Jumanne, 25 Machi 2025

NDOTO ZA SHULENI

NDOTO  ZA SHULENI NA MAANA ZAKE.

Karibuni Sana LEO Tuone Ndoto za Kuota Shuleni Na Maana Zake.

Ndoto huwa ni Taarifa Unayojulishwa jambo linalokuja au lilopita au lilopo

Ayubu;33:14-15 

1:Ukiota Upo mazingira ya shule ya msingi na Unifom

👉👉Unajulishwa Umefungwa Usifanikiwe waitajika uombe kukemea hiyo roho.


2:Ukiota Upo shuleni unamwagilia mimea

👉👉Unajulishwa Watu Utakuwa unawafanyia kazi wezako wanafanikiwa kwa ulicho nacho wewe hutafanikiwa.


3;Ukiota Upo Palendi(Mstarini

👉👉Unajulishwa umeuganishwa na roho ya Kusimama katika hatua zako zisisonge mbele uombe uikatae hiyo roho.


4:Ukiota Upo Unacheza na Wanafunzi wezako shuleni

👉👉Unajulishwa Utateseka kwa Kuwa mpuuziaji wa vitu katika maisha yako.


5:Ukiota Upo shuleni Mwalimu anafundisha wewe huna daftari au Kalamu

👉👉 Unajulishwa Huwezi Kuweka Kumbukumbu Ya Vitu unavyoelekezwa au Kushauriwa ndiyo sababu hufanikiwi


6:Ukiota Unalia Upo maeneo ya shuleni

👉👉 Unajulishwa Unauchungu Kwakuwa Mambo hayaendi mbele kama utakavyo


7:Ukiota Upo shuleni mnafanya Mtihani wezako wanakusanya wewe Upo TU 

👉👉Unajulishwa Huwezi kutatua changamoto unazopitia mpaka usaidiwe ndio utavuka kataa hiyo roho.


8: Ukiota Upo Kwenye chumba Cha Mtihani hujagawiwa Karatasi Wezako wamegawiwa

👉👉Unajulishwa Karibuni Utakutana na changamoto kabla haijakukuta Omba Kemea


9:Ukiota Upo Darasani unafundishwa somo la Hisabati

👉👉Unajulishwa Huwezi kufanikiwa Sababu huna malengo wala mikakati.


10:Ukiota Upo Darasani mnapiga Kelele Mwalimu anaingia

👉👉Unajulishwa wewe unamaneno mengi SI mtendaji wa unachokiongea ndiyo maana huendelei. Omba kemea ndoto hiyo.


11:Ukiota Upo Shule ya O,level

 👉👉Unajulishwa Unamwaga wa Kufanikiwa lakini Waitaji mtu mwenye hekima akuongoze kufikia mafanikio yako


12;Ukiota Upo High School mpaka chuo

👉👉Unajulishwa Unamafanikio lakini jishughulishe na kitu Mungu atakibariki.


13: Ukiota Upo unasoma na Wanafunzi wa chuo lakini wewe hujawahi Kufika au Kusoma chuo

👉👉Unajulishwa Mafanikio yako yaitaji ukae na watu waliokuwa kiroho na kielemu utafanikiwa


14: Ukiota Upo shuleni unakula

👉👉Unajulishwa matatizo yako Yanayokutesa uliyapata ukiwa shuleni.


15;Ukiota Upo shuleni lakini maeneo ya chooni au Bafuni Ndoto ikaja hivyo

👉👉Unajulishwa Ulikanyaga Dawa ukiwa shuleni Mungu Akakukinga nazo hazijakuzuru lakini Waitaji uombee kukemea roho hizo.


16:Ukiota Upo Darasani unawafundisha wezako Mwalimu nae amekaa

👉👉Unajulishwa Utafanikiwa Kile ufanyacho Kupitia kuwasaidia watu wegine.


17:Ukiota Upo O,olevo au High school Unafundishwa na Mwalimu Wa chuo

👉👉Unajulishwa Upo unakwama kusonga mbele Kwakuwa unaitajika ukae na mtu aliyekuwa kiroho au aliyefanikiwa Kimwili ndipo utatoka kwenye pito Hilo.


18:Ukiota Upo shuleni umevaa nguo za nyumbani

👉👉Unajulishwa Unapenda Kujifunza na Kutafuta mafanikio lakini Tabia hubadiliki Unapaswa ubadilike Tabia yako Utafanikiwa


19:Ukiota wewe Ni Mwalimu Upo unafundisha shuleni kwako

👉👉Unajulishwa roho ya kutumikishwa hutaendelea kwa Kuwa unatumikishwa kila utakalokufanya. Uombe kemea


20:Ukiota wewe Mwalimu umeitwa na mkuu wako akakufokea

👉👉Unajulishwa utaitwa na mkuu wako atakuonya 


NDOTO ZA SHULENI WALIZOOTA WATU ZA MASHULENI


1:Bwana Yesu asifiwe baba.Naitwa Happy Nipo Njombe Samahani naomba kujua maana ya hii ndoto nimeota usiku wa kuamkia Leo. Nimeota tulikuwa kwenye shule ya msingi niliyosoma tulikuwa Mimi na rafiki yangu, tumeenda kufundisha darasa la kwanza lakini tulipofika darasani tukamkuta mwalimu mwingine anafundisha na zilikuwa zimebaki dakika kumi na Tano tu muda wa mapumziko ufike basi tukawa tunaondoka. Lakini wakati tunaondoka tukapita nyuma ya majengo ya shule tukawa tunaona Kuna uchafu mwingi karibu kila sehemu tuliyopita kulikuwa na kinyesi Cha binadamu. Je hii ndoto Ina maana gani baba?? Inaninyima raha kabisa.


MAANA YAKE

Unajulishwa unarundishwa nyuma kiroho na hatua za maisha yako kupitia kukosa marafiki sahihi.


Tengeneza list ya watu unaoongozana nao Muombe Mungu akupe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni