Jumapili, 3 Novemba 2024

SOMO:MAOMBI YA KUOMBEA HAJA YA MOYO WAKO

            "DARASA LA MAOMBI "
=============================
SOMO:MAOMBI YA KUOMBEA HAJA YA MOYO WAKO.

Kila mtu huwa Anamatamanio Ya Vitu Anataka Avipate Lakini Hawezi Kuomba Akavipata Sasa Kupitia Darasa hili la Maombi utajifunza uombaje

MUNGU HUZINGATIA 
1;Uwasilishaji wa Maneno.
2;Ukaaji na Uaminifu Wako kwake.
Hakikisha hivi vitu uwe navyo ukitaka unaomba unaleta majibu.

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Tunasimamia Mistari hii.Tusome.
        MITHALI;30;7-8
7 “Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana;
usininyime kabla sijafa:

8 Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo;
usinipe umaskini wala utajiri,
Bali unipe chakula cha kunitosha kila siku

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBA;

1:Omba Kitu Ambacho ukikipata hutamuacha Mungu Sababu kuna Vitu vingine ukivipata tu Wewe Vinakutenga na Mungu.

2;Omba Kataa Umasikini na Kila hali inayofanya Watu Wakudharau.

3:Omba Uwe na Upendo Wa Kiasi kwa Kila Eneo.


NAMNA UTAKAVYOOMBA;

MFANO : 1:UNAOMBA UOLEWE/UOWE.

👉Bwana Wangu Mwokozi Wangu Umenijua toka tumboni mwa mama ukanipima uaminifu wangu kwako katika utoaji wa zaka Na Sadaka Nimekuwa mwaminifu pia hata dhambi ya kuzini nimeishinda Bwana Wewe Mwenyewe Unaona Nilivyosimama Kujitunza Nipate Kibali Machoni Pako Mungu Wangu Niletee Mume Wangu Ubavu wangu au Niletee Mke Wangu Nyama katika mifupa yangu Muda wa Mimi Kuwa na Mwezangu umefika mfungulie Miguu Anifate Katika Jina La Yesu.Amen 

Rudia ×6
ANGALIZO:
Hakikisha Unapoomba uendane na maneno yako uwe kweli zaka umesimama mwaminifu uwe kweli huzini. Mungu huwa hajibu kwa mtu asiyemwaminifu kwake.


MFANO 2; UNATAKA UPATE KAZI.

Baba Yangu Bwana Mwenye nguvu na Mamlaka Nashukuru Kwa Nafasi hii umenipa nione Nami Napendwa nawewe nimeomba kazi Baba Nimeomba Kazi Baba Naomba Jina Langu Lisikosekane Jina langu mimi mwanao Ni Richard Julius Kushoka Ndiyo hivyo nimejaza kwenye usaili Tuma Malaika Wako hili Jina Walipitishe Kila Eneo litapoonekana nami nakuapia Mungu nikipata Kazi Nitakuwa Mwaminifu Sana Tena Sana Kwenye hii Madhabahu Ya Moto Wa Yesu.Amen 

Rudia ×3
ANGALIZO:
Hakikisha Ukipata Kazi Huachi Kutoa Fungu la Kumi Unakuwa Mwaminifu kupita Kawaida.


MFANO;3 KUOMBA UWE NA UZAO YAANI UPATE WATOTO.

👉Shika Tumbo lako Ongea maneno haya kwa mwanamke.

Wewe Tumbo Nakuongelesha uliambiwa nikiolewa tu ulete Uzao Uijaze Dunia ulete Watoto Kwanini mpaka Sasa huna uzao Nakuamru kama kuna anayekuzuia au Amekufunga usinipe watoto nakufungua kwa Jina la Yesu. AMEEN 


👉Mwanaume Shika Kiuno Kama Huzai.

Wewe Kiuno changu Nakuambia kuanzia Sasa ufunguke ukazalishe Mbengu zilizopo ndani yangu zitungishe mimba kila kinachozuia mimi nisiitwe Baba Kiachie Katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×1
ANGALIZO:
Hakikisha unatamka nilivyoelekeza Kwa kila jinsia omba mara kwa mara sio uombe siku moja tu.


MFANO:4 KUOMBA UPATE MTAJI WA BIASHARA 

👉Bwana Yesu Nakuomba uwaruhusu watu uliowadaa wanipe mtaji waje nimechoka kukaa bila kukutolea zaka najiona kama ni mwenye hatia nipe mtaji Baba Uone uaminifu wangu nitakavyosimama kuwa mwaminifu pia unipe na wateja wengi Sana. KATIKA Jina la Yesu Ameen 

        OMBEA WATEJA;
Baba Yangu fungulia Wateja muondoe kwenye mlango pepo anayezuia wateja wasiingie Bwana Weka Malaika wako Awe Anawavuta Wateja Waje waje Waje Kwa Wingi Katika Jina la Yesu.Amen 

ANGALIZO:
Kila uendapo kwenye biashara ombea upate wateja wengi.

MFANO:5 OMBEA MAHITAJI YAKO MBALIMBALI.

Mahitaji yapo mengi Kwa hiyo Ni Vyema Zingatia Uwasilisha wa maneno yako Kwa Mungu unapoomba pia kuwa mwaminifu kwa Mungu acha kuwa mdanganyifu kwa Mungu.

Mfano:Kuomba upone magonjwa;
Baba Yangu Nakuomba niondolee magonjwa mwilini mwangu Baba nitazame mwanao kwa jicho la huruma nipo chini ya miguu yako kwanini unaruhusu magonjwa mwilini mwangu kumbuka nilivyomwaminifu katika madhabahu hii ya Moto wa Yesu sijawahi kuacha kukutolea Zaka na hii ndiyo Madhabahu uliyonipa Bwana Kumbuka nimenunua vyombo vya mziki kanisani nimenunua viti yote hii ni uaminifu na Upendo wangu kwako Baba Kumbuka niliyoyafanya kwako naitaji niendelee Kufanya Nakuomba Uniondolee mateso haya mwilini mwangu Baba nitafanya kwako zaidi ya niliyoyafanya kwako Ansate Mungu umesikia Maombi Yangu Nipe nguvu Sasa kwenye mifupa yangu Mwili wangu nitembee nifanye kazi zangu pasipo na magonjwa nikienda Hospitali wasione tatizo tena nafunga kabisa kwa Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×5

ANGALIZO 
Hakikisha unapoomba uwe kuna vitu unafanya kwa Mungu iwe kama Sababu ya Mungu Akuponye ili uendelee kufanya mengi kwake kama huna Sababu ni ngumu sana kumshawishi Mungu.
Kumbuka Ezekiel alifanya kitu Akaponywa magonjwa.



Natumaini Kuna Jambo umejifunza Naomba ukiwa unaswali niulize inbox WhatsApp number +255759861768

Shirikisha wengine


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni