Swali: Je shetani yule audanganyaye ulimwengu alitoka wapi?
Jibu: shetani kwa asili aliumbwa na Mungu, na kabla ya kuwa shetani alikuwa akiitwa “Kerubi afunikaye”
Ezekieli 28:14 ” Wewe ulikuwa KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA AFUNIKAYE; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto”.
Na MUNGU alimwumba akiwa mkamilifu (asiye na dosari) kama tu MAKERUBI wengine, lakini baadaye moyo wake uliinuka akajidanganya mwenyewe kuwa anaweza kuwa kama MUNGU (aabudiwe kama MUNGU) Na ndipo Uovu huo ukaonekana ndani yake, na hakutaka kubadilika.
Ezekieli 28:15 “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”
Na baadaye alipoasi ndipo akawa shetani, na maana ya shetani ni Mshitaki/Mchongezi, maana yake anawashitaki wanadamu mbele za MUNGU mchana na usiku.
Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU”.
Swali la 2
SWALI LA PILI
. Tukio la Yesu kupaa kwenda mbinguni lilitukia eneo gani?. N.b weka andiko ku sapoti jibu lako
JIBU: Mlima wa mzeituni. Matendo ya Mitume 1:12 [12]Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.
Mlima wa mizeituni..ambayo inapatika kati eneo la Bethania
Luka 24:50-51 [50]Akawaongoza *mpaka Bethania*, akainua mikono yake akawabariki. [51]Ikawa katika kuwabariki, *alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni*
Swali la 3
Swali: Tunasoma Simeoni alipomwona mtoto YESU, Alikiri kuuona Wokovu wa MUNGU, sasa swali ni Wokovu gani huo alioupata?
Jibu: Tuanzie ule mstari wa 25 ili tuweze kuelewa vyema…
Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.
26 Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
27 Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
28 yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
29 Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;
30 KWA KUWA MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU WAKO,
31 Uliouweka tayari machoni pa watu wote;
32 Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli”
Sasa hapo hajasema AMEUPATA WOKOVU..La! bali anasema “MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU”.. kuuona wokovu na kuupata wokovu ni vitu viwili tofauti…
Wokovu wa Mungu unapatikana kupitia mmoja tu, naye ni YESU KRISTO (Matendo 4:12),..Baada ya YESU kusulibiwa ndipo watu wakaanza kuupata wokovu, lakini kabla ya hapo waliusikia na kuuona tu,…waliousikia ni manabii wa kale na watu wote wa agano la kale, na waliouona ni watu waliokuwepo kipindi BWANA YESU anazaliwa, na walioupata ni wote waliomwamini baada ya kufufuka kw
Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?
Swali: Biblia imeandikwa na watu, (kama Paulo, Petro, Musa, Daudi na wengineo) je tutaamini vipi kitu kilichoandikwa na wanadamu kuwa ni kweli,? vipi kama wametoa tu kwenye akili zao, kwanini tukiamini kitabu cha namna hiyo, chenye mikono ya wanadamu?
Jibu: Kabla ya kujibu swali hili, tusome kwanza maandiko yafuatayo…
Yohana 14:11 “Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, SADIKINI KWA SABABU YA KAZI ZENYEWE”
Hapa Bwana YESU anatoa njia za sisi kumwamini yeye, kwamba kama hatutamwamini kwa yeye kutuambia kwa mdomo wake mwenyewe, basi tumwamini kupitia zile kazi anazozifanya ambazo ni ishara na miujiza.
Hiyo hakika ni hekima kuu sana!… kwamba kama sisi ni kazi sana kumwamini yeye kwa maneno ya kinywa chake, basi tuzipime zile kazi anazozifanya ikiwa ni halisi na za kweli, basi tumwamini kwahizo pasipo hata maneno yake.
Vile vile na hata kuhusiana na waandishi wa Biblia, kama hatuwaamini kuwa wameandika mambo waliyovuviwa na MUNGU, basi kupitia matokeo ya kazi hizo, (jinsi yanavyobadilisha watu wengi leo, na kuponya watu wengi) basi tuamin
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni