SOMO:MAOMBI YA WIKI MOJA KUOMBEA NCHI YETU YA TANZANIA
Shalom Shalom Mtoto wa Mungu Nasikia Sauti Tutembee Siku Saba Tukomboe NCHI YETU KUOMBA REHEMA NA TOBA KWA AJILi YA TAIFA LETU.
HATUA YA KWANZA TUTATUBU
2Nyakati:7;14-15
2 Mambo ya Nyakati 7:14
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
OMBA HIVI:
A) . Baba Nasimama Kwa niamba Ya Taifa langu La Tanzania🇹🇿 Ninaomba ulisamehe Taifa langu Kila lilipomwanga Damu na Damu ambazo hazina Hatia Zinapaza Sauti mbele zako zikilalamikia uongozi wa nchi yangu na kuendelea kuilaani Nchi yangu Mimi ni Mwanao nikiwa ndani ya hili Taifa la Tanzania Nasimama kwa Niamba Ya Rais Wa Nchi Nikiwabeba na Washauri wake na viongozi wote waliomzunguka Rais wangu baba naomba msamaha Msamehe Msamehe Rudisha Amani Amani Ya Nchi Yangu na Furaha Katika Jina la Yesu. Amen
Rudia×5
MAOMBI YA KUG,OA KILA WANAOTAKA KUHARIBU AMANI YA NCHI YETU YA TANZANIA.
Soma huuu mstari wa kusimamia
2 Mambo ya Nyakati 7:20
ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote.
B) Baba Yangu Nasimama Katika Nafasi Yangu Kama Mwanamaombi Nikisimama Kwa Ajili ya Nchi Yangu Kug,oa Kug,oa Kila roho inayoingia Kwa Siri ikulu na kutaka kusababisha Uvunjifu wa Amani Kila Mtu anayetaka Watanzania wagonbane au Kukosana Ninatuma malaika wa Ukombozi Kila nguvu Kila mamlaka inayijiinua Naishusha china nakuipandisha Juu mamlaka Uliyoiandaa wewe na kiongozi uliyekusundia Aongoze Watanzania Suhulisho lipatikane kwa Mazungumzo na Muafaka Upatikane bila Damu Kumwangika Katika Jina La Yesu..... Endeleaa KUOMBA unavyoelekezwa na Roho Mtakatifu Ruhusu kutamka maneno yanayokuja Kinywani Mwako.
Tembea Tembea Unapoombea Nchi yako ibebe Tanzania Kwa Machozi Kila Siku Saa Nane mpaka Saa Kumi Kamili Alfajili.
Share na muunge Kila mmoja mwenye upendo na Nchi yake Ya Tanzania
. Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit Church Tanzania🇹🇿
WhatsApp+255710889892
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni