Ijumaa, 16 Mei 2025

SOMO; MALAIKA MKUU URIELI.

     SOMO: MALAIKA MKUU URIELI.

Karibuni Katika Elimu hii Mfahamu huyu Malaika Na Ujue Majukumu yake ili leo umtumie kwenye Maombi yako. SOMO HILI LINALETWA NA PASTOR RICHARD 

     URIELI ni malaika mkuu mwenye hekima nyingi ambaye aliwapa watu ujuzi wa alkemikali . Anaitwa Malaika Mkuu wa Wokovu katika vitabu vya Kiyahudi-Kikristo. Mtu anaweza kupata utambuzi wa kiakili, masuluhisho ya vitendo na uwezo wa ubunifu kwa kuongea naye kwa njia ya maombi.

    MALAIKA URIELI:NI Malaika Wa ngazi ya Juu kama kina Gabriel Michael nk

Kitabu;Waebrania 1:6-14 Ufunuo;7;11 Mathàyo:25:31

MALAIKA URIELI ni Malaika Mkuu wa Ujuzi yaani Vipawa na Karama na Wokovu

KAZI ZAKE HUYU MALAIKA:

1;Kuwaleta Watu Kwenye Wokovu.
Huwafungua ufahamu watu nakusema nao Kuwaweka wazi Wanayoyafanya ni chukizo kwa Mungu huacha na kutubu.

2:Kuweka Hekima na Ukweli ndani ya Watu.
Ndiyo maana unaweza kukuta mtu mkweli kila kitu kipo kinachomsimamia awe hivyo mkweli huyu ni Urieli. Ukiwa muongo muongo ipo roho inakufanya uwe muongo.


3:Malaika Wa Moto Huweka Kiu au Shauku yaani Moto wa kutumika ndani yetu na humsukuma mtu aingie kwa Mungu amtumikie katika karama aliyonayo.

Kama hutakuwa nakiu huwezi kufanya kazi yake Mungu

.4:Malaika Wa Karama Mbalimbali.
Huyu Malaika huvisimamia vipawa ndani ya mtu vifanye Kazi unaweza ukawa na kipawa pasipo Malaika huyu kipawa chako hufa.

5;Hushughulikia Watu Wanaochanganyikiwa Akili au Kuvurungwa Akili kuzituliza Akili zao Wasichukue maamuzi mabaya mfano.Kujiua au kufanya maamuzi yatakayowafanya wajute.


6;Huweka Mwanga Kwa Waliongizani.
Kazi ya huyu Malaika huwatoa watu walio ngizani Waliofungwa kiufahamu au kifikira yeye huzifungua fikira zao nakujua wanapokosana na Mungu.

7;Huyu ndiye alishuka kwa kipindi cha Elisha wakaona Jeshi kubwa Malaika lilikuwa kundi la Malaika URIELI..


JINSI YA KUMTUMIA.
.
Muite aje katika kipindi ukiwa unavurungwa na kuchanganywa na Vitu mfano upo unayumbayumba huna utulivu mara akili inavurungwa upo kipindi kisichoelezeka huyu Malaika Anadili na Mfumo mzima wa ufahamu wako akiingia ataweka vitu Sawa.


OMBA HIVI.

Anza na Kuimba Tenzi au Kuabudu.
Hakikisha umekaa uweponi.

ANZA KUMWAMBIA.

Malaika mkuu URIELI Nakuita uje utilize akili yangu moyo wangu bado sioni mbele yangu nakabiliwa na mambo mengi mpaka yananichanganya akili yangu katika Jina la Yesu.Amen ×4


Malaika Wa Moto URIELI Shuka uteketeze taka zote zilizokamata Ndani yangu shambulia kwa Jina la Yesu.Amen ×4


Malaika URIELI Malaika wa Vipawa Inua vipawa ndani yangu inua huduma ndani yangu katika Jana la Yesu.Amen ×4


Mtumìe huyu Malaika AJE ASHUGHULIKIE ufahamu Akili yako iliposhindwa.


Share Somo hili Nzuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni