Karibuni Tena Mwendelezo Wa Somo letu hili la MALAIKA SABA WASIMAMAO MBELE ZA MUNGU. Ufunuo;8;2-4.
Admin; Bishop Richard Tz
Group la Maombi na Mafundisho
WhatsApp +255710889892
Join ujipatie masomo mbalimbali
Tumetoka kujifunza Malaika wanne
URIELI MALAIKA WA WOKOVU NA UJUZI
RAPHAEL MALAIKA WA AFYA NA UPONYAJI
METATRONI MALAIKA WA WATOTO
NA MIKAEL MALAIKA WA ULINZI NA USALAMA(Hushughulika na Vita vita)
LEO TUNAENDELEA......
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Ninakuletea Somo hili litakusaindia kujua namna ya kuwatumia Malaika Hawa.
LEO TUNAENDA KUMUONA MALAIKA WA TANO ASIMAMAE MBELE ZA BWANA.
MALAIKA MKUU RAGUEL Ndiyo Jina lake huyu ni Malaika Mkuu Wa MOTO.
Huyu Malaika Amefanya kazi na Musa
Kutoka:3:3-5 Alitokea kwa umbo la kijiti
Huyu Amefanya kazi na Elia ukisoma 1wafalme 18: Alishuka akalamba Sadaka na maji
Ufunuo 20:9 Anaoneshwa hapa akishuka kuwateketeza waovu.
Huyu alifanya kazi na Sulemani Ndani ya hekalu la Sulemani Rejea 2Nyakati;7:1
Ndiye huyu alimtenganisha Eliya na Elisha alionekana kama Gari la Moto Rejea 2WAFALME:2:10-13
KAZI ZAKE HUYU MALAIKA RAGUEL.
1;Husimamia na Kuteketeza Waovu kwa Moto.
2;Humdhihirisha Mungu kwa umbo la Moto mfano shadrack na Abnego kwenye Tanuru huyu Malaika alikuwa nao.
3;Hutokea Kwa umbo la Moto kwa muonekano mbalimbali kuligana na Vita ilivyo.
4:Husimamia watu wanaotupwa kwenye ziwa la Moto huyu Malaika huwachukua kuwatupa kule kila hukumu ikisomwa.
5:Huagamiza Miungu Huharibu Madhabahu za Shetani kwa Kuzichoma moto.
6:Yeye ni Malaika Anayeshambulia na kutetea watoto wa Mungu walio katika kipindi cha kuteswa na falme za ngiza.
NAMNA YA KUMTUMIA MALAIKA MKUU RAGUEL.
1:Naangiza Malaika Mkuu Raguel Ashuke Ashuke Akaharibu Kila madhabahu za nyumbani kwetu Ashuke na Moto wake Akaunguze Akachome Akachome katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×4
2;Moto Moto Ushuke Kutoka Mbiguni Uwateketeze Kila watesi wangu kila wanaozuia maisha yangu yasibadilike Moto moto wa Malaika Mkuu Raguel ashushe Ashushe Uokoe katika Jina la Yesu.Amen
Rudia× 4
3:Nilipo hapa hapa Nataka Leo Nimuone Raguel Malaika Mkuu Wa Moto Anashusha Moto Anaharibu Ufalme wa shetani na Wachawi wote wa mtaa huu Raguel Shuka Uwapinge Uwapinge Kwa Moto moto moto katka Jina la Yesu.Amen
Rudia ×5
4:Majeshi ya kikosi cha Moto wakiongozwa na Malaika mkuu Raguel Washuke waje wazunguke zunguke kwenye nyumba yangu katika Jina la Yesu.Amen
Rudia ×7
HITIMISHO
Tunapaswa kuwajua Malaika na Tuwatumie katika Vita vyetu waje watusaindie Tumia Malaika.
Nikuombe Share masomo haya yaliyokuja na nguvu ya kufungua watu kupitia Malaika wakuu wasimamao mbele za Bwana.
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
Makao Makuu Morogoro
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni