Ijumaa, 13 Desemba 2024

SOMO; MAOMBI YA KUKATAA AIBU.

SOMO; MAOMBI YA KUKATAA AIBU.

Mstari Wa Maombi; Isaya:54:4-10

Ipo hivi Unapokuwa unaishi kuna watu wako waliokuzunguka hutamani uaibike au ufedheheshwe eidha na watoto wako au mume wako au mkeo au mwenyewe kwa hiyo vita itakuwa inainuka ya kukuvunja moyo ukate tamaa au uache msimamo wa imani yako yenye ushindi uingie kukubaliana na imani inayoenda kukuangusha.

MFANO HUU;
Mama anamabint zake wanne wamesomo vizuri lakini hawaolewi na wote wazalia nyumbani kumbe ni nini kinaendelea kwenye ulimwengu wa roho imetumwa roho ya Aibu imfedheheshe yule mama na wanae katika jamii kama hataliita Jina la Yesu Kwa Moyo unaweza kushagaa wanaishi na wanaume bila utaratibu. 


Wengine aibu zinawapata makazini ofisi Zima inatambua unatembea na bosi kumbe unateswa na roho ya aibu.

Yaani mtu mwenye aibu popote akiishi atasababisha aibu tu. Hii ni roho ambayo ni mbaya mno ikikutumikisha lakini LEO Katika Maombi Utaleta heshima kama ya Rebecca  au Yaeli Wanawake waliosimama kuleta heshima mpaka Leo Tunawasoma.



MAOMBI OMBA HIVI;

Kwanza ili ujue kuomba jifunze kutamka nakufanya mazoezi ya kuomba mara kwa mara

1:Naikataa Aibu Ya Kuzaa Nje Ya ndoa nakataa Aibu Ya kuishi na Mwanaume ambaye hajafata taratibu nakataa aibu hii naikataa kwa Jina la Yesu.Amen 


2;Kila Aibu iliyotumwa juu yangu mwaka huu niipate natamka I iachie katika Jina la Yesu katika Jina la Yesu.Amen 

3:Nafuta kila Maneno ya Aibu yaliyowahi kutamkwa kwangu kwa jina la Yesu Naondoa Kila Aibu iliyotamkwa kwa wazazi wangu Katika Jina la Yesu.Amen 

4:Natengeneza Maisha ya heshima siitaki aibu kwangu Katika Jina la Yesu Naifuta Naifuta kabisa Katika Jina la Yesu.Amen 

5;Naidai heshima yangu iliyoibiwa kwa maneno au kwa macho Narundisha  Heshima yangu katika Jina la Yesu.Amen 

Endelea kutamka maneno ya kudai heshima yako nakuikataa aibu Fata mfano wa uwasilishaji kama nilivyotamka mimi.



Shirikisha ndugu zako wazazi wako nk


Kujiunga kwenye group la maombi na mafundisho nitumie ujumbe WhatsApp kwenda+255759861768

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni