya utangulizi wake alio uweka ambao unaendana na mwanzo wa injili ya Luka

Matendo ya Mitume 1:1 [1]Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, *Theofilo*, katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha

Luka 1:3 [3]nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, *kukuandikia kwa taratibu, Theofilo* mtukufu,


7;SWALI LA SABA Je! Ni kweli kwamba siku ya pentekoste ni siku ya kujazwa Roho Mtakatifu? N.b weka na andiko ku sapoti jibu lako

JIBU:  Hapana,ni siku ya kukumbuka ujio wa Roho Mtaktifu ndani ya watu. Tuanzie hapa

Matendo ya Mitume 2:1,4 [1]Hata *ilipotimia siku ya Pentekoste* walikuwako wote mahali pamoja. [4] *Wote wakajazwa Roho Mtakatifu*, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

 Asili ya pentekoste ni kutokana na sikuku kuu zilizokuwa zikifanywa huko nyuma na zilikuwa zikiendelea. Sikukuu za mavuno baada ya mavuno walikuwa wakikusanyika pamoja kusherekea mavuno yao

Matendo ya Mitume 2:5 [5]Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu.

Hawa walikusanyika yerusalemu kusherekea mavuno/malimbuko  yao na kuleta malimbuko  siku ya hamsini. Sikukuu ya malimbuko  tunalinganisha na UFUFUKO wa Yesu

1 Wakorintho 15:23 [23]Lakini *kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo*; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. Kwa Hiyo siku ya Pentekoste tuadhimisha kumbukumbu ya ujio wa Roho Mtakatifu na sio kwamba ndiyo siku mtu anatakiwa kujazwa Roho Mtakatifu




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni