Hakikisha hizi CV unazo kabla ya kuwasilisha Mahitaji Yako mbele Zake.
Unajua Watoto Wa Mungu Wengi na Watu Wengi Hufikiria Mungu Ukimuomba Anajibu tu hazingatii chochote Maana Wajibu Wake Kujibu. Hapana Mungu Hayuko Hivyo Mungu Yupo Makini Sana Kumsikiliza Mwanao Anapomuita Kuliko Eneo lolote Sasa ili Amjibu Katika Maombi Yake huzingatia Yafayo:
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
1:KWANZA WEWE UNAYEMUOMBA AFANYE KITU AU AKUJIBU MAHITAJI YAKO UMEFANYA NINI KWAKE..? YAANI UNAALAMA NGANI UMEFANYA KWA MUNGU?
Swali hili jiulize na ufikirie wewe unaomba Mungu Afanye hiki Wewe mwenyewe mwizi wa zaka hujawahi nunua kanisani hata Tenzi za rohoni hata viti hata kushonea watumishi suti au wajane na Yatima. Mungu Akiutazama huu moyo wa hivi Anaacha Anamtafuta mtu Ambaye hufanya kitu kwake Yeye huyo huwa Mwaminifu kujitoa kwake kusaindia wengine nk.
.
REJEA HIVI VITABU UJIFUNZE KITU.
MATENDO;10...Hii habari ya mtumishi mmoja Mkuu wa majeshi Serikalini yeye na familia yake walivyokuwa watoaji
MATENDO;9:35.....Hii habari Ya Bint mmoja Fundi Cherehani Kipato chake cha chini lakini alikuwa mtoaji.
1Samweli:1 ....Hii Habari Ya Wazazi wake Na Samweli walivyokuwa wakijitoa kwa Bwana.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
2:JAMBO LA PILI MUNGU HUANGALIA NAMNA YA UWASILISHAJI WAKO WA MANENO.
Hatuongei ovyo ovyo Bila mtiririko Tunapoomba mbele Za Mungu Tunapaswa Tutambue Tunaongea na Nani na Maneno Yetu Yanatakiwa Yawe ni Kiwango Kipi cha Hekima na Unyenyekevu na Kujishusha Siyo unaongea naye Huombi mbali unalia tu au Unaenda Kwake Umenuna unaanza kumtupia lawama na kumfokea Kinywa chako kikontoro mtoto wa Mungu Usichukulie kuomba ni rahisi rahisi mpaka ulete majibu.
VITABU REJEA
Soma Habari Ya Hanna alipokuwa Anaomba
1Samweli:1:12-20
Soma hata Mitume Walivyokuwa wakiwasilisha maneno wakiwa wanaomba
Matendo:1:23-26
WAKOLOSAI;2:1-5
1;Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi..
2 Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe
, 3 ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa.
4 Nawaambia mambo haya ili mtu yeyote asiwadanganye kwa maneno ya kuwashawishi.
5 Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.
3:UKAAJI WAKATI UKIWA UNAOMBA MUNGU.
Umekaaje Kaaje Unapokuwa Unaomba Au Wewe unajua kukaa tu. Lazima ujifunze ukaaji wako ukiwa unaomba kaa kwa nidhamu na kwa heshima Sababu unaenda kuzungumza na mwenye umri kukuzidi Elimu kakuzidi Uchumi kakuzidi kila kitu Amekuzidi Kwanini ukose Adabu. Wapo watu wanapoomba ukaaji wao utafikiri hawapo kwenye kuomba Anaomba huku Ameshika hiki mara amekaa ovyo. Kama umepiga magoti piga kwa heshima. Kama ni kusimama simama kwa heshima.
REJEA KUSOMA;
➖➖➖➖➖➖➖
Matendo:20:36-38
DANIEL:6:10
10:Basi Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alikwenda nyumbani kwenye chumba chake cha ghorofani ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Akapiga magoti na kuomba mara tatu kwa siku, akimshukuru Mungu wake kama alivyokuwa akifanya mwanzoni.
HITIMISHO
Acha Niseme Kwamba Ni Muhimu Sana Kujua hili Sababu Unaweza Ukawa Mtu wa Kuomba maombi Yasiyo na Matokeo ikafikia hatua ukaanza kumlaumu Mungu wetu nakuona kama Anaubanguzi Anajibu Wengine kumbe wewe mwenyewe upo nje ya Kanuni Zake Mungu katika Eneo la Maombi.
Kama upo nje ya Group la Maombi na Mafundisho mtumie ujumbe WhatsApp Pastor Richard Akuunge +255759861768
Shirikisha ujumbe huu kwa kuutuma kwa watu wengi zaidi mpaka umfikie Anayependa Kumlaumu Mungu hamjibu.
NAKAMA UNAFANYA HAYA MUNGU HAJAJIBU ELEWA NI LA MUDA LAZIMA AJIBU SABABU UNAALAMA KWAKE UNAFANYA VITU NA KUJITOA KUSAPOT KAZI YAKE HAUFURAHII UKIONA INATUKANWA AU WATUMISHI WAKE WAKILALA NJAA UNAJITOA KUWALISHA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni