SOMO; MSINGI IMARA WA NDOA
Naitwa Mwalimu wa Wanandoa Pastor Richard Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
Msingi Wa Ndoa Huanzwa Kujengwa Kwenye Uchumba Kabla hata hujampata mtu wako Sahihi Isaka Anasema Wakati Anamtafuta Rebeca Akaweka Vingezo Au Sifa Ya Kile Anachokitaka. Hicho ndicho kilichowaunganisha Rebecca na Isaka Vingezo alivyo navyo Rebeka Wengine hawakuwa navyo.
1;MSINGI WA KWANZA ANASIFA TOFAUTI NA WENGINE NDIYO MAANA UMEMPENDA.
Mwanzo;24 Habari ya ndoa ya Isaka.
Mwanamke au Mwanaume Mpaka Unakubali kuolewa au Kuowa ukafunga ndoa umemuona Anasifa tofauti na Wanawake Wengine heshimu hilo na ulinde na kutunza siyo siku mbili tu umeanza kuona Sifa zile hana umeanza kutamani wengine.
2:MSINGI WENU WA PILI; RUHUSU MUNGU MWENYEWE AWE MJENZI WA NDOA YENU.
Mnapoyapa nafasi maombi na Ibada Kwenda Kanisani kuomba kuombea malengo yenu na Kuwa Waaminifu Wa Fungu la Kumi Mnamfanya Mungu Aijenge ndoa Yenu Vizuri Tena Kwa Upendo
SOMA HII MISTARI;
Zaburi:127;1
Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.
2 Wakorintho 3:17
Basi ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
===========================/
2:WAPENDENI NDUGU ZENU PANDE ZOTE MBILI;
Wakija ndugu kuwatembelea Unaweza ukaandaa kasupu kawasaki na Vinyard vya kukaaga mama wake zako unawakaribisha huku unajiongelesha yani huku mboga za shida Tumeamua tuwaandalie hii Mboga Mtusamehe tu. Wanawishe kwa heshima hapo.
SOMA MISTARI HAYA:
Warumi 12:10-15
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
===========================
3:MSHIRIKIANE NA JAMII INAYOWAZUNGUKA MFANYIKE BARAKA KWA JAMII:
Shirikiana Na Jamii Katika Mambo Ya Msingi Ambayo hayakutengi na Mungu wako kama msimba maendeleo na Harusi mbalimbali nk unapokuwa umepewa taarifa.
Mithali 1:14-16
14 Wewe utashirikiana nasi; Tutakuwa na vitu vyote shirika.
15 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao; Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
16 Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.
=================================
4:LINDENI HESHIMA YENU.
Jamii inayowashuhudia kwenye tukio la ndoa ambalo Tunalitaja Kuwa la heshima hiyo hiyo jamii itakuja kuwashagaa Mkija Kufanya mambo ya Ajabu.
Mfano; Mkaanza Kupigana Au Kunyanyasa watoto wenu mtakaobarikiwa nao.
Kosa lingine lipo kwa Mwanandoa Akaanza kumpa nafasi za mke wake mwanae mfano ukipata pesa mwanao ndiyo unamkabidhi mkeo anamuomba mwanao au kwenda kulala chumbani kwa mwanao Hii inaondoa heshima Sana.
MISTARI YA KUSOMA
Zaburi 111:3-5
3 Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele.
4 Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; Bwana ni mwenye fadhili na rehema.
5 Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele.
=================================
5:MIOYO YENU IFUNGUKE NA KUWEKANA WAZI USIYOYAPENDA NA UNAYOYAPENDA.
Hakikisheni Tabia Ambazo Unaziona Zinataka Kuingia kwa Mwezako Unakaa naye chini Kwa Utaratibu Na Kwa Heshima muulize Tu Kwanini Anafanya Kitu Ambacho Ulishamwambia Hupendi Pia Mweleze Wewe Unapenda hiki na hiki.
===============================
MISTARI YA KUSOMA
Mithali 17:26-28
26 Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri; Wala si kwema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.
27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
==============================
6:MALIZENI TOFAUTI ZENU NYINYI WENYEWE.
Kila Mnapokuwa mmetofautiana Au Kugombana Mnatakiwa Mmalize Tofauti Zenu Wenyewe bila kuzitoa nje. Msifanye Tofauti Zenu Zikafikia Hatua Zikawa Kubwa mpaka mkashindwa kuzitatua.
=======÷==========÷÷÷÷÷÷==========
MISTARI YA KUSOMA
Wakolosai 3:13-17
13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
7:CHANGUENI WALEZI WA NDOA YENU WALIOKAA MUDA KWENYE NDOA
Sifa za Mlezi wa ndoa
a)Awe Amedumu kuanzia miaka 3 Nakuendelea
b)Awe na Hekima na Busara
C)Awe Mwenye Kuingwa na Mfano wa ndoa yake.
Mithali 11:14
Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
8;Kila Mmoja Aufundishe Moyo wake Kupenda na Kuongea maneno ya Hekima .
Nyinyi ni Wanandoa Mnatakiwa Kupendana na Kuvumiliana Kila changamoto mtakayokuwa mnakutana nayo.
⁶Yohana 13:34
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
9:MANENO MATATU YENYE USHINDI
1:Vumilia Katika Kila Kipindi
1 Petro 2:19
Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo isivyo haki.
2:Usiongope changamoto za Kwenye ndoa
Yeremia 1:8
Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.
3;Amini Kila Jambo linasababu yake.
Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
10;MAFANIKIO NA UPENDO NDANI YA NDOA
MAFANIKIO HUJENGWA NA VITATU HIVI;
1;MUNGU AWE NAMBA MOJA.
Msifanye jambo lolote bila kumhusisha Mungu.
2;MKEO AWE NAMBA MOJA .
Usifanye kitu chochote bila kushauriana na mkeo
3:MUME AWE NAMBA MOJA.
Usifanye Kitu chochote bila kushauriana na mumeo.
UPENDO HUJENGWA NA VINNE.
1;Tumia Neno la "NAKUPENDA" lifelike kwa mwezi wako mara kwa mara
Muite majina mazuri mazuri Hanny Sweet My love mke wangu mume wangu nk
2:Tumia Neno "SAMAHANI" kila mnapokoseana au kwenda tofauti tumia neno Samahani mume wangu.
3:Tumia Neno "ANSATE" kila unapoletewa kitu au kupewa kitu na mwezi wako.
4:Tumia Neno "POLE" Kila Unapomuona mwezako ametoka kazini au chochote Kile Kinachoonesha neno hili litumie.
Nataka Kusema Ndoa inajengwa na nyinyi wawili na wawili nyinyi mnaweza Kuivunja ndoa Lindeni Agano hili mnalolipokea leo liwe mfano wa Kuingwa kwenye mioyo Yenu..
@Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
Maoni