Jumatano, 6 Januari 2021

MSINGI WA IMANI

IMANI YA DHEHEBU:Linaamini Mungu ni mmoja katika nafsi tatu ambaye ni Baba wa wote wamchao na ndiye aliyeumba mbingu na nchi. YESU KRISTO Mwana wa Mungu ni njia pekee ya wokovu kwa wanadamu wote. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni ahadi ya waliopokea wokovu huo.

B. MISINGI YA IMANI YA DHEHEBU:

      Dhehebu linaamini kuwa:


(a) Maandiko yamevuviwa: 
Maandiko ya Agano Jipya yamevuviwa kihalisi na Mungu mwenyewe na ni Ufunuo wake Mungu kwa wanadamu, pia ni Kiongozi cha Imani kisichoshindwa wala kubadilika. ( 2Timo. 3:15-17, 1Wathes. 2:13 2Petro. 1:21 )


(b) Mungu ni mmoja aliye hai na wa kweli: 
Mungu mmoja tu aliye hai na aliye wa kweli amekwisha kujifunua mwenyewe kama "mimi Niko" aliye wa milele, Muumbaji wa mbingu na nchi na Mkombozi wa ulimwengu na wanadamu. Yeye pia amejifunua zaidi kama mwenye kufuata mwenendo wa ushirikiano na husiano katika Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. ( Kumb. 6:4 Isaya 43: 10-11 Mathayo. 28:19 )


(c) Uungu wa Bwana Yesu Kristo: 
Bwana Yesu ni Mwana wa Mungu. Maandiko yanatangaza juu ya:-

(i) Kuzaliwa kwake na Bikira ( Mathayo. 1:18, 20-25 Luka. 1:31-35)


(ii) Maisha yake yasio na dhambi. (Waebrania. 7:26 1Petro. 2:22 )


(iv) Kazi yake ya malipizi juu ya masalaba ( 1Kor. 15:3 2Kor. 5:21 )


(v) Ufufuo wake kimwili kutoka kwa wafu. ( Mathayo. 28:6 Luka. 24:39 1Kor. 15:14 )


(vi) Kutukuzwa kwake upande wa kuume wa Mungu Baba. (Mdo. 1:9, 11:2, 23 Wafilipi 2:9, 11 Ebrania. Sura ya 1hadi ya 3 )


(d) Anguko la Mwanadamu: 
Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu akiwa mzuri na mwema; maana Mungu alisema "Natumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu" Hata hivyo mwanadamu kwa uasi na hiari yake mwenyewe alianguka na kwa njia hiyo akajiletea si mauti tu bali pia mauti ya Kiroho ambayo ni kutengwa na Mungu. ( Mwanzo. 1:26-27, 2:17, 3:16 Warumi 5:12-19


(e) Wokovu wa Mwanadamu:
Tumaini la pekee la mwanadamu la ukombozi ni kwa njia ya damu ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu iliyomwagika. ( Mathayo. 26:27-28, Ebrania. 9:22)

(i) Masharti ya Wokovu 
Wokovu unapatikana kwa njia ya toba mbele za Mungu na Imani katika Bwana Yesu Kristo. Kwa kuoshwa na kufanywa upya, kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho Mtakatifu na kuhesabiwa haki kwa neema kwa njia ya Imani; mwanadamu huweza kufanyika mrithi wa Mungu kulingana na tumaini la uzima wa milele. ( Luka. 24:47 Yohana.3:3 Warumi. 10:13 Waefeso. 2:8 Tito. 2:11, 3:5-7 )


(ii) Ushindi wa Wokovu. 
Ushindi wa wokovu ulio wa ndani ni ule ushuhuda wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu ( Warumi. 8:16 ) Ushindi wa nje kwa watu wote ni maisha ya haki na utakatifu wa kweli. ( Efeso. 4:24)


(f) Maagizo ya Kanisa.

(i) Ubatizo katika maji mengi 
Agizo la ubatizo wa kuzamisha, linatolewa katika maandiko. Wote wanaotubu na kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi na Bwana wanaweza kubatizwa. Kwa njia hiyo wanatangaza kwa ulimwengu kwamba wao wamekufa pamoja na Kristo na pia kwamba wao wamefufuliwa pamoja naye ili kuenenda katika upya wa uzima. ( Mathayo. 28:19 Marko. 16:16 Matendo. 10:27-48 Warumi. 6:4 )


(ii) Ushirika Mtakatifu. 
Meza ya Bwana itakuwa ina mikate na divai ( Divai iwe maji ya matunda ya mzabibu yasiyo na mvinyo) ambayo ni mfano wa kueleza ushirika wetu wa asili ya Ki-Mungu ya Bwana wetu Yesu Kristo kumbukumbu ya mateso yake na kifo chake hata ajapo. (1Korinho. 11:29 )


(g) Ubatizo wa Roho Mtakatifu. 
Waumini wote wanatakiwa na wanayo haki ya kutafuta ahadi ya Baba; yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu kulingana na agizo la Bwana wetu Yesu Kristo. Huu ulikuwa ni ujuzi wa kawaida kwa wale wote waliokuwemo katika Kanisa la Mwanzo la Kristo. Pamoja na ubatizo huo huja uwezo kutoka juu kwa ajili ya maisha ya utumishi na kutolewa kwa karama pamoja na jinsi ya kuzitumia katika kazi ya huduma. ( Luka. 24:49 Matendo 1:4-8 1Kor. 12:1-13 ). Ujuzi huu ni watofauti kabisa ingawa unalingana na ujuzi wa kuzaliwa upya. ( Mdo. 4:12-17 Mdo. 10:44-46 15:7-9 ). Pamoja na ujuzi huo wa ubatizo katika Roho Mtakatifu unakuja ujuzi mwingine wa kujazwa mpaka kufurika kwa Roho huyohuyo, (Yohana. 7:37-39 ) kumheshimu Mungu kwa undani zaidi, ( Mdo. 2:42 ). Pamoja na upendo wenye vitendo zaidi kwa ajili ya Kristo, Neno lake na kwa ajili ya wanaopotea.


(h) Ushahidi wa ubatizo katika Roho Mtakatifu. 
Ushahidi wa waumini katika Roho Mtakatifu unashuhudiwa kwa ishara ya nje iliyo ya kimwili ya kunena kwa lugha nyingine kama Roho wa Mungu anavyowajalia kutamka ( Mdo. 2:4 ). Kusema kwa lugha kunatokea wakati huu wa sasa na ni sawa na kiasi fulani cha ile karama ya lugha ( 1Kor. 12:4-10, 28 ) ingawa ni tofauti katika makusudi ya matumizi.


(i) Utakaso: 
Ni tendo la kutengwa kutokana na kile kilcho kiovu na kuwekwa wakfu kwa ajili ya Mungu ( Warumi 12:1-12 1Wathes. 5:23 Waebrania. 13:12 ). Maandiko yanafundisha juu ya maisha ya utakatifu ambao pasipo huo hapana mtu atakayemwona Mungu ( Waebrania 12:14). Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu sisi tunao uwezo wa kutii amri ile. "Iweni watakatifu kama mimi nami nilivyo mtakatifu" (1Petro 1:15-16 ). 

Utakaso huwa halisi katika muamini kwa kugundua na kufahamu utambulisho wake na Kristo katika kifo chake na kufufuka na kwa imani akajihesabu kila mara kwamba yupo katika muungano huo, na kwa kutoa kila kiungo kila mara kwa ajili ya kutawaliwa na Roho Mtakatifu. ( Warumi 6:11, 13:8-13 Wagalatia 2:20 Wafilipi 2:12-13)


(j) Kanisa: 
Kanisa ni mwili wa Kristo, Makao ya Mungu kwa ajili ya Roho, lenye vyeo vya Kimungu kwa ajili ya utimizo wa kazi yake kuu. Kila mwamini aliyezaliwa kwa Roho ni sehemu ya Kanisa ambalo ni kusanyiko la wazaliwa wa kwanza ambao wameandikwa mbinguni. ( Wefeso 1:22-23, 2:22 Waebrania 12:23)


(k) Huduma: 
Huduma ya Ki-Mungu pamoja na utumishi uliopangwa katika maandiko umetolewa na Bwana wetu kwa makusudi mawili:

(i) Kushuhudia ulimwengu. ( Marko. 16:15-20)


(ii) Kujengwa kwa mwili wa Kristo (Waefeso 4:11-13)


(l) Uponyaji wa Mungu: 
Uponyaji wa Mungu ni sehemu muhimu ya injili. Kufunguliwa kutokana na magonjwa ni kitu kilichopo katika malipizi na ni haki ya kila mwamini. ( Isaya. 53:4-5, Mathayo. 8:16-17 Yakobo. 5:14-16 )


(m) Tumaini lenye Baraka: 
Ufufuo wa wale ambao wamelala katika Kristo ni pamoja na kunyakuliwa kwao ambao wako hai na ambao wamesalia mpaka wakati wa kuja kwa Bwana, na ndilo tumaini lenye Baraka na lililo kuu zaidi katika Kanisa. ( 1Wathes. 4:14-17 Warumi. 8:23 Tito. 2:13 )


(n) Utawala wa Kristo wa miaka elfu: 
Kuja kwa mara ya pili kwa Kristo ni pamoja na kunyakuliwa kwa Watakatifu ambao ni tumaini lenye Baraka, kukifuatiwa na kurudi kwa wazi kwa Kristo pamoja na watakatifu wake kwa ajili ya kutawala hapa ulimwenguni kwa muda wa miaka elfu moja. (Zek. 14:5 Mathayo. 24:27-30 Ufunuo. 1:7, 19:11-14, 20:1-6 ) na utawala huu wa miaka elfu moja utaleta wokovu kwa Israel kama Taifa ( Ezek. 37:21-22 Sefania. 3:19-20 Warumi. 11:26-27 ) na kuanzishwa kwa amani ya ulimwengu mzima. ( Isaya. 11:6-9 Zaburi. 72:1-8 Mika. 4:3-4 )


(o) Hukumu ya Mwisho: 
Kutakuwepo na hukumu ya mwisho ambayo waovu wote watafufuliwa na kuhukumiwa sawasawa na matendo yao. Yeyote ambaye hataonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, pamoja na shetani na malaika zake, mnyama na nabii wa uwongo watateketezwa kwenye adhabu ambayo ni mauti ya milele, katika ziwa liwakalo moto na kiberiti ambayo ni mauti ya pili. ( Mathayo. 25:46 Marko. 9:43 Ufunuo. 19:20, 20:11-15, 21:8 )


(p) Mbingu mpya na nchi mpya: 
Sisi kulingana na ahadi yake twatazamia mbingu mpya na nchi mpya ambamo haki inakaa ndani yake. ( 2Petro.3:13 Ufunuo 21:22 )

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni