Ijumaa, 4 Julai 2025

SOMO: MALAIKA WA SABA RAMIEL

SOMO: MALAIKA  MKUU RAMIEL

Karibu Tu jifunze Leo MALAIKA MKUU RAMIEL huyu ndiye  MALAIKA MKUU WA SABA. 
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

MALAIKA MKUU RAMIEL ni malaika wa kufufua na kurejesha vitu Katika Hali ya Upya huyu hushughulika na ufufuo wa vitu vilivyokufa kabisa

VITABU REJEA:-EZEKIEL;37  Yo te na VITABU hivi chini

ALIFANYA KAZI NA ELIYA

1 Wafalme 17:21-22
21: Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena.

22: Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.

ALIFANYA KAZI NA BWANA YESU. 

Mathayo 28:5-6 
  5:Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.

6; Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.

ANAFANYA KAZI NA SISI

Wakolosai 3:1-2 
2 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Matendo ya Mitume 4:8-11 
 8:Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,

9: Kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa. 

 10:Jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.

 11:Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.


KAZI ZAKE HUYU MALAIKA RAMIEL. 

1:Kufufua Mambo Yetu Yaliyokufa. 

2:Kurejesha Vitu vilivyopotea. 

3:Kuwa na nguvu ya kufanya Mambo Yetu yawe hai. 

4:Kuyauganisha Yaliyotawanyika au kutapanywa kuvikusanya vitu kuwa pamoja. 

5:Anamsaidia MTU Mambo yake yawe na matokeo chanya.

Anazo KAZI nyingi Kwetu Sana huyu Ramiel ukiona Mambo yako yanakufakufa muite huyu


       NAMNA YA KUMUOMBA. 

1:Baba Yangu Uliye mbinguni Muangizie Malaika Mkuu Ramiel Aje Afufue Mahusiano Yangu UCHUMBA wangu Mimi.... Na... Katika Jina LA Yesu. Ameen
Rudia ×3

2:Malaika MKUU RAMIEL Nayatabiria Maisha Yangu yawe na nguvu ya uhai hayataishi ndani ya mifupa mikavu iwe kazi zangu ndoa yangu biashara zangu nk Katika Jina LA Yesu. Ameen

3:Baba Fufua Mikono yangu Ikawe na nguvu ya Biashara kuzitawala Biashara na kuziendesha Katika Jina LA Yesu. 🙏Amen

TUFANYE NINI

MALAIKA MKUU RAMIEL yupo na atakuwa miongoni mwa MALAIKA WAKUU SABA ATAKUJA NA WEZAKE. 

TUMTUMIE HUYU MALAIKA Kufufua KAZI ZETU MAISHA YETU. 

Wito

Tumia WhatsApp hii ukiwa unaswali au unataka uokoke +255710889892

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni