Jumamosi, 19 Julai 2025

SOMO:NIFANYE NINI NIFIKE MBINGUNI

SOMO: NIFANYE NINI NIFIKE MBINGUNI. 
YEREMIA;10:13_17 Mwanzo: Sura ya 7 Na 8 Mwanzo:27:28, 39 Kumb. Torati:14:35

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
Morogoro Veta Dakawa
Karibuni Watoto Wa Mungu Tu jifunze Tunafanyaje nini nifike Mbinguni au Tupate Kigali na Sisi Kwa Mungu Sababu hatuwezi kumfurahisha Mungu Endapo Swali ndogo kama hili Tutasema Tufanye mema tu ndiyo Tufike Mbinguni Lazima Tujue Kuna visababishi vyakutufanya Tufanye Vizuri Na Tupate kukubalika katika Mbingu. 

Mbinguni ni Makao Ya Mungu Wetu hapa chini ni Sehemu ya kuwekea Miguu Yake. 

Tunaposema "MUNGU" Ni Roho lakini  kazi zake anazifanya Kimwili na kiroho

Mwanzo 1:2 
 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

KUNA MAMBO HAYA YAFANYE ILI  UFIKE MBINGUNI

1;MPENDE MUNGU WAKO. 
Vitabu:Kumb.Torati.6:5 Luka. 10:27

Kumpenda Mungu huhusisha maeneo Manne ya mwili wako. 

1:Nafsi Yako mepende Mungu kuliko dunia

2:Moyo wako mpende Mungu kuliko dunia

3:Akili Yako Mpende Mungu kuliko dunia

4:Nguvu zako Mpende Mungu Kuliko vyote.

5:Roho yako Mpende Mungu kuliko dunia. 

Anasema Yesu  HAYA LUKA;10:27 

Paulo Mtume Katika Warumi Anasema Faida Ya MTU Akimpenda Mungu Hataipendeza Dunia Atafanya kwa kumpendaza Mungu. 

    Warumi 8:8 
 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

      Warumi 12:2 
 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Huwezi Kusema Unampenda Mungu Akili yako haipo pamoja na Mungu au moyo wako haupo kwake au nafsi yako. 


2:MANENO YA MUNGU NA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU YAISHI NDANI YAKO. 

Rejea Haya Maandiko
       1 Timotheo 4:16 
  Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.

Yoshua 1:8
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Ayubu 22:21
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.


MAMBO HAYA YA TAKUWA  KWAKO. 

1:Kuwa Karibu na Mungu. 

2:Njia yako ya maisha kuwa namwelekeo. 

3:Kusikia Maelekezo na yakupasayo ufanye kutoka kwa Mungu moja kwa moja. 

4:Amani na ushindi kwa Adui zako. 

5:Utaongezeka Kiroho nakusimama imara na Mungu. 


3;JITOE KWA MUNGU. 

Matendo;10:1_5

Warumi 6:13
wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.


HAYA YAPO UNAPOJITOA. 

1:Kazi Ya Mungu Itasonga mbele

2;Utahubiri injili kupitia kile ulichokitoa

3:Utabarikiwa mjini na vijijini

4:Mateso na vifungo vitaondoka

5:Mambo Mengi hubadilishwa na baraka mbalimbali zipo kwenye utoaji. 


HAYA NILIYOYAFUNDISHA ndiyo Tiketi ya kwenda Mbinguni kama unataka kufika Mbinguni anza kujifunza Kumpenda MUNGU akilini mwako kwenye moyo wako 


Wapo watu wapo tayari Asiifanye injili iende mbele lakini aende kwa mchumba azini naye na amjegee nyumba au gari amnunulie Hakikisha Unapoweka Alama Ya Kupapenda ndipo hata ukifa moyo wako utatulia hapo ndiyo maana Huwa nasema fundisha moyo wako kuwa mwaminifu Wa zaka Wapo watu akili zao wamezifundisha zikikutana na changamoto kidogo zimuache Mungu na ziache kutoa zaka anaanza kuyafanya yake Mungu anabaki naye mdomoni tu. 


Ndugu yangu Jifunze Akili moyo wako kuiamuru Impende Mungu HAYA yanayokupa kiburi yataishia duniani Ipende kazi ya Mungu. 



Wito

Kama SOMO limekuponya Nifate inbox WhatsApp+255710889892

Niulize Swali nitakujibu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni