Jumamosi, 14 Juni 2025

SOMO;MALAIKA MKUU RANGUEL

SOMO:MALAIKA MKUU RAGUELI.

Karibuni Tena Mwendelezo Wa Somo letu hili la MALAIKA SABA WASIMAMAO MBELE ZA MUNGU. Ufunuo;8;2-4.

Admin; Bishop Richard Tz
Group la Maombi na Mafundisho
WhatsApp +255710889892
Join ujipatie masomo mbalimbali 

Tumetoka kujifunza Malaika wanne  
URIELI MALAIKA WA WOKOVU NA UJUZI

 RAPHAEL MALAIKA WA AFYA NA UPONYAJI

 METATRONI MALAIKA WA WATOTO 

NA MIKAEL MALAIKA WA ULINZI NA USALAMA(Hushughulika na Vita vita)

LEO TUNAENDELEA......
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 
Ninakuletea Somo hili  litakusaindia kujua namna ya kuwatumia Malaika Hawa.


LEO TUNAENDA KUMUONA MALAIKA WA TANO ASIMAMAE MBELE ZA BWANA.

MALAIKA MKUU RAGUEL Ndiyo Jina lake huyu ni Malaika Mkuu Wa MOTO.

Huyu Malaika Amefanya kazi na Musa 
Kutoka:3:3-5 Alitokea kwa umbo la kijiti

Huyu Amefanya kazi na Elia ukisoma 1wafalme 18: Alishuka akalamba Sadaka na maji

Ufunuo 20:9 Anaoneshwa hapa akishuka kuwateketeza waovu.

Huyu alifanya kazi na Sulemani Ndani ya hekalu la Sulemani Rejea 2Nyakati;7:1

Ndiye huyu alimtenganisha Eliya na Elisha alionekana kama Gari la Moto Rejea 2WAFALME:2:10-13

KAZI ZAKE HUYU MALAIKA RAGUEL.

1;Husimamia na Kuteketeza Waovu kwa Moto.

2;Humdhihirisha Mungu kwa umbo la Moto mfano shadrack na Abnego kwenye Tanuru huyu Malaika alikuwa nao.

3;Hutokea Kwa umbo la Moto kwa muonekano mbalimbali kuligana na Vita ilivyo.

4:Husimamia watu wanaotupwa kwenye ziwa la Moto huyu Malaika huwachukua kuwatupa kule kila hukumu ikisomwa.

5:Huagamiza Miungu Huharibu Madhabahu za Shetani kwa Kuzichoma moto.

6:Yeye ni Malaika Anayeshambulia na kutetea watoto wa Mungu walio katika kipindi cha kuteswa na falme za ngiza.


NAMNA YA KUMTUMIA MALAIKA MKUU RAGUEL.

1:Naangiza Malaika Mkuu Raguel Ashuke Ashuke Akaharibu Kila madhabahu za nyumbani kwetu Ashuke na Moto wake Akaunguze Akachome Akachome katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×4


2;Moto Moto Ushuke Kutoka Mbiguni Uwateketeze Kila watesi wangu kila wanaozuia maisha yangu yasibadilike Moto moto wa Malaika Mkuu Raguel ashushe Ashushe Uokoe katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia× 4


3:Nilipo hapa hapa Nataka Leo Nimuone Raguel Malaika Mkuu Wa Moto Anashusha Moto Anaharibu Ufalme wa shetani na Wachawi wote wa mtaa huu Raguel Shuka Uwapinge Uwapinge Kwa Moto moto moto katka Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×5

4:Majeshi ya kikosi cha Moto wakiongozwa na Malaika mkuu Raguel Washuke waje wazunguke zunguke kwenye nyumba yangu katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×7


HITIMISHO 

Tunapaswa kuwajua Malaika na Tuwatumie katika Vita vyetu waje watusaindie Tumia Malaika.

Nikuombe Share masomo haya yaliyokuja na nguvu ya kufungua watu kupitia Malaika wakuu wasimamao mbele za Bwana.


Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 
Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 
Makao Makuu Morogoro 


Jumamosi, 7 Juni 2025

MALAIKA MKUU MIKAELI

    SOMO; MALAIKA MKUU MIKAELI.


KIUMBE wa roho anayeitwa Mikaeli hatajwi mara nyingi katika Biblia. Hata hivyo, kila mara anatajwa akitenda jambo fulani. Katika kitabu cha Danieli, Mikaeli anapigana na malaika waovu; katika barua ya Yuda, anabishana na Shetani; na katika Ufunuo, anapigana na Ibilisi na malaika wake waovu. Anapoutetea utawala wa Yehova na kupigana na adui za Mungu, Mikaeli anatenda kupatana na maana ya jina lake—“Ni Nani Aliye Kama Mungu?” Lakini Mikaeli ni nani?

Nyakati nyingine, watu huitwa majina mbalimbali. Kwa mfano, mzee wa ukoo Yakobo aliitwa pia Israeli, na mtume Petro aliitwa Simoni. (Mwanzo 49:1, 2; Mathayo 10:2) Vivyo hivyo, Biblia inaonyesha kwamba Mikaeli ni jina lingine la Yesu Kristo, kabla na baada ya maisha yake duniani. Hebu tuone sababu za Kimaandiko zinazotufanya tukate kauli hiyo.

Malaika Mkuu. Neno la Mungu linamwita Mikaeli “yule malaika mkuu.” (Yuda 9) Ona kwamba Mikaeli anaitwa yule malaika mkuu. Hilo linaonyesha kwamba kuna malaika mmoja tu aliye mkuu. Isitoshe katika Biblia, jina “malaika mkuu” linatumiwa katika hali ya umoja tu, wala si kwa wingi. Zaidi ya hayo, Yesu anahusianishwa na wadhifa wa malaika mkuu. Kuhusu Bwana Yesu Kristo aliyefufuliwa, andiko la 1 Wathesalonike 4:16 linasema: “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni akiwa na mwito wenye amri, kwa sauti ya malaika mkuu.” Kwa hiyo sauti ya Yesu inafafanuliwa kuwa sauti ya malaika mkuu. Basi, andiko hilo linadokeza kwamba Yesu mwenyewe ndiye Mikaeli yule malaika mkuu.

Kiongozi wa Jeshi. Biblia inasema kwamba ‘Mikaeli na malaika zake walipigana na yule joka mkubwa na malaika zake.’ (Ufunuo 12:7) Kwa hiyo, Mikaeli ni Kiongozi wa jeshi la malaika waaminifu. Pia kitabu cha Ufunuo kinamtaja Yesu akiwa Kiongozi wa jeshi la malaika waaminifu. (Ufunuo 19:14-16) Naye mtume Paulo anamtaja kihususa “Bwana Yesu” na “malaika zake wenye nguvu.” (2 Wathesalonike 1:7) Kwa hiyo, Biblia inataja Mikaeli na “malaika zake” na Yesu na “malaika zake.” (Mathayo 13:41; 16:27; 24:31; 1 Petro 3:22) Kwa kuwa Neno la Mungu halionyeshi popote kwamba kuna majeshi mawili ya malaika waaminifu mbinguni—moja likiongozwa na Mikaeli na lingine likiongozwa na Yesu—ni wazi kwamba Mikaeli si mwingine ila ni Yesu Kristo akiwa katika wadhifa wake mbinguni. *

MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA

Shetani Alitoka Wapi..?

Swali: Je shetani yule audanganyaye ulimwengu alitoka wapi?


Jibu: shetani kwa asili aliumbwa na Mungu, na kabla ya kuwa shetani alikuwa akiitwa “Kerubi afunikaye”

Ezekieli 28:14 ” Wewe ulikuwa KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA AFUNIKAYE; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto”.

Na MUNGU alimwumba akiwa mkamilifu (asiye na dosari) kama tu MAKERUBI wengine, lakini baadaye moyo wake uliinuka akajidanganya mwenyewe kuwa anaweza kuwa kama MUNGU (aabudiwe kama MUNGU) Na ndipo Uovu huo ukaonekana ndani yake, na hakutaka kubadilika.

Ezekieli 28:15 “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”

Na baadaye alipoasi ndipo akawa shetani, na maana ya shetani ni Mshitaki/Mchongezi, maana yake anawashitaki wanadamu mbele za MUNGU mchana na usiku.

Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10  Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU”.



Swali la 2


SWALI LA PILI

. Tukio la Yesu kupaa kwenda mbinguni lilitukia eneo gani?. N.b weka andiko ku sapoti jibu lako


JIBU:    Mlima wa mzeituni. Matendo ya Mitume 1:12 [12]Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.


Mlima wa mizeituni..ambayo inapatika kati eneo la Bethania


Luka 24:50-51 [50]Akawaongoza *mpaka Bethania*, akainua mikono yake akawabariki. [51]Ikawa katika kuwabariki, *alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni*



Swali la 3

Swali: Tunasoma Simeoni alipomwona mtoto YESU, Alikiri kuuona Wokovu wa MUNGU, sasa swali ni Wokovu gani huo alioupata?


Jibu: Tuanzie ule mstari wa 25 ili tuweze kuelewa vyema…

Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26  Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27  Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28  yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29  Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30  KWA KUWA MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU WAKO,

31  Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32  Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli”

Sasa hapo hajasema AMEUPATA WOKOVU..La! bali anasema “MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU”.. kuuona wokovu na kuupata wokovu ni vitu viwili tofauti…

Wokovu wa Mungu unapatikana kupitia mmoja tu, naye ni YESU KRISTO (Matendo 4:12),..Baada ya YESU kusulibiwa ndipo watu wakaanza kuupata wokovu, lakini kabla ya hapo waliusikia na kuuona tu,…waliousikia ni manabii wa kale na watu wote wa agano la kale, na waliouona ni watu waliokuwepo kipindi BWANA YESU anazaliwa, na walioupata ni wote waliomwamini baada ya kufufuka kw

Je Kuna Haja gani Ya Kuamini Biblia Iliyoandikwa Na Watu?

Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?

Swali: Biblia imeandikwa na watu, (kama Paulo, Petro, Musa, Daudi na wengineo) je tutaamini vipi kitu kilichoandikwa na wanadamu kuwa ni kweli,? vipi kama wametoa tu kwenye akili zao, kwanini tukiamini kitabu cha namna hiyo, chenye mikono ya wanadamu?

Jibu: Kabla ya kujibu swali hili, tusome kwanza maandiko yafuatayo…

Yohana 14:11 “Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, SADIKINI KWA SABABU YA KAZI ZENYEWE”

Hapa Bwana YESU anatoa njia za sisi kumwamini yeye, kwamba kama hatutamwamini kwa yeye kutuambia kwa mdomo wake mwenyewe, basi tumwamini kupitia zile kazi anazozifanya ambazo ni ishara na miujiza.

Hiyo hakika ni hekima kuu sana!… kwamba kama sisi ni kazi sana kumwamini yeye kwa maneno ya kinywa chake, basi tuzipime zile kazi anazozifanya ikiwa ni halisi na za kweli, basi tumwamini kwahizo pasipo hata maneno yake.

Vile vile na hata kuhusiana na waandishi wa Biblia, kama hatuwaamini kuwa wameandika mambo waliyovuviwa na MUNGU, basi kupitia matokeo ya kazi hizo, (jinsi yanavyobadilisha watu wengi leo, na kuponya watu wengi) basi tuamin


Ijumaa, 16 Mei 2025

SOMO; MALAIKA MKUU URIELI.

     SOMO: MALAIKA MKUU URIELI.

Karibuni Katika Elimu hii Mfahamu huyu Malaika Na Ujue Majukumu yake ili leo umtumie kwenye Maombi yako. SOMO HILI LINALETWA NA PASTOR RICHARD 

     URIELI ni malaika mkuu mwenye hekima nyingi ambaye aliwapa watu ujuzi wa alkemikali . Anaitwa Malaika Mkuu wa Wokovu katika vitabu vya Kiyahudi-Kikristo. Mtu anaweza kupata utambuzi wa kiakili, masuluhisho ya vitendo na uwezo wa ubunifu kwa kuongea naye kwa njia ya maombi.

    MALAIKA URIELI:NI Malaika Wa ngazi ya Juu kama kina Gabriel Michael nk

Kitabu;Waebrania 1:6-14 Ufunuo;7;11 Mathàyo:25:31

MALAIKA URIELI ni Malaika Mkuu wa Ujuzi yaani Vipawa na Karama na Wokovu

KAZI ZAKE HUYU MALAIKA:

1;Kuwaleta Watu Kwenye Wokovu.
Huwafungua ufahamu watu nakusema nao Kuwaweka wazi Wanayoyafanya ni chukizo kwa Mungu huacha na kutubu.

2:Kuweka Hekima na Ukweli ndani ya Watu.
Ndiyo maana unaweza kukuta mtu mkweli kila kitu kipo kinachomsimamia awe hivyo mkweli huyu ni Urieli. Ukiwa muongo muongo ipo roho inakufanya uwe muongo.


3:Malaika Wa Moto Huweka Kiu au Shauku yaani Moto wa kutumika ndani yetu na humsukuma mtu aingie kwa Mungu amtumikie katika karama aliyonayo.

Kama hutakuwa nakiu huwezi kufanya kazi yake Mungu

.4:Malaika Wa Karama Mbalimbali.
Huyu Malaika huvisimamia vipawa ndani ya mtu vifanye Kazi unaweza ukawa na kipawa pasipo Malaika huyu kipawa chako hufa.

5;Hushughulikia Watu Wanaochanganyikiwa Akili au Kuvurungwa Akili kuzituliza Akili zao Wasichukue maamuzi mabaya mfano.Kujiua au kufanya maamuzi yatakayowafanya wajute.


6;Huweka Mwanga Kwa Waliongizani.
Kazi ya huyu Malaika huwatoa watu walio ngizani Waliofungwa kiufahamu au kifikira yeye huzifungua fikira zao nakujua wanapokosana na Mungu.

7;Huyu ndiye alishuka kwa kipindi cha Elisha wakaona Jeshi kubwa Malaika lilikuwa kundi la Malaika URIELI..


JINSI YA KUMTUMIA.
.
Muite aje katika kipindi ukiwa unavurungwa na kuchanganywa na Vitu mfano upo unayumbayumba huna utulivu mara akili inavurungwa upo kipindi kisichoelezeka huyu Malaika Anadili na Mfumo mzima wa ufahamu wako akiingia ataweka vitu Sawa.


OMBA HIVI.

Anza na Kuimba Tenzi au Kuabudu.
Hakikisha umekaa uweponi.

ANZA KUMWAMBIA.

Malaika mkuu URIELI Nakuita uje utilize akili yangu moyo wangu bado sioni mbele yangu nakabiliwa na mambo mengi mpaka yananichanganya akili yangu katika Jina la Yesu.Amen ×4


Malaika Wa Moto URIELI Shuka uteketeze taka zote zilizokamata Ndani yangu shambulia kwa Jina la Yesu.Amen ×4


Malaika URIELI Malaika wa Vipawa Inua vipawa ndani yangu inua huduma ndani yangu katika Jana la Yesu.Amen ×4


Mtumìe huyu Malaika AJE ASHUGHULIKIE ufahamu Akili yako iliposhindwa.


Share Somo hili Nzuri.

Alhamisi, 3 Aprili 2025

SOMO MITENGO MITATU MIKUBWA

SOMO; MITENGO MATATU MIKUBWA SHETANI ANAYOTUMIA KUTESA WATEULE WA BWANA:

Hili Somo naletewa nikufundishe ujifunze kitu wakati  mwingine ili uwe  mshindi wa maisha yako jitaidi  kumjua adui yako mbinu mbalimbali anazozitumia kukushambulia wakati upo na Yesu. Itakusaindia hii.

1:MITENGO MKUBWA SHETANI HUTUMIA MANENO UJITAMKIE UDHAIFU au UTAMKIWE UDHAIFU. HESABU;30

Mfano: Hivi mawasiliano yako na mpenzi wako yanaendaje..? HUU NI MTENGO WEWE pasipo kujua unasema.

Mawasiliano saivi ananitafuta mara moja moja kikweli haya mahusiano siyaelewi.

Adui Anakunasa MAHUSIANO SIYAELEWI Hakika hutakuja kuyaelewa .

Mfano: Unatoaga zaka ?
Yaani Mwezi huu sikutoa na madeni na mama mgonjwa 

Adui anakamatia hapohapo kuongeza shida ili usitoe.

IPO HIVI KILA  MANENO UKIONGEA MABAYA  YANA Roho nyuma yake hufanya iwe hivyo ukijinasua kwenye mtengo huu ujue unielewe kweli.

2:MITENGO WA PILI NIKUZIMA MOYO WA UTOAJI WA ZAKA AU KUTOA KWA KUDANGANYA KIASI SAHIHI. 
Malaki:3:8-11 Matendo 5.

Shetani anajua wapi akikushikia huwezi kuona matokeo kama atakuacha uwe mwaminifu wa zaka atakamata kinywa chako kiwe kinajifunga nakujinenea matatizo.

Shetani anajua Mungu hupenda watu wanaomheshimu kwa zaka na Mali zao zinapeleka injili mbele ya Bwana Yesu.

NINI HUKiFANYA.

1:Kuhakikisha Anakupa mawazo unatoa zaka kwa ajili ya jambo fulani Bwana atende siyo unatoa kama sheria na upendo kwa Mungu wako.


2:Kuweka Uvivu na Upuuziaji usitowe zaka.

3:Kuleta matatizo upatapo hela ya Kutoa zaka matatizo ndiyo yanatokea kumbe linaitaji limiriki ufahamu wako na moyo wako.

4:Utaongiwa roho ya wizi wa zaka hata kama ulikuwaga mwaminifu wa zaka.
Lengo Afirisi biashara aharibu kazi yako watoto familia mke au mme nk

Uonapo haya ujuwe umeshakamatwa na shetani.

Hakikisha unainga mfano wa Matendo:10



3:MTENGO WA MWISHO KUUA KIU YA KUOMBA UTARUDI NYUMA KIMAOMBI

Wapo Watu walikuwa fire 🔥 fire katika maombi lakini saivi wamepoa kumbe katika roho wamekamatwa wanatumikishwa adui ili aviharibu vitu vyao.


TUFANYE NINI SASA SISI

Kama Mtoto Wa Mungu chochea Maombi usikubali kuimba Fungu la Kumi  Pia Usijitamkie matatizo jitabirie mazuri usijinenee uchawi kuwa umelongwa usiseme mapepo yamezuia nisiowe au kuolewa kinywani mwako toa panda mbengu njema kwa kutamka mazuri.

Kwa kufanya hivi utajinasua kwenye mitengo ya shetani mingi Lakini yaitaji umakini mno na unaweza kuniuliza inbox kama unaswali.

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 

Jumamosi, 29 Machi 2025

UCHUMBA MASWALI NA MAJIBU

UCHUMBA MASWALI NA MAJIBU 

=======:::::::::=====+++++++====
1:Baba shalom Naitwa Farinda,,, samahani naomba kuuliza ivi nikitaka kufanya maombi nijue mtu sahihi wa kuolewa naye inabidi nifanyaje?

MAJIBU YAKE

Kwanza Futa Akilini Mwako Usiwe na mtu.
Omba mwambie Mungu Naomba umlete mume wangu umri wangu wa kuolewa/Kuowa umefika popote alipo namcharaza fimbo fimbo Aje haraka wiki hili Nionane naye Awe Amenyoka awe Na hofu ya Mungu kama mimi ninavyokupenda Katika Jina la Yesu.Amen 
Simamia Mithali;31:10


2;UCHUMBA MASWALI NA MAJIBU.
==========:::::::::::=======
Bwana Yesu Asifiwe Naitwa Tute Baba Yangu Pole kwakweli mabint unatusaindia mno..
Baba kwe hili swala LA kuomba MTU sahh kwakwel nichangamoto mno   mm wakat fulan nilikutana nakijan flan ambae nimtumishi wa Mungu  hyu kijan  Kna wakat alikuw anatembelea  nyumba hadi nyumba kjua washirik wake cku hyo alinikta nyumbn  wengne walikuw hawapo  wakat pale wanauliza mambo yakuombea nilitaka baadh bt aliniuliza una mchumb elim yako  nakadhalik ukwel nilijiuliza kwann ananiuliza maswal hayo  na hata nilipokuw nakutana naye alikuw ananichangamkia xna na ata wakat mwengne akiniona ananiangalia xna    nikimuangalia anakuw anaangalia then anaangalia pemben  lakn cku ambayo piah nilishangaa  ni cku ambayo tulikuw na ckukuu yavibanda(makambi) Ka ilivyo kwa kila mwaka wasabato yy alikuw anatufundisha somo la uchumba  kwa vijan nilivyokja nilikuw nimechelewa nikakta wapo kwe Yale maombi ya minyoror ingawa bado walikuw hawajaanza kuomba alivyonionat  alini niita yan ww ndo una kja njo hapa  nikaenda  akawa amemuachia MTU mkono nikaingia pale akanishik mkono   hudum ikaendelea  lakn wakat huo wakaw wa nakja wengne akawa anawaambia ingien kwe  mraba   namengne mengi ukwel  nimchungaj ambae niliamin  huenda ndiye mungu alieniandalia ingawa hajanitongoza bado tpo Ka marafiki mana cku zilivyoenda alihamishwa nakupangwa mtaa mwengne  cz pale nikam alikuw filid cz ndo alikuw amehitim chuo ?

swali baba ang iv nnavyoomba kwa ajil ya MTU hyu nakosea ?

 Maan mm naona Ka Kuna vikwanzo flan  shetani anavizuia  Coz ata mwaka Jana alikuja huku moshi kulikuw na maazimisho ya miak hamsin ya dini  na huku  sa walikuja wachungaj mbalimbali nayeye alikuwepo   yan nilishangaa yupo nyum yang wakat anasalimia watu wengne anaojuana nao mm alikuw  ananipga macho  But Kama mchungaj halafu kijana  inakuwa nichangamoto  eti kaja na kunisalimia halafu mbele zawatu wengi alikuja akasimama akaniangalia then akaondoka nihistoria ndefu BUT  ukwel Mungu angeruhusu  hili litokee  nafurahishwa Sana jinsi anavyotumika shambani mwa Bwana.

MAJIBU YA SWALI HILI.
Ansate Sana Kwa Swali Nzuri Na Mabint Wengi Wamekuwa Natabia hii wakimuona kijana au mtu anawaonesha Upendo anawachangamkia au Kuwasalimia kwa bashasha Akili zao na mioyo yao inaanza kuvutiwa taratibu Mwisho Wa Siku Wanaingia Maombi Kumuomba Mungu Awape Mume Lakini Akili zao Zinamtaka yule wa kanisani kwa kuwa humchangamkia nakumsaindia Akija Kuomba ataomba Akiwa Anatengemea Atakuja Kumtongoza ndiyo akutane na Mchungaji Asiye elewa Protoko za Mungu kukupa mume atakuambia huyo ni mumeo kumbe siyo ukimpata wa hivyo huyo unakuwa umejipa kwa Akili Zako.

MADHARA YAKE.
1;Mtazini kabla ya kusudi la ndoa kutimia.

2;Ukiingia ndani ya ndoa  utapitia maumivu na machungu ndani ya ndoa utachukia kwanini uliolewa.


3;Kiuchumi utashuka Mungu huwa habariki palipo na uchungu palipo na maumivu ya moyo palipo na manug'uniko Haya maisha itakuwa sehemu yako.


UFANYE NINI SASA..?

Subiri Mungu akupe hata kama atachelewa atakuja tu Acha Kijana Kuwa na Harakaraka. Unatazama Umri Mungu anajua hilo.

Bora ndoa yenye Furaha milele Kuliko yenye machozi milele.


JIUNGE Kwenye Group la Maombi na Mafundisho upate masomo yakuponye +255710889892
Pastor Richard Wa Morogoro

Jumanne, 25 Machi 2025

NDOTO ZA SHULENI

NDOTO  ZA SHULENI NA MAANA ZAKE.

Karibuni Sana LEO Tuone Ndoto za Kuota Shuleni Na Maana Zake.

Ndoto huwa ni Taarifa Unayojulishwa jambo linalokuja au lilopita au lilopo

Ayubu;33:14-15 

1:Ukiota Upo mazingira ya shule ya msingi na Unifom

👉👉Unajulishwa Umefungwa Usifanikiwe waitajika uombe kukemea hiyo roho.


2:Ukiota Upo shuleni unamwagilia mimea

👉👉Unajulishwa Watu Utakuwa unawafanyia kazi wezako wanafanikiwa kwa ulicho nacho wewe hutafanikiwa.


3;Ukiota Upo Palendi(Mstarini

👉👉Unajulishwa umeuganishwa na roho ya Kusimama katika hatua zako zisisonge mbele uombe uikatae hiyo roho.


4:Ukiota Upo Unacheza na Wanafunzi wezako shuleni

👉👉Unajulishwa Utateseka kwa Kuwa mpuuziaji wa vitu katika maisha yako.


5:Ukiota Upo shuleni Mwalimu anafundisha wewe huna daftari au Kalamu

👉👉 Unajulishwa Huwezi Kuweka Kumbukumbu Ya Vitu unavyoelekezwa au Kushauriwa ndiyo sababu hufanikiwi


6:Ukiota Unalia Upo maeneo ya shuleni

👉👉 Unajulishwa Unauchungu Kwakuwa Mambo hayaendi mbele kama utakavyo


7:Ukiota Upo shuleni mnafanya Mtihani wezako wanakusanya wewe Upo TU 

👉👉Unajulishwa Huwezi kutatua changamoto unazopitia mpaka usaidiwe ndio utavuka kataa hiyo roho.


8: Ukiota Upo Kwenye chumba Cha Mtihani hujagawiwa Karatasi Wezako wamegawiwa

👉👉Unajulishwa Karibuni Utakutana na changamoto kabla haijakukuta Omba Kemea


9:Ukiota Upo Darasani unafundishwa somo la Hisabati

👉👉Unajulishwa Huwezi kufanikiwa Sababu huna malengo wala mikakati.


10:Ukiota Upo Darasani mnapiga Kelele Mwalimu anaingia

👉👉Unajulishwa wewe unamaneno mengi SI mtendaji wa unachokiongea ndiyo maana huendelei. Omba kemea ndoto hiyo.


11:Ukiota Upo Shule ya O,level

 👉👉Unajulishwa Unamwaga wa Kufanikiwa lakini Waitaji mtu mwenye hekima akuongoze kufikia mafanikio yako


12;Ukiota Upo High School mpaka chuo

👉👉Unajulishwa Unamafanikio lakini jishughulishe na kitu Mungu atakibariki.


13: Ukiota Upo unasoma na Wanafunzi wa chuo lakini wewe hujawahi Kufika au Kusoma chuo

👉👉Unajulishwa Mafanikio yako yaitaji ukae na watu waliokuwa kiroho na kielemu utafanikiwa


14: Ukiota Upo shuleni unakula

👉👉Unajulishwa matatizo yako Yanayokutesa uliyapata ukiwa shuleni.


15;Ukiota Upo shuleni lakini maeneo ya chooni au Bafuni Ndoto ikaja hivyo

👉👉Unajulishwa Ulikanyaga Dawa ukiwa shuleni Mungu Akakukinga nazo hazijakuzuru lakini Waitaji uombee kukemea roho hizo.


16:Ukiota Upo Darasani unawafundisha wezako Mwalimu nae amekaa

👉👉Unajulishwa Utafanikiwa Kile ufanyacho Kupitia kuwasaidia watu wegine.


17:Ukiota Upo O,olevo au High school Unafundishwa na Mwalimu Wa chuo

👉👉Unajulishwa Upo unakwama kusonga mbele Kwakuwa unaitajika ukae na mtu aliyekuwa kiroho au aliyefanikiwa Kimwili ndipo utatoka kwenye pito Hilo.


18:Ukiota Upo shuleni umevaa nguo za nyumbani

👉👉Unajulishwa Unapenda Kujifunza na Kutafuta mafanikio lakini Tabia hubadiliki Unapaswa ubadilike Tabia yako Utafanikiwa


19:Ukiota wewe Ni Mwalimu Upo unafundisha shuleni kwako

👉👉Unajulishwa roho ya kutumikishwa hutaendelea kwa Kuwa unatumikishwa kila utakalokufanya. Uombe kemea


20:Ukiota wewe Mwalimu umeitwa na mkuu wako akakufokea

👉👉Unajulishwa utaitwa na mkuu wako atakuonya 


NDOTO ZA SHULENI WALIZOOTA WATU ZA MASHULENI


1:Bwana Yesu asifiwe baba.Naitwa Happy Nipo Njombe Samahani naomba kujua maana ya hii ndoto nimeota usiku wa kuamkia Leo. Nimeota tulikuwa kwenye shule ya msingi niliyosoma tulikuwa Mimi na rafiki yangu, tumeenda kufundisha darasa la kwanza lakini tulipofika darasani tukamkuta mwalimu mwingine anafundisha na zilikuwa zimebaki dakika kumi na Tano tu muda wa mapumziko ufike basi tukawa tunaondoka. Lakini wakati tunaondoka tukapita nyuma ya majengo ya shule tukawa tunaona Kuna uchafu mwingi karibu kila sehemu tuliyopita kulikuwa na kinyesi Cha binadamu. Je hii ndoto Ina maana gani baba?? Inaninyima raha kabisa.


MAANA YAKE

Unajulishwa unarundishwa nyuma kiroho na hatua za maisha yako kupitia kukosa marafiki sahihi.


Tengeneza list ya watu unaoongozana nao Muombe Mungu akupe.