SOMO; UTOFAUTI WA AGANO LA UZINIFU NA AGANO LA TENDO LA NDOA NDANI YA MTU.
Mwanzo 4:25
[25]Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.
Adam ni Mwanandoa Akiwa Na Eva Mkewe.
Kabla ya Kuowa Adam Alikuwa Akitembea na Agano la Tendo la ndoa hivyo hivyo hata Eva Kabla hajaolewa Alikuwa Akitembea na Agano la Ndoa
Tunasoma
.Mwanzo 2:23
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
AGANO LA TENDO LA NDOA.
Huwa linamvuta Mtu Aingie Kwenye ndoa Linamtenga Mbali na Agano la Uzinifu Kwakuwa Tayari Adam na Eva Walijitunza na hawakuzini Mpaka Mungu alipo wauganisha Pamoja.
Mwanzo 38:24
[24]Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe.
Tamari Aliingia Kwenye Akiwa na Agano la Uzinifu lilimtesa Sana ndani ya ndoa
Mtu mwingine mke wa Hosea Aliingia Kwenye Ndoa na Agano la Uzinifu.
Hosea:2
UTOFAUTI AGANO LA TENDO LA NDOA NA UZINIFU.
========÷÷÷÷÷=====÷÷÷÷
ISHARA ZINAZO KUJULISHA UPO AGANO LA UZINIFU
1;Kuwa na Hali ya Mwili wako Kutumika Katika Kuzini Mara kwa Mara.
2:Kupata Wachumba Ambao ukiwapata lazima Uzini nao na Ukizini nao Tu Mnaachana.
3.Kupata Wanaume Wenye nia ya Kukuowa Unavunja hali fulani ya nyinyi kugombana Mahusiano yenu yanaishia njiani.
4;Kuwa na nguvu ya kuzalia nyumbani watoto kila mtoto na Baba yake.
5:Kuwa na mvuto wa wanaume kukutamani Kimwili siyo kukutamani wa kuowe.
6:Kuwa na Historia za kuvunja mahusiano yanayoeleweka na kudumu katika mahusiano yasiyoeleweka.
AGANO LA TENDO LA NDOA.
1:Kuwa na Hali ya Kuchukia Dhambi ya Kuzini na Kuepuka mwenyewe.
2:Ukifanya dhambi ya Kuzini moyo unakosa Amani na Utalia Sana.
3:Kutokuzaa Kabla ya Kuitwa mke wa mtu.
4;Kuutunza Mwili wako na Kuepusha na Dhambi.
5: Kuwa na Msimamo wa ndoa siyo uchumba.
6:Kutokukaa Katika Agano la Uzinifu
Huwezi Kuendeshwa na Dhambi ya Kuzini.
TUFANYE NINI SASA.
Watu wengi Hutembea na Agano la Uzinifu Bila Wao Kujua Wanapotamani Kuowa au Kuolewa roho zinaanza Kuwazuia ndoa nakutaka kuwapeleka wawe Wanazini Bila hata utaratibu Watajitaidi kuombewa ila roho ya uzinifu inawavuta tena Ni ngumu kuingia kwenye ndoa.
NAMNA YA KUJIONDOA KWENYE ROHO HII.
1:Kuweka msimamo wa kutokuzini.
2:Kukataa kuitwa mama kabla ya kuitwa mke wa mtu.
3:Kukataa Kuwa unajirahisisha.
Dhambi ya kuzini huhitaji msimamo tu kwamba sitaki kuzini
Ansate Sana
Niulize inbox Swali kama Hujaelewa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni