Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kutoka Kanisa la Holy Spirit Tanzania
Kuna Uponyaji Katika Kuondoa Vitu unavyoviona Havikufai Wewe na Siyo kukaa mpaka mwingine Aje Akuondolee mfano mzuri Wewe ukiombewa unaanguka mapepo lazima uondoe hayo mapepo kwa kuacha kukiri huo udhaifu kuwa unaaguka na mapepo
Mfano; Wewe huolewi ukipata wanaume Wanaishia kukundaganya tu Hii hali Kama Wewe Mwenyewe Hutaiondoa Tengemea Itaendelea hii hali kukutesa Sababu umeishikilia hutaki kuiachia.
Unatakiwa Uache Kujikubali kuwa wewe unamatatizo ya kutokuolewa kubali wewe unaolewa si muda tembea na imani hiyo.
Kwa mfano Umekuwa ukiomba kazi hepati ujue ipo nguvu inayozuia ukiendelea kukubaliana na hiyo hali ukawa unasema mimi sipati kazi kila maombi nikituma sijibiwi utaendelea kutokuvuka hilo eneo.
===$$$$=====$$$======$$$=====$$$$$
Mhubiri 11:9-10
[9]Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
[10]Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.
ZINGATIA HAYA UOMBAPO;
====::::::::====:::::::::=====:::::
1;Ondoa Kinywa Kinachokufanya Ukiri Udhaifu.
2:Weka Kinywa Chenye Kukiri Ushindi na Kujitamkia Baraka mwenyewe
3:Fata Muongozo na Masomo Kama ninavyokuongoza Vitu vingi utaviondoa kwenye maisha yako.
4;Jikubali wewe ni wa kubarikiwa siyo wa kuteseka na kulia Lia.
TUNAVYOTAKIWA KUOMBA SASA
MSTARI WA KUSIMAMA
Marko:16;3-4
1;Bwana Yesu Naondoa Kila Mzingo wa Mawazo Akilini Mwangu Katika Jina la Yesu.Amen
2:Bwana Yesu Naondoa Kila Mzingo wa fikira mbaya fikira za kushindwa ndani yangu katika Jina la Yesu.Amen
3;Baba Katika Jina la Yesu Ninaondoa Kila Namna inayosababisha maisha yangu yawe ya kukwama au kutokuwa na hatua hiyo roho Ichomoke iniachie katika Jina la Yesu.Amen
4:Naondoa Hofu ndani yangu Hasira ndani yangu Kuanzia muda huu kwa jina la Yesu.Amen
5:Naondoa Huzuni na Mawazo moyoni mwangu siyataki katika Jina la Yesu.Amen
6;Naondoa Usingo ndani yangu Siutaki kabisa katika Jina la Yesu.Amen
7:Naondoa Ndoto mabaya nazifuta Katika Jina la Yesu.Amen
8:Naondoa Vizuizi mbele yangu sivitaki Katika Jina la Yesu.Amen
9:Naondoa Na kufuta Kila Vifungo vya manano katika Jina la Yesu.Amen
10:Naondoa kila ugumu na majaribu ninayoyapitia katika Jina la Yesu.Amen
Omba kwa mfumo huu Ombea kuondoa Vitu mbalimbali vinavyokutesa
Sababu ukiona hali yeyote unayoipitia ujue katika ulimwengu wa roho umeisaini mwenyewe iendelee kuwa hivyo unavyoiona lazima uondoe Saini zako kila eneo ulilokubali na kuliishi.
Muda wowote haya maombi uombe
Tenga utulivu usafiri nao katika kuomba tu Maombi ya Kuondoa Yanalenga uombe ukiwa unatembea tembea Tamka neno kuondoa
Tusome👇👇👇👇👇
Marko 16:3-4
[3]wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?
[4]Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno.
I
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni