Alhamisi, 23 Mei 2024

SOMO: SI SAHIHI KUFANYA HAYA MBELE ZA MUNGU.

:::::"""""DARASA LA UCHUMBA::::""""""",,,,,
===============================
SOMO: SI SAHIHI KUFANYA HAYA UNAPOTAKA MWEZA

Tusome Mwanzo:24 Yote

Karibu Ujue mambo Ambayo Siyo Sahihi Kuomba mke au mume mbele za Mungu ukiwa navyo Akilini mwako vitakupa majibu siyo sahihi ukivishikilia Hivi vitu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Tusome hii misitari.
👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Mathayo 1:19
[19]Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 


Mwanzo 24:28
[28]Basi yule msichana akapiga mbio, akawaambia watu wa nyumba ya mama yake mambo hayo. 


Mambo Haya Siyo Sahihi Kuomba Huku Ukiwa navyo  Mbele Za Mungu Ukitaka Akupe Mume kutoka Kwake.
🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🍉🌳🌳🌳

1; KUOMBA  MAOMBI YA KUPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA MUNGU HUKU UKIZINI


Yaani ukiwa upo katika kutafuta mme au mke wa kutoka kwa Mungu lazima uwe mwaminifu Wa kuacha kuzini Na Kuwa mwaminifu kwa Mungu kuepuka dhambi hii 

Lakini Usipoepuka Kuzini Na Ukawa unaomba nakufunga Mungu Akupe mke au mume Shetani atafulululiza kuwaleta watu wake ambao watakuja na Mawazo ya Kuzini nawewe tu na ukifanya hivyo wanakuacha.

Mithali:6:32 Ukizini unabembelea mikosi laana na hata kukosa thamani ya kuitwa mtoto wa Mungu tena.


2.KUOMBA HUKU UKIWA UMEWEKA MTU AKILINI.

Usiende Kuomba huku mawazo yako Kuna kijana au Bint Kanisani Anakuvutia kwa kuwa yupo karibu nawewe au anakuchangamkia ukionana naye au Kuanza Kuomba Mtu fulani Akuowe Huku ukimtaja Jina lake Au Kuanza Kumwambia Kijana Akuowe Ambaye hujaomba umekaa tu mawazo yako yakakutuma kwa kuwa umeona yupo kwenye Group la maombi linaloongozwa na Pastor Richard ukajua sahihi omba kujirizisha.

Kama Wewe huombi ni rahisi Shetani kukuletea mtu ambaye siyo sahihi kwako.


3:NI MUHIMU UWEKE VINGEZO KAMA ISAKA UNAPOOMBA.  USIOMBE BILA VIGENZO KUWEKA ILI UJUE KIURAHISI


Ili iwe rahisi Kwako Kujua maombi yako Mungu Amekujibu Ni Muhimu Kuweka  Viashiria fulani au kuweka Alama endapo huyo mtu ni wako Mungu Afanye vitu hivi na hivi.

Ukiona Mungu Amevifanya hivi vitu ujue huyo ni sahihi ubavu wako taba naye usimuache.
Ukiona hakuna haijatokea ulivyosema achana naye maana si ubavu wako. Yupo anakuja uliyeandaliwa endelea kuomba.


4;KUWA NA BABA YAKO WA KIROHO ALIYE VIZURI KIROHO ILI AKUONGOZE VIZURI NA HAKIKISHA UNAMTII NA KUFATA MUONGOZO  USIOMBE MAOMBI UKIWA HUNA BABA.

Hii watu wengi hupuuza wanakuwa na wachungaji wengi au mababa wa kiroho wengi Unajikuta hata Mungu Unamvuruga Eleweka Uwe na Baba yako wa Kiroho utakayeshuhudiwa ndani yako huyu ndiye atakuwa baba yangu hata niende wapi nitamshirikisha mambo yangu yeye nitaomba ushauri nayeye ndiye atakayeniombea Usiwe wa kuombewa ombewa na kila mtu anakushika kichwa chako uwe na mtu mmoja Baba mmoja kwigne kasali kisha toka ukiambiwa wenye matatizo pateni mbele kama siyo kwa Baba yako Usitoke 

Heshimu mafuta na Upako alumnae Baba yako unaweza kukuvusha Mungu kamwamini ndiyo maana akakupa akuongoze kiroho awe anakuombea.

Eleweka utulie Sehemu moja Fungu la kumi toa kwa Baba yako wa kiroho na Siyo kila sehemu unatoa fungu la kumi.


5:WEKA RATIBA NA UKOMO WA MAOMBI 
USIOMBE BILA MUDA


.Unatakiwa uwe na muda maarumu uliotulia kuombea hili lakini unapoombea

Anza kutoa fungu la kumi kwa huyo Baba wa kiroho mshirikishe kila hatua Na Ufate Muongozo wake na Atakavyokushauri Endelea kuomba mpaka Ukomo wa Muda uliojiwekea.

Ukifika huo muda hujaona majibu endelea kushukuru kwa Mungu na uache kuombea tena hilo baadala yake Uwe mwaminifu wa fungu la kumi kwa Huyo Baba yako wa kiroho na kuomba mahitaji mengine.

Mungu atakuja kukujibu Maombi yako na ukijibiwa utaona viashiria vyote ambavyo uliziweka huyo mtu anavyo  utaelewa kwa haraka.


USHAURI WANGU KWAKO.

Changua kwanza uwe na Baba wa Kiroho Uanze kufata muongozo wa Baba yako wa kiroho pia kumshirikisha Changua Baba atakaye kulea kukuongoza kukusikiliza na unamwelewaa anapokufundisha pia Ambaye huyo ndiyo atakufikisha kwenye majibu yako na uhakikishe Uaminifu wa Fungu la Kumi kwake.

Baba wa Kiroho hata akiwa yupo mbali nawewe lakini unaweza kuongea naye akakushauri kukusikiliza ukamwelewa Basi huyo atakufaa 

Huwezi Kwenda Kiroho Kama humsikilizi Baba yako wa Kiroho Mungu aliyekupa kama utapata wa nje na unaposali ni vyema ukamuomba nataka uwe Baba yangu wa kiroho nakuanzia Leo nitatoa zaka kwako.

Ukifanya uchanguzi wako uwe na msimamamo usiyumbe yumbe utulie huko

Ikitokea kanisa unalosali linakulazimisha utoe utatumia Hekima maana Wengi Fungu la kumi hulichukua kimwili Utakachofanya mwezi huu utatoa kanisani mwezi ujao unatoa kwa Baba yako wa kiroho ili kutembea na Madhabahu yako ujue ulipo siyo Madhabahu yako.


HITIMISHO 

Ansateni Sana Kwa Masomo haya najua umepata picha Ya vitu unaweza ukawa una unafanya siyo sahihi

Nifate inbox uniulize Ambapo hujaelewa 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni