Kuna Watu Wanayonguvu ya kutafuta na Kupata Pesa Lakini Hawana nguvu ya kutumia Pesa yao ikawapa faida. Hii ni roho hatari imekuwa ikitesa Watu Wengi Sana Wapo wengine Wanapata kazi mwaka mmoja Ameshapoteza Kazi Tena. Wengine wamepoteza wachumba wao wengine ndoa zimepotea. Nk.
KUTAFUTA=Ni kujishughulisha na kitu.
KUPOTEZA=Ni kutumia ulichokipata katika mambo ambayo hayana Maana.
Karibu Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kutoka Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania
MISTARI YA KUSIMAMIA TUSOME.
Nehemia:6:16 Isaya:44:12
Muhubiri:3:6
6 wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,
wakati wa kuweka na wakati wa kutupa
Kumb.Torati:15:9
9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia Bwana dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.
KABLA YA KUOMBA FANYA HAYA.
1:Kwanza Uwe na Utayari kuikataa hali ya kupoteza.
2;Ingia uombe hakikisha unatamka Maneno
➖"Natafuta Pesa nitazitumia Sitapoteza Pesa ikae mikononi mwangu kuanzia Leo Katika Jina la Yesu.Amen
➖Nakataa kuwa mtumwa wa kutafuta Pesa halafu hazikai mikononi mwangu Sasa ninaamuru Pesa nitakayoishika kuanzia mwezi huu Katika Jina la Yesu.Amen
➖Roho ya Kupoteza Achia Kazi yangu achia Uchumi wangu achia ndoa yangu achia Katika Jina la Yesu.Amen
➖Baba Yangu Ninaomba kila kifungo kilichounganishwa ndani yangu kinifanye niwe napoteza vitu kiniachie katika Jina la Yesu.Amen
Endelea Kuombea kila mazingira Ambayo umekuwa ukipoteza wapo wengine wanashika mimba zinaharibika Wengine Wamepoteza Afya zao Wapo wengine wachumba wamepoteza hata mawasiliano hakuna Sasa basi Shughulika Bila kuchoka hii roho ikutoke.
UTAJUAJE UMESHAFUNGULIWA.
Hutapoteza Vitu utakuwa unaona faida.
Waliokukopa watakulipa Madeni.
Utashika mimba na haitaharibika
Utafanya kazi Faida utaona.
HITIMISHO
Unajua watu wengi mikono yao imefungwa wanatufuta hawatumii kuleta faida katika kile walichokitafuta.
Basi Tuombe Mungu atufungue roho za kupoteza Tusiwe Tunapoteza.
Tuma ujumbe WhatsApp Uombe kuungwa kwenye group hili la maombi na mafundisho +255759861868
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni