Mungu alimuumba mke na mme ili Waishi Pamoja na Wakazaene ili Kuongeza Uzao na Kuifanya Dunia iendelee. Hii Haimanishi Mungu Ndiyo Anamlazimisha mtu kuowa au kuolewa.
Ndoa Ya Kikristo ni Ya mke Mmoja na Mme Mmoja Imani moja.
MPANGO WA MUNGU JUU YA NDOA.
Mpango wa Mungu ni kwamba mume mmoja na mke mmoja waishi
pamoja wakati wote bila Kuachana
1:WASAIDIANE:
Mwanamke Awe msaidizi Katika maisha Yao .
Mungu alipomuumba mwanamke awe ‘msaidizi wa kufanana’ na
mume (Mwanzo 2:18), alitaka wasaidiane kwa kila mmoja
kumjali mwenzake kwa kila hali; kiroho, kimwili na kifikra.
2:WAWE WAMOJA.
Mungu Anataka Kuona Wanakuwa Waaminifu Kwenye ndoa Zao.
Mungu aliposema ya kuwa wawe ‘mwili mmoja’ (Mwanzo 2:24),
alionesha kuwa walipaswa wawe wamoja, mmoja kwa mwingine:
waaminifu, wanaoelekeana, wakweli na wanaotegemeana wakati
wote.
3:WAZAE WATOTO WAKIKE NA WAKIUME
Huu mpango wa Mungu Kuona Mwanamke anazaa na Mwanaume anazalisha ndio Maana Ya Kuwaumba Mwanamke na Mwanaume
Mungu alipowabariki Adamu na Hawa na kuwaagiza wazae na
kuongezeka (Mwanzo 1:28) alikuwa akionesha kuwa, ndoa iliyo
imara inatoa fursa nzuri ya watoto kukulia ndani yake.
NDOA: Inakamilishwa na Familia Yaani Watoto wakike na Wakiume wawe ndani ya Ndoa hiyo wakifurahia na kurukaruka.
KUHUSU KUJAMILIANA KABLA NDOA.
Mungu Tendo la Kujamiliana aliliweka Yeye ili Kuendeleza Kizazi alichokiumba lakini Utofauti
Ni Kulifanya nje ya Utaratibu Wa Makumbaliano ya Patano la ndoa. Nje ya ndoa unakuwa umevunja Sheria aliyoiweka.
1Wakoritho;6;9-10
KUTAFUTA MUME AU MKE KWA MKRISTO
===========================℅[[[[[[[[[[[
2Wakoritho:6:14
¶=Lazima Mkristo aolewe na Mkristo Mwezake Mungu anamtaka Kijana wa Kikristo na Bint wa Kikristo Anamtaka Atafute Wa Imani yake Yaani Mkristo mwezako.
¶=Kujua ni Sahihi Uliyempata Utasikia Amani ya moyo na Furaha Uwepo wake hiyo Ndiyo Dalili Kuu inakujulisha Umepata mtu Wa kutoka kwa Mungu.
KUHUSU WA JANE NA WAGANE
1Wakoritho;7;39
Mungu anawapa ruhusa ya kuolewa Kama wakiitaji Kutengeneza Familia tena. Wasikae bila kuolewa kushinda dhambi ya Uzinifu.
Mwanamke hufungwa na Mwanaume Akiwa Yupo Hai lakini Akira Yupo guru kuolewa.
HITIMISHO.
Masomo haya Yanaletwa na Pastor Richard Kwa Msaada Wa Roho Mtakatifu Kuhakikisha Yanakuvusha Sehemu na Unaenda Sehemu Kwa hiyo ni Vyema Kujifunza ili kuijenga ndoa Yako vizuri.
Share hili Somo kwa Rafiki mmoja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni