Somo: Kufupisha Muhula wa Shetani
Shetani Hutengeneza Muhula Yaani Majors ya Kumtesa mtu na Kumuonea Hasa Mtu Asiyejua hili Anaweza Akawa Anateseka Wanajipa Moyo Kumbe Anakuwa YUPO kwenye Kipindi cha Muhula kwa Audi
Karibu ufatane namimi
Mwalimu: Pastor Richard (Morogoro)
WhatsApp+255710889892
1. Pointi za Msingi (Misingi ya Somo)
- a) Mungu Ndiye Mwenye Mamlaka ya Majira:
- Shetani hana mamlaka ya kudumu juu ya muda wako; Mungu anaweza kuingilia kati na kukatisha mpango wa adui.
- Zaburi 31:15: ✍🏾"Zama zangu [nyakati zangu] zimo mikononi mwako; Uniponye na mikono ya adui zangu, nao wanaonifuatia."
- b) Shetani Anajua Muda Wake ni Mfupi:
- Adui hufanya kazi kwa shinikizo kwa sababu anajua hana muda mrefu wa kutawala.
- Ufunuo 12:12:✍🏾 "Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao ndani yake. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu."
- c) Ahadi ya Mungu ya Kufupisha Siku za
- Dhiki:
- Mungu ana uwezo wa kupunguza muda wa mateso kwa ajili ya wateule wake ili wasiangamie.
- Mathayo 24:22: "✍🏾Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mwili wo wote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupizwa."
- d) Mamlaka ya Kisheria ya Muumini: ✍🏾Unayo haki ya kisheria ya kusimamisha utawala wowote wa giza kupitia kile unachokitamka.
- Mathayo 18:18: ✍🏾"Amin, nawaambia, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."
2. Njia za Kibiblia za Kufupisha Muhula wa Adui
A. Kwa Kupitia Nguvu ya Damu ya Yesu
Damu ya Yesu inabatilisha kila mkataba wa muda ambao adui alikuwa ameupanga kukaa kwenye maisha yako.
- Waebrania 9:12: ✍🏾"Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele." (Ukombozi huu unavunja vifungo vya muda).
B. Kwa Kutumia Maombi ya Hukumu na Amri
Unapotoa amri, unabadilisha majira ya kiroho kinguvu.
- Ayubu 22:28:✍🏾 "Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na nuru itaziangazia njia zako."
C. Kwa Njia ya Kufunga na Kuomba (Fasting)
Kufunga kunaongeza kasi ya kupata matokeo na kuvunja vizuizi vya muda ambavyo adui ameweka.
- Isaya 58:8: ✍🏾"Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakuwa nyuma yako ukulinde." (Neno "mara" linamaanisha kufupisha muda wa kusubiri).
D. Kwa Kuleta Sadaka na Ibada ya Sifa
Sifa na dhabihu zinahamisha usikivu wa Mungu na kufanya adui akimbie nafasi yake haraka.
- 2 Mambo ya Nyakati 20:22: "Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waotea juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa." (Hapa muhula wa vita ulifupishwa ndani ya muda wa sifa).
E. Kwa Kutumia Neno la Ushuhuda.
Kushuhudia kile Mungu alichofanya kunamfanya adui asipate nafasi ya kuendelea kukaa.
- Ufunuo 12:11:✍🏾 "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; kwa maana hawakupenda maisha yao hata kufa."
HITIMISHO
Shughulikia Kukatisha Muhula Wa Shetani Ili Usione Mateso uone Wokovu Wa Bwana.
Shirikisha SOMO wengine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni