Alhamisi, 7 Januari 2021

MISINGI YA IMANI YETU

MISINGI YA IMANI YETU

Kanisa linaitwa Huduma Ya Roho Mtakatifu Ikiwa Ni Wito alioniita Bwana nakunipa Jina Hilo 2014 nakuita rasimi Mwaka 2015 Angizo na Sauti inasema Watu wafundishwe Katika Roho Mtakatifu ambaye hujenga MISINGI Yake Kupitia Neno la Mungu na Maombi.

Kanisa la Roho Mtakatifu (2Wakoritho;3;6) Huu mstari ndio unabeba imani Yetu

DHEHEBU HILI LA ROHO MTAKATIFU LINAAMINI KUWA.

1;UMOJA WA NAFSI TATU ZA MUNGU
  ✓Baba✓Mwana✓Roho Mtakatifu
Yohana;5;20-22 Yohana:6:44 Yohana;10;29-30

DHEHEBU HILI LINAAMINI Mungu Wetu Ni Nafsi Tatu Ambaye Baba Alituumba Mwana Alituletea imani ya wokovu akatukomboa na Roho Mtakatifu anaendeleza Kustawisha Kazi zilizofanywa na Baba na mwana.

2:MUNGU NI ROHO
Yohana:4:24 Yohana:6;63

Tunaamini Mungu Wetu Ni Roho na Anauwezo Mkubwa katika Roho na Anatenda Kazi Zake Katika Roho naye ndio Atiaye Uzima ndani Yetu na Kutufanya Tuishi Tupumue Na Sisi Tumfatao Tunamwendea Na Kumwabudu Katika Roho.

3:ONDOLEO LA DHAMBI KUTUBU NA KUIACHA MWENYEWE;(TOBA)

Mathayo:3:8 Marko:1:4 Luka:3;8 Warumi;2:5

Tunaamini Mtu hupatana na Mungu pale anapotubu nakuiacha Dhambi mwenyewe Sio Akatubu Dhambi akaendelea nayo Tunaamini Ondoleo la Dhambi lipo Katika Toba Ya KWELI Sisi Kama Watoto Tulioitwa Tuushuhudie ukuu wa Roho Mtakatifu Tunapaswa Tuwe Watu wa Toba nakuacha Dhambi.

4;MSAINDIZI NI ROHO MTAKATIFU KIONGOZI WA KANISA
Yohana;14:26 Yohana;15:26 Yohana;16;7

Tunaamini Uongozi wetu wa Kiroho na msaada wetu wa Safari ya mbinguni Ni Roho Mtakatifu Tukimpokea Katika Toba ya Kweli na Ushuhuda uliosafi mbele za Mungu na KWA Wanadamu Tukiushuhudia ulimwengu na Dunia Nzima habari za Roho Mtakatifu Kupitia Neno na Maombi. Tunaamini Roho Mtakatifu Ni Kiongozi wa imani Yetu

5;NENO LA MUNGU NA UWEZA WAKE
Mathayo:24:35 Marko;4:14-22 Yohana:8:31-32,47 Yohana:1:1

Tunaamini muujiza na uponyaji unapatikana Mtu KWA Kufundishwa Neno la Mungu na Kuongozwa Katika Roho ili Kukuza Imani Yake nakumfanya ajue Kumtengemea Mungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni