Maana Ya Ndoa;
Ni Muuganiko wa watu wawili jinsia ya kike na ya kiume Wanaokubaliana Pamoja Kwenda Kuanza maisha yao nakutengenenza familia zao.
TUKIO LINALOKAMILISHA NDOA huitwa harusi hili huwa tukio linaloheshimiwa na kukusanya watu wengi katika Jamii.
UCHUMBA:Hiki ni kipindi wanachokipitia Wanandoa Kujuana Vizuri Tabia Zao Mienendo Yao.
Ambayo huweza kuchukua mwezi miezi na mwaka mmoja Inatosha hawa kujuana Vizuri
Uchumba ukikaa muda mrefu hupelekea hawa wawili kuanguka dhambini.
Waebrania 13:4
[4]Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
NDOA IMEGAWANYIKA MARA TATU
==============================
1:MAISHA NDANI YA NDOA.
2:VIPINDI VYA NDOA
3:CHANGAMOTO ZA NDOA.
4:MAFANIKIO NDANI YA NDOA
Haya ni Muhimu Kabla Hujaingia Kwenye Ndoa Uyatambue Karibu Ujifunze Kitu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
MAISHA YA NDOA.
===================
Kuingia Kwenye ndoa ni wewe Kujifunga uanze Kuishi Maisha ya ndoa na kufata Kanuni Sita Za Namna Ya Kuishi ndani Ya Ndoa
TUNAISHI NDANI YA NDOA KWA KUFATA HAYA
ππππππππππππππ
1;TUNAISHI KWA HEKIMA; (Mithali;14;1)
Ili ndoa Zetu Ziwe Salama Tunaitaji Mungu atujalie hekima ya hali ya juu sana Ndoa Siyo uchumba ndoa siyo kitu rahisi kama huna Hekima Nikushauri tu ni bora usiowe au kuolewa sababu utaumia sana ukiingia ndani ya ndoa huna hekima.
TUSOME ANDIKO..
Mithali 14:1
[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Lishike hili Angizo la Kwanza liwe kwenye ndoa yako.
2.TUNAISHI KWA AKILI SANA; (1Petro:3:7)
Wanandoa Pekee Wanaitaji wawe na Akili ya kujuana haraka kumjua mwezako mapungufu yake kujuana tabia zenu ukiwa ndani ya ndoa harafu mwezako humjui au Akili zako mpaka zishutuliwe ndiyo ujielewe upo ndani ya ndoa ufahamu wa kujiongeza mwenyewe huna uwezo wa kufanya vitu huna Upo upo tu Ndoa hii kwa vyovyote itakuwa na shida.
Ukiingia ndani ya ndoa sababisha kuleta utofauti wa maisha yako kabla hujaowa na baada ya kuowa.
TUSOME ANDIKO:
1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu
3.TUNAISHI KWA KUTII (Waefeso;5;22)
Utii huwa unanguvu Sana Mwanamke Mtii mumeo na kumsikiliza unapoingia ndani ya ndoa ukianza kiburi na jeuri Mtaanza Kupisha na kugombana Kumbe neno utii mumeliondoa Ndani Ya Ndoa. Mumeo akisema hapendi matumizi mabaya ya Pesa uelewe kuna vitu unavinunua hivina maana kwa wakati huo basi msikilize uache mara moja.
TUSOME ANDIKO:
Waefeso 5:22
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
4;TUNAISHI KWA TENDO LA NDOA;
(1 Wakoritho; 7:3)
Mwanamke ukiwa ndani ya ndoa ni wajibu wako kumpa tendo la ndoa mumeo muda wowote ule anapoitaji hali kadhalika na Mwanaume mkeo akiitaji tendo la ndoa ni wajibu wako Kumpa tendo la ndoa mkeo Asiwepo kati yenu Anayemzuia mwezake katika haki yake ya ndoa Na hii itawafanya Ndoa Yenu I imagine Zaidi.
TUSOME ANDIKO:
1 Wakorintho 7:3
[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
.
5.TUNAISHI KWA UPENDO MWINGI (Waefeso:5;25-29)
Ni wajibu wa mke na mume upendo kwao kupendana katika viwango vikubwa chochoeni Upendo ndani ya ndoa Msiupuguze Upendo fanyeni vitu mnavyojua vinawapa upendo zaidi na Kukaa ndani ya upendo.
TUSOME ANDIKO
Waefeso 5:25
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
6:TUNAISHI KWA KUSHAURIANA NA KUONYANA KUHESHIMIANA(1Wathesalonike.5:12-22)
Ndoa huhitaji kushauriana kabla hujafanya kitu sharing na mwezako Pia Kama Amekosea muonye kwa Kukaa naye nakumuelekeza kwa sauti nzuri usimfokee au Kumgomba mwezako pia mheshimiane nyinyi kwa nyinyi ndani ya ndoa Yenu.
TUSOME ANDIKO;
1 Wathesalonike 5:14
[14]Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.
TUFANYE NINI SASA;
Tunatakiwa kuzitengeneza ndoa zetu sasa katika vile biblia inavyotuangiza kama tulivyojifunza
2:VIPINDI VYA NDOA.
πππππππππ
Ndani Ya ndoa huwa Kuna Vipindi Vitatu
Ni Lazima mtavipitia ni vyema kuvijua ili mmoja wenu akikianzisha unamponya mwezako.
1;KIPINDI CHA UTOTO WA NDOA YENU.
==================================
Marko:10:20
Hiki huwa ni kipindi Ambacho mnakuwa hamjuani Vizuri Tabia Zenu na Kila mmoja Anahamu na Mwezake Mengi mnafichana Na ni kipindi pekee mtaitana majina mazuri mtalishana hadi chakula mtaongozana hata kupika mtapika pamoja.
Hiki kipindi kitakufanya ufurahie ndoa yako.
2;KIPINDI CHA UJANA WA NDOA YENU.
1Timotheo:4:12
Hiki ni Kipindi Pekee cha nyinyi Wanandoa Kila mtu Anataka Afanye maamuzi yake Mmeshajuana Tabia Zenu kila mmoja anaanza Kufanya Visa Kutoka nje Kujibu ovyo na Kulalamika yaani najuta kukuowa wewe atakuwa mtu mwenye kiburi mwenye kujivuna tabia mbalimbali huibuka hiki kipindi usipokijua ndoa nyingi huvunjika kipindi hiki.
Inakupasa uwe makini ukimuona mwezako anaenda ujana wewe mwambie nenda peke yako mimi nabaki kwenye utoto.
3:KIPINDI CHA UZEE.
✍✍✍✍✍✍✍✍✍✍
Mwanzo 15:15
[15]Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
Hiki Kipindi cha Kuvumiliana imladi mlee watoto wenu kila mmoja Anaamua Apuuzie Tabia za mwezake Yaani utafanya vituko vyako hakuna anayejishughulisha nawewe.
3:CHANGAMOTO ZA NDOA
==========/////=/=//////=====
===============================
SOMO: VILIMA VITATU NDANI YA NDOA VYA KUVUKA.
Nimeamua Somo hili nilipe kichwa cha Somo kinachosema Vilima ndani ya ndoa ambavyo kila mwanandoa aliyemo huwa lazima Avishinde hivi ili kuifanya ndoa yake izidi Kuwa na Furaha na Amani
Mwanandoa na Unayetarajia muingie kwenye ndoa Fatana na Mimi Katika Darasa hili.
Mwaadaaji ni Mimi Mwalimu Wa Wanandoa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa
VILIMA NI NINI?
Ni vitu vya kuvuka ili ufike hatua nyigine ndani ya ndoa
VITU HIVI HAKIKISHA UNAVIVUKA NDANI YA NDOA.
MLIMA WA KWANZA;
=====$$$=====$$$$
1;MJUE VIZURI MWEZAKO
Mkeo au Mmeo Unatakiwa umjue na ujue Madhaifu yake na Mapungufu alimonyo Uelewe Namna utakavyomchukulia na kuyabembelea madhaifu na siri zake.
1 Wakorintho 11:3
[3]Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
MAMBO MATATU YAWE SILAHA YA KUVUKA.
1:Mpende Sana Na Udhaifu wake alionao.
2:Usimuumize au Kumdharau kwa alivyo.
3:Vumilia Hatua Zake Usitoke nje hata kama yeye anatabia hiyo usiinge.
Wewe Mshukuru Mungu Kwa Zawadi hiyo.
Mfanye Awe mtu anayempenda Mungu na Aliyekaribu na Mungu.
MFUNDISHE HAYA
=================
1;Utoaji: mweleze Baraka na Umhimu wa kutoa zaka na kuwa waaminifu wa Fungu la kumi.
2:Ibada: Mfundishe Na Kuweka Utaratibu wa Kufanya ibaada kabla hamjalala.
3:Ushirikiano; Mfundishe Awe Mwenye kufanya mambo kwa umoja na umuondolee ubinafsi wa vitu mbalimbali alivyo navyo.
4:Tengenezeni Mipango Mikakati maisha yenu ya kiroho na Ya Kimwili yawe yenye mafanikio.
3 Yohana 1:2
[2]Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako
.MLIMA WA PILI .
================
2;TENDO LA NDOA:
Tendo la ndoa ni kitendo cha kukutana kwa jinsia mbili ya kike na kiume Hii ndiyo huleta muuganiko wa ndoa na Tafsiri ya Mwili mmoja.
1 Wakorintho 7:3-4
[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
[4]Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
STAYLE ZA UFANISI WA TENDO LA NDOA.
Kuna stayle nyingi Sana Katika Tendo la Ndoa na Kila stayle ina Eneo lake la kutumika ndani ya ndoa uwapo na mwezi wako.
1:Stayle Za Kufanya Tendo la ndoa ukiwa unaitaji mtoto
●.hapa unatakiwa ufanye Tendo la ndoa katika Mikao Inayomfanya mkeo au wote wawili kutoshelezana na Kufikia kileleni haraka kwa mkeo.
●Fanya Tendo la ndoa Mkiwa hamjagombana kila mmoja afurahie tendo la ndoa
●Usifate Kalenda Mimba huweza kuingia hata bila Kalenda.
MLIMA WA TATU
3:LINDA PATANO LA KIAPO CHENU CHA NDOA
Mwanzo 9:9
[9]Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;
Hiki ni kipengele mhimu simamia na kulinda makubaliano Yenu.
Wanandoa Wengi Wanapopita katika vile vipindi vitatu ndani ya ndoa utaona wanaanza kugombana hasa wanapokuja kufanikiwa
Mwanamke au mwanaume simamia Patano la ndoa Yenu.
Ndoa hujengwa na nyinyi wawili msipende kutoa siri zenu za ndani hakikisheni usalama wa ndoa Yenu.
4: MAFANIKIO NDANI YA NDOA
=======///====///====///====
Mafanikio Ndani Ya Ndoa hutengemea misingi mitatu utakayoinjega kwenye ndoa Yenu.
Pembe hizo ni
1:MUNGU;
Kwenye ndoa Yenu muwekeni Mungu mbele kuliko Akili zenu.
Palipo na Mungu
Pana hofu ya Mungu.
Pana Uvumilivu wa juu.
Pana Upendo Wa Dhati.
Pana Amani
Pana Kuthamini
Pana Maombi
Pana Utoaji
Nk
2;MKE MMOJA;
Palipo na nanafasi ya mke mmoja Hapatakuwa na Usaliti Au Kuumizana tena.
Kwa kuwa umeowa futa namba za wapenzi wako wa Zamani Tulia na mkeo utembee ndani ya Agano la Mke mmoja.
3:MME MMOJA;
Palipo na Mume Mmoja Hakuna Usaliti tena au Maumivu tena
Mwanamke hakikisha unaweka Agano na mme mmoja waliokuwa wanakusumbua uwaambie kabisa nimeolewa Sasa. Sitaki Usumbufu.
5:MAMBO AMBAYO HUPASWI UFANYE.UKIWA NDANI YA NDOA
1;Kufanya vitu Bila Kushauriana na Mwezako.
2:Kueleza Siri au udhaifu unaouona kwa mwezi wako.
3;Kumsaliti au Kuvunja Agano lenu la ndoa
4;Kutokutoa Zaka au ibada na Mungu.
Wapo watu wakiingia kwenye ndoa wanaacha kutoa fungu la kumi.
5;Mkigombana Malizeni Utofauti wenu nyinyi msianze kuwapigia wazazi mtavunja ndoa Yenu.
MISTARI YA KUSIMAMIA KWENYE NDOA
πππππππππππππ
Methali 18:22: “Anayepata mke mwema amepata kitu chema.”
Maana: Biblia inaonyesha kwamba kufunga ndoa ni jambo jema.
Malaki 2:15: “Usimtendee kwa hila mke wa ujana wako.”
Maana: Mungu anawataka waume na wake wawe waaminifu na kutendeana kwa heshima, hata baada ya kuishi katika ndoa kwa miaka mingi.
Marko 10:9: “Kile ambacho Mungu ameunganisha, mtu yeyote asikitenganishe.”
Maana: Mungu alikusudia ndoa iwe muungano wa kudumu.
Waebrania 13:4: “Ndoa na iheshimiwe kati ya wote.”
Maana: Wenzi wa ndoa wanapaswa kuthamini sana ndoa yao na kutia jitihada ili kuilinda.
1 Wakorintho 7:28: “Wale [wanaofunga ndoa] watakuwa na dhiki katika mwili wao.”
Maana: Hakuna ndoa kamilifu; wenzi wa ndoa wanahitaji kushirikiana ili kushinda changamoto zinazojitokeza
HITIMISHO
Ni vyema kujua haya kabla ya ndoa kuanza kuishi
Wito
Shirikisha wengine Somo hili.