Jumanne, 1 Oktoba 2024

MAOMBI YA USIKU WA MANANE MWEZI OCTOBER '------DECEMBER 2024

SOMO: MAOMBI YA USIKU WA MANANE OCTOBER____DECEMBER 2024

Karibu Katika Msimu WA  Mwisho WA Maombi Ya Usiku Wa Manane Kwa Mwaka 2024 Ambao Ni Mwaka Wa Kusitawi 
Mwanzo 26;13

TUMEONA SHUHUDA WATU WENYE MIAKA 52 WANAOLEWA KUPITIA MAOMBI YA USIKU WA MANANE 

TUMEONA WASIO NAKAZI WANAPATA KAZI

TUMEONA WATU WENYE MIAKA 48 WANAZAA

TUMEONA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI WANAFUNGULIWA KATIKA MSIMU ULIOPITA.


MAOMBI YA USIKU WA MANANE PEKEE YANAWEZA KUKUFUNGUA VIFUNGO VYAKO

AMKA SAA SABA USIKU OMBA MPAKA SAA TISA PUMZIKA


NAMNA TUTAKAVYOOMBA.

Soma Mistari 

👇👇👇👇👇👇

1:●ANZA NA TOBA.

Zaburi;86:5  2Nyakati:7:14-16

Piga magoti mbele ya kitanda

"Baba Nakuja mbele Zako mimi mwanao Richard Nimekukosea mengi kuanzia January mpaka Sasa nimezini kimawazo nimeimba kimawazo nimeshindwa kutii maangizo ya Baba yangu wa Kiroho nimekuwa ni mwizi Na ninajiona Kabisa mambo hayaendi lakini nakuja kugundua ni sababu ya wizi wa zaka Malaki;3;8-9 Nisamehe  Nisamehe Bwana Nisamehe Bwana ninatubu maovu yangu na Dhambi Zangu Katika Jina la Yesu.Amen 🤲🤲


2;●KUKIRI USHINDI KWA KUTUMIA NENO 
.mfano huu kama ninavyoonesha.

Kuna Wakati Kiri Ushindi Siyo Kukiri mapepo au kusikiliza Sauti Za Mapepo roho za kushindwa.

1;Sitaki kutumikia Vifungo au Magonjwa mimi "Nataka Nimtumikie Bwana" Kutoka:23;25


2;Sitaki Kuitwa Tasa mimi au Kuharibu mimba "Nataka Nizae watoto siyo mtoto".
Kutoka:23:26

3;Sitaongopa Adui Zangu" Kuanzia Leo nitakuwa na Utisho Mkubwa Kila Adui yangu Ataniongopa" Kutoka;23:27

4:Sitaongopa kwa kuwa "Bwana ni ngome yangu atawarundishia mabaya yao"
Zaburi;94:22-23

5:Sitaacha Kutoa zaka" Nitakuwa mwaminifu kwa Bwana ili Anibariki umasikini siutaki"
Kumb.Torati:28:1

6:Sitaumwa Tena Maana "Mungu Amenirundishia Afya Yangu"
Yeremia:30:17

7:Sitaki Kuwa mnyonge tena "Nakata Unyonge Ndani Yangu Kuanzia Leo"
Wafilipi:3:21 Zaburi:136:23


HAKIKISHA UNASOMA HIYO MISTARI YA BIBLIA NA KUITAFAKARI.


3●JITABIRIE BARAKA MWENYEWE.

1;Mwezi huu Mimi nitaolewa na nitatolewa mahali au mwezi huu mimi nitaowa na nitafunga ndoa kabisa.



2;Maombi ya kazi niliyotuma naenda kupata kazi majina yakirundi na langu lipo 


3:Mkuu Wangu Atanipandisha cheo na mshahara wangu utapanda juu niweze kutia Zaka nzuri.

4;Nitajenga mwezi huu nitashusha tofali kwenye kiwanja changu au nitanunua kiwanja mwezi huu.

5;Mimi na Mchumba wangu Tutaowana mwaka huu


Endelea kujitabiria MWENYEWE kama mfano huu nilivyokuanzishia



4●SHUKURU MUNGU AMEJIBU.

Nyosha mikono juu Inuka simama piga makofi mara nyingi Sema Nashukuru Mungu kwa Kujibu ombi langu Nashukuru Nashukuru Nashukuru Mungu Sana Pokea Sifa na Utukufu wako Katika Jina la Yesu.Amen 

5:●FUNIKA MAOMBI YAKO KWA DAMU YA YESU

Nayafunika maombi Yangu Kwa Damu Ya Yesu Nakuomba Bwana Uyazungukie kwa ulizi wako Katika Jina la Yesu Ameen 


BAADA YA KUMALIZA FUNGUA AUDIO  YA MAOMBI NILIYOTUMA UGANISHA NA RADIO SAFIRI NAMI KATIKA MAOMBI 

Huu Utaratibu Tunaenda nao Mpaka December Tutaanza Kujiandaa nauli ya kutufikisha Morogoro Veta Dakawa Kuja kufunga mwaka Pamoja Tar 30 Tunaingia Makao makuu kuja kufunga mwaka huu wa kustawi 2024 Nakuingia Mwaka tutakaopewa Jina. Uje na Sadaka yako ya kufunga mwaka Tunakuwanga na Maombi moto moto Sana Usikose.

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Askofu mkuu wa makanisa ya Holy Spirit church Tanzania 

Simu +255759861768

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni