πͺπ«DARASA LA UCHUMBA ππ
π΄π΄π΄ππππππππππ
Mithali;12;1-3
.Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
Zaburi 121:7-8
[7]BWANA atakulinda na mabaya yote,
Atakulinda nafsi yako.
[8]BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,
Tangu sasa na hata milele.
Kuna Hiki Kwenye Mahusiano Kitambue Usianzishe Mahusiano ukiwa upo unapitia stress au umetoka kuumizwa au kuna vitu vinakuvurunga.
Hii ni Kwa Ajili ya Usalama Wako Wa Kiakili na Hata Kiufahamu .
HAYA YAFATAYO HUJITOKEZA KWA ANAYEJICHANGANYA.
1;STRESS NDIYO ZITAKUWA FIMBO ZA SHETANI KUZITUMIA.
Mara nyigi ukiwa umetoka kujeruhiwa au unavitu vinakusumbua akilini akuanzisha Mahusiano Tengemea uchumba wenu utakuwa wa ugomvi au kukosa Amani Sababu umeingia Kwenye uchumba na maroho ya kujeruhiwa na maumivu mbalimbali shetani atakuhubiria STRESS zako kwenye uchumba mpya nao utavunjika.
2.USIZITUMIE STRESS ZAKO KWA MCHUMBA WAKO. ULIYENAYE.
Matatizo yako au changamoto ulizowahi kuzipitia au unazozipitia usianze kumweleza mchumba wako ambaye hajakuowa au hujamuowa Usiaze Kumtwika madeni yako au Kodi Akulipie au Karo hivyo hivyo mwanaume Bint kama hujamuowa usiaze Kuchukua Pesa au Kwenda kwenye Nyumba aliyopanga Bint au anapokaa Usiaze kumwambia Akupe mtaji
Hakikisha Akuowe au uolewe naye ndiyo uanze kumuomba hela na kufanya mambo kama mke na mume.
3.NAFASI YA MKE AU MUME USIAZE KUITUMIA KWENYE UCHUMBA.
Mwanamke hurusiwi kwenda kwa kijana ukamfulie nguo au ukampikie au Kwenda Kumtandikia Kitanda chake Na Wewe Kijana Wa Kiume Usiende kwa Bint Ukaanza kumhudumia kumgharamia wakati siyo mkeo na hujui wewe ndiyo utaishi naye.
Hayo yafanye ndani ya ndoa
4:USIMKATIE SIMU MCHUMBA WAKO AU KUTOKUJIBU SMS KISA UNAPITIA KIPINDI.
Usianze Kuvunja uchumba wako au Kuharibu furaha ya Mahusiano yako kwa matatizo au changamoto zinazokuvurunga hasira ukazirundisha Kwa akupenda ukaacha kuongea naye au kukata simu zake wakati yeye anakuwa hajakukosea lakini kazini umevurungwa unaleta hasira kwenye uchumba wako.
Utavunja Mahusiano yako mwenyewe ukiwa hivi.
5; UWE NA MSIMAMO USIWE MLEVI WA UCHUMBA.
Mlevi huyumba yumba haeleweki amesimama au anaenda kuaguka chini Wewe unatakiwa uwe na msimamo mkali Wa kuolewa siyo kuchezewa au Kutumiwa na shetani kwa dhambi za kuzini mbali Mungu akutumie ufanye Tendo la Ndoa
Hakikisha huvunji uhusiano wako na Mungu kwa Kuzini na mtu asiyejulikana kwa wazazi.
TUFANYE NINI
Uchumba Unaitaji Uanzishe Ukiwa hujavurungwa akili ikiwa ipo vizuri na unao utimamu wa kiafya na kiakili Sababu unaenda Kuandaa Ndoa na Familia Bora ya Baadae.
WITO
Niulize inbox au tuma kero yako inbox nitakujibu pia share kwa watu ujumbe huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni