SOMO:SILAHA ZA MAOMBI LEO USIKU WA MANANE
Jifunze Kutumia Silaha Za Bwana unapopambana katika Maombi yako ya Vita shambulia Adui Zako kwa Silaha.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
1) KUTAWANYWA USEMI:
ππππππππ
Andiko la kusimamia (Mwanzo 11:7-9)
. Kama alivyouvuruga usemi wa wajenzi wa wasielewane, vivyo hivyo akavuruge hila za ibilisi na mapepo yake zisipatane juu yangu Vikao vyote na mipango inayopangwa kwenye maisha yangu Vurunga vurunga Bwana Kwa Jina la Yesu.Amen
RUDIA×5
2) MOTO WA BWANA:
πππππππππ
Andiko la kusimamia (2Wafalme 1:10).
"Moto ukaunguze mapando yote, ya ibilisi, aliyoyapanda moyoni mwangu kila roho na nguvu zozote ndani yangu zinazonifatilia au kutilia mkazo naziunguza Moto wako Bwana Katika Jina la Yesu.Amen
RUDIA ×5
3) NZIGE, PARARE, MADUMADU, TUNUTU:
ππππππππππππ
Andiko la kusimamia (Yoeli 2:25).
Bwana akatumie jeshi lake la Nzige, Parare,Tunutu,wakatafune kazi zote za mwovu, wakalete hasara, warudishe nyuma, na kudhoofisha ufalme wote wa giza Katika Jina la Yesu.Amen
RUDIA ×7
4) MAJIPU YA BWANA:
ππππππππ
Andiko la kusimamia (Kutoka 9:9).
Bwana alete hali mbaya ya mateso, kwa wakuu wote wa giza wafanyao vita juu yangu wanaopanga ubaya juu yangu katika Jina la Yesu.Amen
RUDIA ×4
(5) TETEMEKO:
πππππππππ
Andiko la kusimamia (1Samweli 14:15) .
"Bwana alete utisho na mashaka, na tetemeko kwa wakuu wa giza na mapepo yasimamopo kinyume cha kazi ya Mungu Ndani yangu au kwenye Maisha Yangu Katika Jina la Yesu.Amen
RUDIA ×9
(6) UKAME (KIU na NJAA):
Andiko la kusimamia (Amosi 8:11).
Bwana alete ukame wa kiroho, kwa majoka yote yanayosimama kutaka kumeza uchumi wangu au kazi yangu Katika Jina la Yesu.Amen
RUDIA×5
(7) RUNGU LA BWANA:
πππππππππππ
Andiko la kusimamia (Yeremia 51:20).
RUGU LA BWANA Lipige na kuleta majeraha katika ufalme wa giza, liziraishe na kupoozesha mapepo yote na vikaragosi vyake vyote vifanyavyo vita na wewe
Zipo na silaha nyingine nyingi katika maandiko Hatuwezi kuziorodhesha zote, Hivyo kwa jinsi Neno la Mungu linavyokaa ndani yako, ndivyo utakavyoweza kuzivumbua na kuzitumia. Na zote hizo ni sharti tuziombe katika jina la Yesu na uweza wa damu yake.Maombi ya namna hii yana nguvu sana, na yatakufanya udumu kwa muda mrefu katika kuomba. Na kufungua vifungo vingi sana katika ulimwengu wa Roho.
Kumbuka pia, vita hivi hatuvielekezi kwa wanadamu, bali kwa Shetani na majeshi yake ya mapepo na kazi zake zote. Kwasababu maandiko yanasema vita vyetu sio juu ya damu na nyama, maana yake ni kwamba sio juu ya wanadamu wenzetu. Bali ni juu ya falme za giza, zikawaachilie mateka, waje kwa Bwana, na sio tuwaue wao pamoja na mateka wao.
Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 6.13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama”
Nasimama Kuwapinga majeshi na wakuu wa ngiza hili wanaofatilia hatua za maisha yangu Katika Jina la Yesu.Amen
Share kwenye Group Zako mbalimbali
WhatsApp Group +255710889892
Endelea Kuwaunga Watu Kwa Group
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni