Jumatatu, 20 Mei 2024

SOMO: MAISHA YA NDANI YA NDOA

    .,,,,,.SHULE YA WANANDOA,,,,,,
$$$===================$$$$$$


   SOMO:MAISHA NDANI YA NDOA  


Habari Wanandoa  Tuongee+18 Nawakaribisha Somo hili Ambalo Limenijia Usiku huu niweze kufundisha Wanandoa Mambo Sita yanayotufanya Ndoa Tuishi na Kuifurahia na Kuiongoza vyema Bila Matatizo au Misukosuko Tunaotaji Kukubali Neno liingie kwenye maisha ya ndoa zetu 

Biblia Inaangiza namna ya Kuishi ndani ya ndoa.

Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa Nipo Morogoro Veta Dakawa Kutoka Kanisa la Moto wa Yesu.


TUNAISHI NDANI YA NDOA KWA KUFATA HAYA 


1;KWA HEKIMA; (Mithali;14;1)


Ili ndoa Zetu Ziwe Salama Tunaitaji Mungu atujalie hekima ya hali ya juu sana Ndoa Siyo uchumba ndoa siyo kitu rahisi kama huna Hekima Nikushauri tu ni bora usiowe au kuolewa sababu utaumia sana ukiingia ndani ya ndoa huna hekima.

TUSOME ANDIKO..

Mithali 14:1
[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; 
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. 


Lishike hili Angizo la Kwanza liwe kwenye ndoa yako.


2.KWA AKILI SANA; (1Petro:3:7)

Wanandoa Pekee Wanaitaji wawe na Akili ya kujuana haraka kumjua mwezako mapungufu yake kujuana tabia zenu ukiwa ndani ya ndoa harafu mwezako humjui au Akili zako mpaka zishutuliwe ndiyo ujielewe upo ndani ya ndoa ufahamu wa kujiongeza mwenyewe huna uwezo wa kufanya vitu huna Upo upo tu Ndoa hii kwa vyovyote itakuwa na shida.

Ukiingia ndani ya ndoa sababisha kuleta utofauti wa maisha yako kabla hujaowa na baada ya kuowa.

TUSOME ANDIKO:

1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu


3.KWA KUTII (Waefeso;5;22)

Utii huwa unanguvu Sana Mwanamke Mtii mumeo na kumsikiliza unapoingia ndani ya ndoa ukianza kiburi na jeuri Mtaanza Kupisha na kugombana Kumbe neno utii mumeliondoa Ndani Ya Ndoa. Mumeo akisema hapendi matumizi mabaya ya Pesa uelewe kuna vitu unavinunua hivina maana kwa wakati huo basi msikilize uache mara moja.


TUSOME ANDIKO:

Waefeso 5:22
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 


4;KWA TENDO LA NDOA;(1 Wakoritho; 7:3)

Mwanamke ukiwa ndani ya ndoa ni wajibu wako kumpa tendo la ndoa mumeo muda wowote ule anapoitaji hali kadhalika na Mwanaume mkeo akiitaji tendo la ndoa ni wajibu wako Kumpa tendo la ndoa mkeo Asiwepo kati yenu Anayemzuia mwezake katika haki yake ya ndoa Na hii itawafanya Ndoa Yenu I imagine Zaidi.

TUSOME ANDIKO:

1 Wakorintho 7:3
[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 

.
5.KWA UPENDO MWINGI (Waefeso:5;25-29)


Ni wajibu wa mke na mume upendo kwao kupendana katika viwango vikubwa chochoeni Upendo ndani ya ndoa Msiupuguze Upendo fanyeni vitu mnavyojua vinawapa upendo zaidi na Kukaa ndani ya upendo.

TUSOME ANDIKO 

Waefeso 5:25
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 


6:KWA KUSHAURIANA NA KUONYANA KUHESHIMIANA(1Wathesalonike.5:12-22)


Ndoa huhitaji kushauriana kabla hujafanya kitu sharing na mwezako Pia Kama Amekosea muonye kwa Kukaa naye nakumuelekeza kwa sauti nzuri usimfokee au Kumgomba mwezako pia mheshimiane nyinyi  kwa nyinyi ndani ya ndoa Yenu.


TUSOME ANDIKO;

1 Wathesalonike 5:14
[14]Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. 



         TUFANYE NINI SASA;

Tunatakiwa kuzitengeneza ndoa zetu sasa katika vile biblia inavyotuangiza kama tulivyojifunza 

Ulikuwa Pamoja nami Pastor Richard katika kukuandalia Nakala hii kwa usaindizi wa Roho Mtakatifu 


.Share Somo hili au Lisave hata kama hujaolewa litakusaindia ukija Kuolewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni