IJUE BIBLIA - Sehemu ya I
UTANGULIZI
Biblia ni nini?
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyo andikwa na waandishi tofauti-tofauti 40 kwa takribani miaka 1500. Waandishi walikuwa wafalme, wavuvi, makuhani, viongozi wa serikali, wakulima, wachungaji, na madaktari. Biblia ni kitabu cha ajabu! Pamoja na kwamba vitabu vyake vimeandikwa na waandishi wengi tena kwa muda mrefu sana, bado kuna mtiririko na muunganiko wa ajabu kuanzia kitabu cha kwanza hadi cha mwisho. Hivyo basi kwa ujumla wake Biblia imeandikwa na wanadamu chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu wa Mungu
“Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinenayaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” (2 Petro 1: 20, 21)
MGAWANYIKO WA BIBLIA
Utangulizi
Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inaitwa agano la kale lenye jumla ya vitabu 39 na sehemu ya pili inaitwa agano jipya lenye jumla ya vitabu 27. Kisha ikagawanyika katika sehemu nane; nne za agano la kale na nne za agano jipya. Yesu Kristo ndiye mzungumzwaji mkuu katika biblia nzima. Huonekana kama Mwokozi, tumaini la kweli kwa wanadamu wote. Yeye mwenyewe (Yesu Kristo) alishuhudia kuwa ndiye mhusika (mzungumzwaji) mkuu katika agano jipya
- Katika Mathayo 5: 17, 18 alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie.”
- Alipokuwa akitembea na wanafunzi wake kuelekea Emau baada ya kufufuka, Luka 24: 13-31 inasema “ ... Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe...
- Kisha baadaye jioni alipokuwa akizungumza na wanafunzi wake aliwaambia “... hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.”
- Katika Yohana 5:39 na 40, wakati Yesu anazungumza na Wayahudi alisema “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndaniyake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima”
Zaidi sana, katika Ufunuo 19:10 biblia inasema “... kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii” Kwa maneno mengine, asili na kusudi halisi la unabii na maandiko yote ni kumtangaza au kumdhihirisha Yesu Kristo. Anguko na uhitaji wa wokovu kwa mwanadamu, hasa ndivyo vinavyo changia Kisto Yesu kudhihirishwa and kutangazwa kwenye maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya. Kupitia Yesu Kristo tunapata uzima wa milele (Yohana 10:10)
Agano la Kale
Agano la kale lina jumla ya vitabu 39 ambavyo vimegawanyika katika makundi makuu manne kama ifuatavyo:
NO. | MGAWANYIKO WA AGANO LA KALE (A.K) | NO. | VITABU HUSIKA NDANI YA MGAWANYIKO WA A.K |
1. | Vitabu vya Sheria | 1. | Mwanzo |
2. | Kutoka | ||
3. | Mambo ya Walawi | ||
4. | Hesabu | ||
5. | Kumbukumbu la Torati | ||
2. | Vitabu vya Kihistoria | 1. | Joshua |
2. | Waamuzi | ||
3. | Ruthu | ||
4. | 1 Samweli | ||
5. | 2 Samweli | ||
6. | 1 Wafalme | ||
7. | 2 Wafalme | ||
8. | 1 Mambo ya Nyakati | ||
9. | 2 Mambo ya Nyakati | ||
10. | Ezra | ||
11. | Nehemia | ||
12. | Esta | ||
3. | Vitabu vya Kiushairi | 1. | Ayubu |
2. | Zaburi | ||
3. | Mithali | ||
4. | Muhubiri | ||
4. | Vitabu vya Manabii | ||
a) Vitabu vya Manabii Wakubwa | 1. | Isaya | |
2. | Yeremia | ||
3. | Ezekiel | ||
4. | Danieli | ||
b) Vitabu vya Manabii Wadogo | 1. | Hosea | |
2. | Yoeli | ||
3. | Amosi | ||
4. | Obadia | ||
5. | Yona | ||
6. | Mika | ||
7. | Nahumu | ||
8. | Habakuki | ||
9. | Zefania | ||
10. | Hagai | ||
11. | Zekaria | ||
12. | Malaki | ||
Agano la Jipya
Agano jipya lina jumla ya vitabu 27 ambavyo vimegawanyika katika makundi makuu manne kama ifuatavyo:
NO. | MGAWANYIKO WA AGANO LA JIPYA (A.J) | NO. | VITABU HUSIKA NDANI YA MGAWANYIKO WA A.J |
1. | Vitabu vya Kihistoria | 1. | Mathayo |
2. | Marko | ||
3. | Luka | ||
4. | Yohana | ||
5. | Matendo Ya Mitume | ||
2. | Nyaraka za Mtume Paulo | 1. | Warumi |
2. | 1 Wakorintho | ||
3. | 2 Wakorintho | ||
4. | Wagalatia | ||
5. | Waefeso | ||
6. | Wafilipi | ||
7. | Wakolosai | ||
8. | 1 Wathesalonike | ||
9. | 2 Wathesalonike | ||
10. | 1 Timotheo | ||
11. | 2 Timotheo | ||
12. | Tito | ||
13. | Filemoni | ||
3. | Nyaraka za Jumla (kwa watu wote) | 1. | Waebrania |
2. | Yakobo | ||
3. | 1 Petro | ||
4. | 2 Petro | ||
5. | 1 Yohana | ||
6. | 2 Yohana | ||
7. | 3 Yohana | ||
8. | Yuda | ||
4. | Kitabu cha Unabii | 1. | Ufunuo wa Yohana |
Endelea kufuatilia somo linalofuata kwa uchambuzi wa kina. Share kwenye mitandao ya kijamii ili watu wapete nafasi ya kujifunza kama wewe ulivyojifunza.
Machapisho maarufu kutoka blogu hii
MAANA YA WOKOVU
WOKOVU NI NINI? Kuokoka si lugha mpya masikioni kwako msomaji! Mara nyingi umesikia kwa watu mbalimbli na katika maeneo tofautitofauti kuwa mtu fulani “ amenusurika na janga la moto” au “ ameokolewa kwenye moto” au “jeshi la nchi fulani limekomboa mateka wake” au “ mtu amepona kwenye ajali mbaya”. Yote haya yanaelezea hali ya kunusurika au kuokoka kutoka kwenye hali hatarishi au kwenye mateso makali. Hii ndio hasa maana ya kuokoka Nini maana ya wokovu? Kuokoka ni kunusurika, kusalimika, kukombolewa, kufunguliwa au kupona kutoka katika janga au hatari fulani. Ili kuelewa hasa maana ya wokovu kibiblia, yakupasa kujua yafuatayo:
HIVI NDIVYO MTU ANAVYOOKOKA
Biblia husema ... “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka . Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. ” [Warumi 10: 9,10] Ili mtu aokoke alizima... 1. Kuamini moyoni kuwa Mungu alimfufua Yesu katika wafu. Hii ina maana ya kuamini kazi nzima ya ukombozi wa mwanadamu ambayo Yesu Kristo aliikamilisha baada ya kufa msalabani na kufufuka siku ya tatu. Unapofika mahali pa kuyaangalia maisha yako na kuona kweli unamhitaji Yesu, basi hapo unapaswa kwanza kuamini kuwa Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako ili upate msamaha wa dhambi.
Maoni