Alhamisi, 6 Novemba 2025

MFUNGO WA SIKU 30

MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU 30 Tumeanza Tar. 1 Tayari Tunaendelea 

Tunaoweza Tu jiugamanishe na Huu Mfungu siku ya 30 Tutatoa Sadaka Ya Mfungo. 

Tunafunga Masaa 12 

Tunaombea Mahitaji Yetu mbalimbali Tunaombea Taifa Letu na Serial take na Uongozi Wote Tunamuombea Baba Yetu Wa Kiroho Pastor Richard 

Maombi haya Ya siku 30 Tumeyagawanya hivi. 


➖ASUBUHI SAA;11:40-12:30 Tunaombea hayo mahitaji

➖MCHANA SAA:6:30-7:30 MCHANA Tutaombea haya mahitaji

➖JIONI SAA:10:00-12:00 JIONI

Tutaombea hayo mahitaji


Mashart Ya Mfungo huu. 

1;Kaa Patulivu na Usikwazane na watu. 

2:Epuka makwazo

3:Usizini au Kufanya matukio yatakayoharibu Mfungo wako. 

4:Unaruhusiwa Ku Jiconect na Maombi ya hapa madhabahuni Moto Wa Yesu kupitia Sadaka Yako unanitumia inbox mahitaji Yako. 

Pia nitakuwa na post audio za Maombi


Rejea Vitabu hivi kabla ya kuomba

ZABURI. 126:5-6
“Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.  Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda.


 Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”



ZABURI. 124:1-3, 6-8


“Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,  Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia.    Papo hapo wangalitumeza hai, 

Hasira yao ilipowaka juu yetu  Na ahimidiwe BWANA; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.  


Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.    

Msaada wetu u katika jina la BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.”

2. Tumkabidhi Mungu mipango yetu ili aweze kuithibitisha na kuifanikisha sawsawa na mapenzi yake.


MITHALI:16:1, 3


1“Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.  Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.”

3. Katika mambo yote tunahitaji neema na rehema za Mungu.


WAEBRANIA. 4:16


16“Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.”






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni