SOMO:MAOMBI YA USIKU. KABLA HUJALALA
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
Karibu Maombi Ya Kuomba ulizi Usiku Mungu Akulinde Omba hivi.
6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;
Isaya 62 :6
๐ Baba katika jina la Yesu , achilia nguvu yako , mamlaka yako,na uweza wako juu ya yule baba, mama, kaka na dada katika familia yake usiku huu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.Amen
๐Katika jina lipitalo majina yote la BWANA wetu YESU KRISTO wa Nazareth tunaagamiza kila silaha iliyotengenezwa toka kwenye ufalme wa giza kumdhuru yule baba mama , kaka na dada pamoja na familia yake , tunawasambaratisha wote waliokaa ili kumtumia mabaya na mateso ,tunawaangamiza hata majini na mapepo na wanyama , wadudu au ndege waliotumwa kuleta mabaya wakati wa kulala katika jina la Yesu .
15 Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.
Isaya 54 :15
16 Tazama, nimemwumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu.
Isaya 54 :16
17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.
Isaya 54 :17
๐ Tunaondosha kila pigo na nguvu za mauti kwa yule baba, mama, kaka , dada pamoja na familia yake katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
๐Ee roho ya Mauti , mauti ya magonjwa kwenye macho , tumbo , kichwa , masikio , kifua, moyo , milango ya uzazi , miguu , mikono , uti wa mgongo , ngozi n.k .Tunakuamuru katika jina la,Yesu toka , achia mwili wa yule baba,mama, kaka,dada ,na familia yake na marafiki zake , roho ya mauti hutainuka tena tunakuseta kuzimu katika jina la Yesu .
๐Wasimamizi wa ndoto mbaya , majoka ,roho za wafu, matambiko , majeneza na makaburi imeandikwa hivi
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
14 Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.
Hosea 13 :14
toka katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
๐Naamuru kila roho za mapepo na majini kuangamizwa kwa damu ya Yesu , ninaamuru kila nira ya magonjwa kutoweka kwenye mwili ,nafsi na roho ya yule baba mama na familia yake katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
27 Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
Isaya 10 :27
Naitwa Pastor Richard
Kutoka Kanisa la Holy Spirit Tanzania
Moto wa Yesu
Morogoro Veta Dakawa
Share
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni