Ndoa ni tendo ambalo Mungu aliliumba kwa makusudi kabisa, ili kumpa mwanadamu picha ya jinsi ndoa yake halisi itakavyokuwa kati ya yeye na watu wake, baada ya ulimwengu huu kuisha.
Uhusiano walio nao mke na mume, ni mfano mdogo sana wa uhusiano atakaokuwa nao Mungu na watu wake watakaoshinda, katika mbingu mpya na nchi mpya.
Hivyo tutaitazama mistari michache ihusuyo ndoa za kibinadamu, na vilevile tutaitazama mistari michache ihusuyo ndoa ya ki-mbinguni(yaani Kristo na kanisa lake).
NDOA YA MKE NA MUME
Mwanzo 2:24 “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”
⌚⌚⌚π₯π₯π₯ππππ
2;MWANAUME AMPENDE MKE WAKE
Waefeso 5:25 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake”;
π₯π₯π₯πππππ₯π₯π₯π₯
Waefeso 5:33 “Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe”π₯
3;MWANAUME MFURAHIE MKEO⌚ππππ₯π₯π₯
Mithali 5:18 “…. Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako”
4;MCHUKULIANE YOTEπ₯π₯π₯π₯⌚⌚⌚
Waefeso 4:2 “kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; 3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani”.
5;MUUGANIKO WENU UDUMUπ₯π₯π₯⌚⌚⌚⌚
Marko 10:9 “Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe”
6:IWE MUHURI MOYONI KUWA UNAMKE NA UNAMKE.
Wimbo 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.
7 Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa”.
7;MLIHESHIMU AGANO LA NDOA.
Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.
8:MTEMBEE MWENDO WA MSHIKAMANO.
Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.
19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana”.
9;MKE MWEMA ANATABIA NJEMA.
Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani”.
10:MNYANYUANE PALE MNAPOAGUKA KIMAISHA SIYO MKIBIANE.
Mhubiri 4:9 “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto”?
11:PASIWEPO NA UBINAFSI.
Mathayo 19:6 “Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”
12;TUMIENI AKILI VYEMA
1Petro 3:7 “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe”
13;HAKUNA KUACHANA.
Malaki 2:16 “Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli…”
14;POPOTE ATAKAPOISHI MMEO NAWEWE UWEPO. Muabatane wote.
Ruthu 1:16 “Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami”
.
15;MPENDANE MSICHOKANE.
Yohana 13:34 “Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo”.
1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya”;
16;MSITENDEANE MAMBO YA KUUMIZANA.
Malaki 2:14 “Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
15 Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni